Msaada wanaJF,
Nahitaji dawa ya kutibia ugonjwa wa pua kuziba ila nikipenga kamasi hazitoki. Mara nyingine pia husababisha maumivu ya kichwa hasa katika paji la uso. Wenzetu wa Tanga ugonjwa huu huuita kambako(u).
tukijua unaishi wapi tunaweza kukusaidia .
Jaribu kuchemsha maji moto halafu weka vicks kwenye hayo maji na ufanye kama unaji steam uso, au unajifunika na kitambaa usoni halafu unavuta hewa ya hiyo maji, pole sna kumbuka kwenda hospitali
Inawezekana uko mikoa yenye mawingu mengi. Huu ulinisumbua sana nilipokaa Arusha na Tanga hasa sehemu za milima.
Kama sikosei utakuwa na ugonjwa wa Low Blood pressure.
Dawa nzuri jaribu kubadilisha mazingira kama unaweza na nenda mikoa isiyo na milima na mawingu. Unaweza kukuta hiyo shida imeisha. Mie nimesha apa nikipangiwa kazi Arusha siendi. Labda niende kutembea au kupita ntavumilia pua kuziba na kichwa kuuma na kama sikosei mishipa usoni inakuwa imesimama,,,,,,,,,,,,,,,,
Nenda umuone Dr na atakupa maelezo zaidi.
Je kwenye familia yenu mna wagonjwa wa Asthma??
kwanza kamuone Daktari ili ujue tatizo ni nini.Hii tabia ya kukimbilia dawa kabla ya kujua tatizo lilisababishwa na nini ni hatari sana.
Nadhani unaumwa POLYPSE ni vinyama vinavyoota puani na ukiwa alergic kwa vumbi au baridi basi vitabana na kuwasha sana. Nakushauri uende kwa Dr moja kwa moja manake huwa wanatoa dawa lakini vikiwa serious sana wanafanya minor operation na kuvichoma au kuvikata. Pole sana mkubwa!
Inaweza isiwepo lakini ikaanzia kwako, so sio mbaya ukaenda kuicheki piaKuna ukweli kiasi kuhusu unayosema, nipo Dar ila kukiwa na mawingu ni kweli hali inazidi kuwa mbaya. Kuhusu Asthma hakuna case hiyo kwetu. Thanks for caring!