Msaada wa tiba ya kifua cha mtoto kisichopona

Yajoh

Member
Jun 5, 2020
31
27
Habari za hapa,

Mwanangu ana umri wa miaka sita anasumbuliwa sana na kifua ambacho hakiponi, nimejaribu kumpeleka hospt lakini hakijawahi kupona zaidi ya kutulia kwa siku kadhaa.
 
Kumekuwa na changamoto kubwa kwenye kutibia matatizo ya kifua/kikohozi kwa watoto. Hii inatokana na watoto pia kuwa kundi ambalo si rahisi kufuata taratibu zinazotolewa ili kuleta uponyaji.

Kuna vitu vya kujuuliza kwanza:
1: Je kuna watu wenye asili ya mzio/ allergy kwenye familia?
2: Je mtoto anapokohoa anakuwa na homa?
3: Je mtoto alizaliwa akiwa njiti?
4: Je mtoto alinyonya bila kuchanganyiwa chakula kwa miezi sita ya mwanzo?
5: Je mtoto akikohoa anatoa makohozi?
6: Je mtoto anakohoa zaidi wakati gani?
7: Je uzito wa mtoto unaendana na umri wake au umeshuka?
8: Je mtoto anatumia feni au kiyoyozi wakati wa kulala?
9: Mtoto anatumia sana vitu hivi?
A:Baridi
B: Rangi: Ice cream, ubuyu, juisi za viwandani, blue band,
C: Nyumbani kunamifugo
D: Dhulia lako nyumbani vs sofa
Mwone daktari wa watoto ili uweze kung'amua mahusiano ya vitu tajwa hapo na kikohozi cha mtoto. Pamoja na mengine mengi na tiba mahsusi.
 
Asante kwa ufafanuzi na maswali yako, nitamuuliza mama wa mtoto ili niweze kujibu zaidi maswali

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Habari za hapa,

Mwanangu ana umri wa miaka sita anasumbuliwa sana na kifua ambacho hakiponi, nimejaribu kumpeleka hospt lakini hakijawahi kupona zaidi ya kutulia kwa siku kadhaa.
Pengine luna chakula au mazingira yanayompa allarge

Chukua kijiko kimoja cha asali mbichi changanya na mdalasini mlambishe kila siku kabla ya kulala

Lakini pia jaribu kuchunguza chanzo cha hicho kifua, kama ni allarge jaribu kuepuka vitu vinavyomsababishia lets say chakula, vinywaji, na hato vumbi au harufu kali kama perfumes, mazulia ya ndani yasafishwe mara kwa mara na nguo zake zikauke vizuri kwenye jua na kupigwa pasi

Epuka vity vyenye sukari na rangi kama juice za dukani, ice sugar, biscuits na chocolate, pia epuka maziwa ya ng'ombe kama inawezekana go for maziwa ya kopo, epuka mayai ya kisasa pia mara kwa mara
 
Maelezo ya mamake ambaye alikuwa anaishi nae ni kuwa toka yupo mtoto kifua kilikuwa kinamsumbua
Kinaweza kutulia kwa miezi labda minne hv kisha kaanza kukooa tena, mwanzoni makohozi yalikuwa hayotoki ila kwa sasa yanatoka baada ya kumpa dawa.. vitu vya rangi labda kama atakuwa anakula shuleni

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Binafsi nilikumbana na hiyo changamoto, mtoto tukampatia dawa za kikohozi, minyoo, mpaka na Antibiotic ila tatizo likawa linajirudia kila baada ya siku chache.

Nikashauriwa nimwanzishie dozi ya Kitunguu swaum unakitwanga kisha unachanganya na asali, unampa asubuhi na Jioni kwa muda wa siku saba. Alipona mpaka Leo hakimsumbui, Mungu mkubwa!
 
Asante , nami nitajaribu kumpatia hio dawa then ntaleta mrejesho wake

Back
Top Bottom