Msaada wa tafsiri ya ndoto ya kurudi shule mara kwa mara

chaz beezz

JF-Expert Member
Nov 26, 2020
217
841
Habari Wana Jamiforums natumani mko poa kabisa.

Kuna ndoto moja ina inanitesa Sana nimeona bora leo nilielezee hapa jukwaani angalau niweze kupata ufafanuzi kidogo kuhusiana na ndoto hii ninayo ota ikijirudia Mara kwa Mara kila Napo lala usiku.

Nimuda Sasa yapata Kama miaka Saba tangu nihitimu elimu ya sekondari lakini licha ya muda mrefu kidogo kupita tangu nimemaliza kidato Cha nne nimekua nikiota ndoto zikionesha kuwa nimerudi shule nasoma pia mazingira ya shule ni yale yale walimu wanafunzi wenzangu pia niliosoma nao ni wale wale.

Kiufupi naota ndoto hii imekua ikijirudia Sana na siku zinavyozidi kwenda nazidi Kuota hii ndoto na chaajabu ndoto hii uonesha kua nimerudi shule na wenzangu nimekuta wanaendelea na masomo Kama kawaida huku me nikionekana nilikua mtoro sihudhurii masomo yanayoendelea kwa Sasa katika kipindi icho ambacho Mimi nipo uraiani nimeshamaliza shule.

NB.
- Ndoto zote naota nipo tu sekondari wala sio shule ya msingi ama chuo

- Ndoto nyingi huwa naota nikiwa katika kipindi Cha kutaka kuadhibiwa wa mwalimu au kuhaibishwa mbele ya wanafunzi wenzangu

- Kwa mwezi naweza ota mara2 hadi tatu ndoto za aina hiyo ya kurudi shule.

kwa anaejua maana ya ndoto hii wakuu anisaidie tafsri yake Nini na kwanini ijirudie Mara kwa Mara ndoto Aina moja, inanitesa Sana kiukwel wakuu nakosa Raha naposhtuka usingzini baada ya Kuota ndoto hii na kichwa uwa kizito Sana. Nifanyeje ili niweze ondokana na ndoto hii?
 
Mwl Mwakasege amewahi zungumzia ndoto ya namna hii

Shule maana yake ni sehemu ambayo unaenda kwaajili ya kufanya maandalizi ya wakati ujao au kitu kinacjotarajiwa. Mwanafunzi anapoenda darasani maana yake anaenda kujiandaa na ujuzi au taaluma flan kwaajili ya matumizi mbele ya safari yake ya kimaisha.

Sasa unapooneshwa upo darasani maana yake kuna sehemu ulizembea/tegea katika maandalizi ya msimu ujao, hivyo unakumbushwa ujiandae.

Pia unapoona mazingira ni yale yale na wanafunzi ni wale wale maana yake umekwama katika maandilizi flan, ndio maana huoni ukienda hatua ya mbele katika ndoto hiyo ya darasani!

Kama wewe ni mkristo na unaamini katika mafundisho wa Mwl Mwakasege, Tafuta hilo somo la ndoto litakusaidia!!
 
Kama vipi rudi shule kasome, hutakuja kuota hizo ndoto.

Badala yake utaota ndoto umemaliza chuo na umedaka kitengo nyeti unakula mema ya nchi unapush ndinga kali na upo kwenye mjengo wa maana.

Oya mzee baba usinisahau ukifika huko
pamoja mkuu
 
Hizo ndoto ni za kuzipuuza mara nyingi ni kumbukumbu ambazo zina rotate kwenye ubongo wako there is nothing behind
Napojaribu simulia watu baadhi Yao huniambia Wenda nachezewa mkuu na Mimi siamini Sana katika Mambo hayo
 
Mwl Mwakasege amewahi zungumzia ndoto ya namna hii

Shule maana yake ni sehemu ambayo unaenda kwaajili ya kufanya maandalizi ya wakati ujao au kitu kinacjotarajiwa. Mwanafunzi anapoenda darasani maana yake anaenda kujiandaa na ujuzi au taaluma flan kwaajili ya matumizi mbele ya safari yake ya kimaisha.

Sasa unapooneshwa upo darasani maana yake kuna sehemu ulizembea/tegea katika maandalizi ya msimu ujao, hivyo unakumbushwa ujiandae.

Pia unapoona mazingira ni yale yale na wanafunzi ni wale wale maana yake umekwama katika maandilizi flan, ndio maana huoni ukienda hatua ya mbele katika ndoto hiyo ya darasani!

Kama wewe ni mkristo na unaamini katika mafundisho wa Mwl Mwakasege, Tafuta hilo somo la ndoto litakusaidia!!
Zingatia hapa. Nakazia.
 
Spiritual wanasema ndoto hizi ni dalili za spirit of delay au kurudishwa nyuma

But watu wa universe pia wanasema ndoto hizo hua zinakuja mara nyingi ukiwa na jambo either linakutatiza au unataka kufanya maamuzi but hujui namna ya kufanya

Ukiweza tafuta vitabu vinavyoelezea conscious na subconscious mind cinaelezea vizuri sana
 
Mimi nilikua naota Sana nafanya mitihahi chuo..na simalizi. Siku niliyoota nimemaliza kabla ya wenzangu ndiyo ilikua mwisho wa kuota hiyo ndoto

Sasa zimekazana za shule ya sekondari, mara naenda hostel ya o level kukaa..mara nipo na marafiki wa sekondari. Jana tu nimetoka kuota nipo na marafiki wa chuo na sekondari pia ila tumevaa uniform za o level..mweeeeh

MUNGU atupiganie tu
 
Kak hyo ndoto hiyo imeniteza San na nimekuja kugungua tafsir zake siyo ndoto nnzur hyo ..hyo ndoto inakupa alert kuwa utarudi nyuma sna ktk mambo yako wew so jipange San kuzikabiliana nazo usichukulie POA kirahis mm inafika naota ndoto imefana na yako Ni nwanafuz wa kdg Cha nne na au Cha sita wachuo cjawai kuwaota ila Hawa wa fom 4 n 6 nimewaota San Niko nao darasani

So jipange mnk hyo inakuonesha Kuna maswal yako yatarudi nyuma San hvyo Anza kuonmba na Toba pia huku ukihakiksha unasali sna

Mm ikipita mwezi sijaota wanafuzn wenzangu bas namshukuru mungu San na Mambo yangu yanakah mkao Ila nikiwaota tu lzm siku zinazofta Nile loss au shot hatari .kwa ujumla sipendi ndoto za namna hyo
 
Mimi nilikua naota Sana nafanya mitihahi chuo..na simalizi..siku niliyoota nimemaliza kabla ya wenzangu ndiyo ilikua mwisho wa kuota hiyo ndoto

Sasa zimekazana za shule ya sekondari..mara naenda hostel ya o level kukaa..mara nipo na marafiki wa sekondari..Jana tu nimetoka kuota nipo na marafiki wa chuo na sekondari pia..ila tumevaa uniform za o level..mweeeeh
MUNGU atupiganie tu
Amen🙏
 
Back
Top Bottom