Msaada wa suggestions za broker responsive DSE

JATU idea yao ni nzuri na bidhaa zao hata miaka 100 zina soko, issue ni business model walioiichagua.

Sioni kama ni sustainable maana ni ponzi scheme
Hawa jamaa nililiwawazia sema sijampata muda wa ukiisoma business model yao so nime-refrain from buying. Ila kama wasemayo ni kweli basi hii ni nuksi!
 
Kwwa mawazo yangu ni heri ununue treasury bonds kuliko kusubiri dividends. Treasury bonds ni risk free wakati kupata dividends sio kitu cha uhakika. Chukua mfano wa TCC, share price ni shs 17,000 na dividends kwa share mwaka 2019 ni shs 300. Assume hii itaendelea mpaka 2020, ni sawa na return ya 1.76% kwa mwaka. ambayo ni ndogo mno. Ukiangalia hapa, utaona kuwa Treasury bonds ya miaka miwili unapata 7.82% kwa mwaka. Naamini kuna benki ambazo wanatoa interest kubwa kwenye fixed deposit kuliko ya Treasury bonds. TPB walikuwa wanatoa 12% per annum, sijui kama wanaendelea. Fanya utafiti.
Kima cha chini cha kununua treasury bonds ni kiasi gani?
 
Tsh 1m in multiple of 100,000.
Asante.

Considering wanafanya kwa mnada haina guarantee kuwa utapata sio?
Plus kuweka 1/5m for 5/10/15 years unaona Ina make sense maana naamini wengine wananunua shares since they can't afford kutoa a million at a go
 
NMB iko vizuri sana, mana government inaitumia kwa transactions zake, so projections zake ziko vizuri, ila nahc wengi wamenunua shares (good projections=high demand of shares, ndo mana bei yake ni kubwa), na kama nyng zimeuzwa, dividend value per share inakuwa ndogo.

Kwa CRDB, projections zake nimeona kwa web flan bei kufika 220Tsh, zinaweza kuwa nice buy, lakini benk haina back up nzuri sana.

Ikumbukwe, dividends value ni amount ya profit gawanya kwa idadi ya shares...
Mi nataka kununua share kwa style yangu ya kipekee ambao sitakuwa nategemea dividend. Hebu typos link ya hiyo web tukajionee.
 
Mi nataka kununua share kwa style yangu ya kipekee ambao sitakuwa nategemea dividend. Hebu typos link ya hiyo web tukajionee.
Naona jamaa walikuwa sahihi na projection ya CRDB, at that time price ilikuwa 185, now iko 215, bado Tsh 5 tu, projection yao iwe 100% true.
Screenshot_20210113-174211.jpg
 
Won't that make CRDB lose more value?
Hapana, kuexpand na kufungua matawi, means capital imeongezeka, na hyo inamaanisha pia productivity imeongezeka, na consequently profit inaongezeka. Share value itapanda kama profit ya kampuni inaongezeka, mana investors tunatazama profit ya kampuni tunayoinvest
 
Kwa investor sikushauri kuweka hela yako NMB, kwanza Capital gain ni kama haipo.. price imeganda sehem moja mwaka mzima. Devident wanatoa lest than 6% ya share price.. ukitaka kuuza share za NMB utasubir mwezi mzima.. Kwa CRDB n tofauti Bei zinachanga sana sana yani.. mtakua mashahidi ni Juzi January tu bei zilikua 215 na wiki jana imefika 300. devident wanatoa 10% kupanda juu.. pia ukitaka kuuza ni muda wa masaa tu zishauzika. kwa broker binafsi namtumia Solomoni Brokers wako active zaidi whatsapp na insta, japo nimeona kuna wanaoitwa Orbit wanasemwa vizuri pia.
 
Nifanyie mpango wa list ya companies wanatoa divident ya walau 10% ya share price
 
Back
Top Bottom