Msaada wa sheria za kazi kwenye madai yasiyo na mkataba

mzushi flani

JF-Expert Member
Jan 20, 2020
1,627
2,466
naomba nifike moja kwa moja kwenye mada.

naomba kufahamishwa kama kuna sheria inaweza kunisaidia katika kupata madai(malipo) yangu.

kuna sehemu nilifanya kazi toka tarehe 15 mpka tarehe 30 ya mwisho wa mwezi kwa makubaliano kua ningepewa nusu ya mshahara na baada ya hapo tungeanza kupeana mshahara kamili na mkataba vilevile, ila ilivofika tarehe 2 mwezi uliofata, nikaacha kazi baada ya kujua kua wana uswahili mwingi na hawakua na lengo la kutoa hata mkataba achilia mbali kua wanachelewesha mishahara mpaka miezi miwili au mitatu kabisa, na yenyewe unaweza kupata nusu.

sasa wakuu naomba kufahamishwa sheria itakayonilinda na kutumika, ama hatua za kuchukua ili kupata madai yangu ya siku 15 hizo nilizozifanyia kazi maana napigwa kiswahili mwezi wa pili huu.

NB: hata hao wafanyakazi wengine nliowaacha wanadai pesa nyingi na hawana mikataba vilevile.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom