TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,507
- 11,252
Wakuu nina swali naomba mnisaidie, Hebu chukulia unatoka Dar kwenda Arusha: kufika Chalinze ukasimamishwa na trafki akagundua kuwa huna Fire Ext, ukalipishwa faini kwa hilo kosa, je ukikutana na Trafiki mwingine kwa mfano Segera akakubana kwa nini huna Fire Ext. ilhali umeshalipishwa faini. Je huyo Trafiki ana haki kisheria kukulipisha faini nyingine? au una haki kisheria kutumia risiti ya mwanzo kujitetea kuwa umeshalipa faini kwa kosa hilo hilo na ukifika mwisho wa safari basi utalishughulikia kosa lako?