Msaada wa sheria za barabarani (Madereva) !!

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,502
11,248
Wakuu nina swali naomba mnisaidie, Hebu chukulia unatoka Dar kwenda Arusha: kufika Chalinze ukasimamishwa na trafki akagundua kuwa huna Fire Ext, ukalipishwa faini kwa hilo kosa, je ukikutana na Trafiki mwingine kwa mfano Segera akakubana kwa nini huna Fire Ext. ilhali umeshalipishwa faini. Je huyo Trafiki ana haki kisheria kukulipisha faini nyingine? au una haki kisheria kutumia risiti ya mwanzo kujitetea kuwa umeshalipa faini kwa kosa hilo hilo na ukifika mwisho wa safari basi utalishughulikia kosa lako?
 
Ukishalipa hiyo moja na ukapewa risit basi tumia hiyo hiyo na ukifika karibu na maduka nunua, kimsingi ukilipishwa faini inakubidi kabla ya kuendelea na safari basi uitafute na kuinunua!
 
Ukishalipa hiyo moja na ukapewa risit basi tumia hiyo hiyo na ukifika karibu na maduka nunua, kimsingi ukilipishwa faini inakubidi kabla ya kuendelea na safari basi uitafute na kuinunua!

Sheria inasema huwezi kuadhibiwa mara mbili kwa kosa moja, ukilipa faini kwa njia ya notification ni kuwa umekubali kosa na umepewa adhabu na umeitumikia kwa kulipa faini. Hivyo kwa mtazamo wangu unaweza kuamua kutembea bila fire extiguisher mpaka wewe mwenyewe utakapoamua
 
Mkuu Ngambo Ngali,

Mimi natofautiana na wewe kwa suala dogo kwamba hiyo fire extinguisher ni kwa faida yako na ni tahadhari kabla ya hatari ya moto kutokea. Ni heri ukanunua hiyo FE kwa kuwa hiyo risiti ya faini haitakusaidia kuzima moto endapo utatokea kwenye gari lako. Yatupasa kufahamu kwamba moto unaweza kudhibitiwa kwa urahisi ndani ya dakika kumi tu za mwanzo. Na yatupasa kufahamu kuwa kazi ya polisi wote pamoja na hawa wa barabarani ni kuhakikisha sheria tulizojiwekea tunazifuata kwa usalama wetu na mali zetu.
 
Hujakosea hata kidogo,Nilikuwa nazungumzia kwenye legal context. Ukiangalia sana hata mimi ningekuwa trafiki nisingempa mtu notification kwa kukosa fire extinguisher sana sana ningemuambia akanunue tu hiyo "faya tingisha". Ni kama vile kumpa mtu faini kwa kutoandika pembeni jina la mwenye gari, yaani hilo kosa hata ingekuwaje haiwezi kusababisha ajali. wakati wanafanya hivyo gari lenye magururdumu yaliyokwisha linaachwa lipite tu tena likiwa na abiria kibao. In short askari wetu wa usalama barabarani hawajui kwa nini wapo pale wao wanajua kazi yao ni kushika magari na kuongoza misafara.
 
Back
Top Bottom