Msaada wa Secondary - Dar.

Steven Sambali

JF-Expert Member
Jul 31, 2008
352
170
Kwa wenyeji wa Dar,
Kuna mtoto wa kaka yangu yupo Dar na ninataka arudie mtihani wa form 4. Sasa kabla hajafanya huo mtihani mwakani nimeona ni heri asome kuanzia form 3 sasa hivi na mwakani arudie mtihani huo kama mwanafunzi wa shule hiyo au atajilipia mwenyewe na kufanya kama private popote pale pengine. Sasa kwa kujisomea mwenyewe itakuwa shida sana heri awe na wenzie.
Msaada ninaoomba ni kuwa natafuta shule nzuri ambayo ataweza kuwa anakwenda kusoma na jioni kurudi nyumbani. Ntaomba anwani ya shule na ikiwezekana ghalama zake kwa mwaka. Nitalipa CASH kuanzia huu nusu mwaka na mwakani nitalipa ada ya mwaka mzima. Naomba hii kitu haraka ili ikibidi kijana mwezi huu wa nane aanze shule. Nimeambiwa Makongo ni shule nzuri. Ila nikipata nyingine na kuamua kati ya uzuri na ghalama na hapo nitafute katikati shule ipi itanifaa na nitajiweza kulipia.
Thanx all un advance.
SSAMBALI@HOTMAIL.COM
 
Bora Wewe Unawazia Watoto Kitu Chema...! Kuna Wanaowaza Viwanja Gani Wawapeleke Watoto Wao....!
 
Bora Wewe Unawazia Watoto Kitu Chema...! Kuna Wanaowaza Viwanja Gani Wawapeleke Watoto Wao....!

Mahesabu,
Kijana ni mtoto wa marehemu kaka yangu. Nafikiri siku zote kuwa kama ingelikuwa tofauti basi na yeye angelijali familia yangu. Kwa sababu hiyo ninajisikia kuwa inabidi kumsaidia kijana na itakuwa asante kubwa kwa merehemu kaka yangu ambaye alikuwa msaada mkubwa sana wakati na mimi niko shule. Ni hiki kitu kisemwacho kuwa "ukumbuke unatokotoka..". Ukisahau basi siku moja utaishia pabaya.
Nategemea kuna mwalimu wa secondary au anayemjua mtu anayeweza kuwa msaada kwangu. Shule za pembeni pembeni poa sana si lazima zile za city Center.
 
Kuna shule inaitwa Kamene Sec. School iko Tabata kuelekea Segerea. Kuna kijana wangu anasoma huko Form V. Matokeo yake ya Form IV mwaka jana yalikuwa mazuri sana kwa shule ambazo sio za serkali. Anwani yao ni SLP 8943 Dar Es Salaam. Simu ni 255 22 280 8384.

Jaribu shule hiyo nadhani kijana atafaidika.

macinkus
 
Kaka,
asante kwa uamuzi wa kumpa jembe huyo dogo,nisahihishe kidogo kuhusu location ya kamene, kamene iko Tabata Kimanga sio njia ya Segerea,unapanda daladala la Tabata kimanga,kilipo kituo cha daladala Kimanga ndio shule ilipo(kituo kinapakana na shule).Mabasi hayo yanapitia Mawenzi.

Ni kweli ni nzuri sana,perfomance yake inapanda kwa kasi,nikupe na simu nyingine ya ziada (0754850461).Kwa kuwa leo ni jumamosi tumia hiyo mobile utapata majibu faster.
 
Huu ndo usafiri pekee wa wanafunzi wa Dar hauna bughudha.
Wanafunzi.JPG
 
Kaka,
asante kwa uamuzi wa kumpa jembe huyo dogo,nisahihishe kidogo kuhusu location ya kamene, kamene iko Tabata Kimanga sio njia ya Segerea,unapanda daladala la Tabata kimanga,kilipo kituo cha daladala Kimanga ndio shule ilipo(kituo kinapakana na shule).Mabasi hayo yanapitia Mawenzi.

Ni kweli ni nzuri sana,perfomance yake inapanda kwa kasi,nikupe na simu nyingine ya ziada (0754850461).Kwa kuwa leo ni jumamosi tumia hiyo mobile utapata majibu faster.
Ni ya bweni au day? je karo yao ni kiasi gani mkuu? Nami natafuta shule nzuri kwa ajili ya wanangu
 
Hiyo shule ni ya bweni na kutwa,ada sifahamu kwa uhakika,ila ukitumia hiyo mobile phone utapata kila kitu.

Nasema ni shule nzuri kwa sababu m/kiti wake namfahamu sana,ni miongoni mwa watu wachache wanaojua nini kifanyike.
 
Malila,
Nasema asante kwa sababu nimeongea na Ngowi na kujitambulisha kwake. Kwa sababu sipo Dar, kuna dada yangu kumbe anaishi karibu tu hapo na alikuwa kasahau kabisa juu ya hii shule. Anamfahamu pia mwalimu mmoja wa hapo. Ngowi kaniambia kuwa ada kwa shule ya mchana ni laki 5 kwa mwaka na kulala sijui ikoje maana sikuuliza.
Kanipatia simu ya pale ambayo member pale juu ameiweka na kuniambia jumatatu nipige kuongea na Mwalimu mkuu. Asante kwa msaada wenu na kweli JF si porojo tu ila ni DUNIA yetu mpya kwa sasa ambapo unapata misaada, maadaui, marafiki, wachumba, kazi nk nk.

NB: Ngowi kasema kuwa ANAKUFAHAMU.
 
Kuna shule inaitwa Kamene Sec. School iko Tabata kuelekea Segerea. Kuna kijana wangu anasoma huko Form V. Matokeo yake ya Form IV mwaka jana yalikuwa mazuri sana kwa shule ambazo sio za serkali. Anwani yao ni SLP 8943 Dar Es Salaam. Simu ni 255 22 280 8384.

Jaribu shule hiyo nadhani kijana atafaidika.

macinkus

Macinkus,
Asante kwa jina la shule na namba ya simu. Huwezi amini kuwa dada yangu anakaa si mbali na sehemu hii. Hivyo kama kijana atapata ni kuwa atakuwa anakwenda kwa mguu shuleni. Shule nasikia kweli nzuri na imefaulisha wanafunzi wengi na inasemekana inazidi kupanda.
Nimeagiza waende jumatatu kufuatilia juu ya kijana kuanza shule.
 
na pia kama ikiwezekana, usisahau kumsaidia kijana kuwa na Tuition, believe me, zinasaidia mno, na kwa dar, wanafunzi wengi wanasoma tuition.
kuna Tuition iko Mwenge, kuna mwalimu mmoja maarufu sana pale anaitwa Musa, basi hapo ni kiboko kwa taaluma
 
Malila na wengine,
Jamaa yangu alienda hapo na kukuta shule imejaa kabisa (Kamene) na wakasema hawawezi kumchukua. Ila nimeambiwa kuwa njia nzuri kwa kijana anayetaka ku-reseat mtihani ni kwamba:-
Kuna jamaa wanafanya kitu kama kozi ya kumuandaa mwanafunzi arudie shule. Unawalipa na wao wanaenda hadi kumfanyia usajili na anapata namba ya mtihani. Nasikia hii ni bora kuliko kwenda kukaa darasani na kurudia alichosoma tayari. Hii shule ni nzuri kwani wao wanadeal zaidi na Mitihani na si kusoma kama kusoma. Nafikiri hata huyu Mwalimu Musa atakuwa ni aina hiyo. Gamba la nyoka lete basi mitaa ya huyo Mwalimu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom