Msaada wa nyumba nzuri ya kulala wageni karibu na maeneo ya Hospitali ya Muhimbili

kituli one

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
408
301
Wakuu salama,

Naomba msaada wa kupata lodge nzuri na yenye bei nafuu kuanzia 20,000 hadi 30,000 maeneo ya jirani na Muhimbili hoapitali.

Mke na mwanangu wanakuja huko hospitali
 
Wakuu salama,naomba msaada wa kupata lodge nzuri na yenye bei nafuu kuanzia 20000 hadi 30000 maeneo ya jirani na muhimbili hoapitali.Mke na mwanangu wanakuja huko hospitali
Nitashukuru kama ntapata jina na mawasiliano ya lodge husika nifanye booking mapema
 
Sidhani kama maeneno hayo kuna Guest house au lodge za hiyo bei,labda hapo mitaa ya Fire na Jangwani unaweza kubahatisha...
 
Upanga hakuna lodge nyingi ni apartments na hata kama zingekuweko basi ni ghali. Ila mitaa ya kariakoo au magomeni utapata nyingi sana na kwa bei nzuri. Uzuri usafiri kariakoo-muhimbili ni bwerere hata mtu akiamua kutembea pia anaweza.
 
Kwa Muhimbili nafikiri si rahisi (sijafika huko muda mrefu) ila ni vyema kupata kutoka maeneo mengine ya karibu ambyayo kuna route za Muhimbili kama Magomeni hospital, Magomeni Mapipa, Mkwajuni Kinondoni nk.

Jamani ninyi wakazi wa Dar wenye namba za bodaboda wa Magomeni na Kinondoni mumpe itakuwa rahisi kwao kumuelekeza jamaa lodge muafaka, mlioishawahi kuuguza mnajua hekaheka za kuwa mbali na eneo la matibabu

Pia bajeti yako si mbaya.
 
Ushauri mzuri na ambao nauunga mkono ni kutafuta guest house pale Magomeni mapipa au maneneo ya fire uelekeo wa jangwani ambapo zipo Lodge za bei nzuri itakuwa rahisi kwako.

Kama unaona Unaweza kukaa kwa miezi zaidi ya mmoja basi tafuta Apartment hapo jirani na muhimbili itakusaidia sana, maana kama budget yako ni 20,000per day X 30 =600,000/- ambapo unaweza kupata.
 
Back
Top Bottom