Msaada wa namna ya kupata mawasiliano yangu ya nyuma

suley hazard

Member
May 19, 2014
61
116
Habari za muda huu wanajukwaa, poleni na shughuli za ujenzi wa taifa.

Ni takribani miezi miwili sasa tangu nipatwe na msiba wa mzee wangu kipenzi, lakini siku chache kabla ya kifo chake nilizungumza nae mambo "confidential" kwa simu yangu binafsi, ila kwa bahati mbaya, stress za msiba na kutopata utulivu wa akili nimepoteza kumbukumbu zote za kimaandishi na za kichwani kuhusu mambo kadhaa ambayo nilizungumza nae hiyo siku.

Swali langu ni je kuna uwezekano wowote naweza kupata hayo mawasiliano tena maana nimesahau sehemu muhimu sana ya maelezo ambayo ina umuhimu mkubwa katika mustakabali wa marehemu na tuliobaki pia.
 
Back
Top Bottom