Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Kuna jambo moja ambalo si wengi tungependa kulizungumzia. Lakini ninomba kuligusia hapa kwa wana jamii. Je ndoa inaweza kuwa batili iwapo mmoja kati ya wana ndoa ni muathirika wa VVU? Nikimaanisha ubatili kikanisa na kiserikali.
 
Kuvunja ndoa ya kikisto hasa kwa wakatoliki ni ngumu nafikiri haiwezekani kama kuna chance kama hiyo ni negligible, mimi nimeshuhudia watu wanapambana kuvunja ndoa imepita miaka 40 sasa wameamua kurudiana, na hata kanisa la uingereza yaani the church of England lilitokea baada ya mfalme wa uingereza kipindi hicho kutaka askofu wa rome(vatkan) kutaka aivunje ndoa yake yule askofu alikataa na hapo mfalme akaamuru waingereza wote kuasi kanisa katoliki na kuanzisha the church of enlgand ili tu apate kibaraka atakaye vunja ndoa yake na aweze kuoa mke mwingine amtakaye yeye, nahitimishs hivii.......kuvunja ndoa ni ngumu sana cha msingi kama umechoka we ni kujiondokea ukaanze maisha mengine asanteni
 
ulokole @ work...........hivi mie najiuliza kwanini akina mama ndio wanao hamaga dini sana? yaani utakuta mama kazaliwa mlutheri akaolewa Rc so akabadili( of which is not bad) huko nako akaona hakuna Mungu kwa imani utamkuta kwa mwingira kesho akiona nako hakuna dini utamkuta Agape sasa najiuliza ivi sisi wanawake tumelogwa ama ni ujinga wa kuzaliwa? kwanini sisi kila siku ni chanzo cha matatizo kwa kupenda kuyumbisha misingi ya familia?

naumia kwa hili sana tu halafu utakuta mama akiingia kwenye haya makanisa ya siku hizi kutwa kucha anakesha kanisani kusali na kutumikia kanisa anasahau familia kabisa siriaz niliona mama mmoja anamuhudumia mch kuliko mumewe hadi mume akamwambia sasa ama uende ukaish na huyo mch ama ubaki hapa nyumban na penyewe bado mama akagom ukawa ugomvi wa ajabu hadi padri kuingilia kwani mama alianza kumyima mumewe unyumba kisa tu hajaokoka jamani jamani acheni tu dunian kuna mambo........

Itakua mchungaji alianza kummega huyo mama hao wachungaji wana sound c mchezo
 
Jee, ni taratibu zipi za kufuata ili mwanandoa aliyefunga ndoa ya Kikristo kanisani aweze kuivunja ndoa hiyo kimahakama au kisheria?

Wataalamu wa Sheria tafadhali naomba mnifahamishe. Natanguliza shukrani.

Uelewa wangu wa Theology ni kuwa Ndoa ya Kikatoliki haivunjwi, it is for life mpaka kifo kiwatenganishe. Kanisa linaweza kuvunja ndoa ya kikatotliki ikiwa tu vigezo vya masharti ya ndoa vilikiukwa, vigezo hivyo vinaitwa canonical impediments to marriage. Viko kumi (10) (main) au hatua tatu za kukamilisha ndoa hazikufanyika nazo ni announcement, registration na consumation. Hatua ya tatu inabidi ifanyike within the same day of the marriage. Kuendelea na reception mpaka zaidi ya saa sita ya usiku kunaweza kuwa ni sababu tosha ya kubatilisha ndoa ya kikatoliki.
 
Hapa naona umezungumza mambo ya maana. Jee, unaweza fafanua zaidi kuhusu kigezo cha "tofauti za dini/kubadili dini"?

Mfano, inatosheleza kwamba mmoja wa wanandoa amebadili dhehebu ndani ya Ukristo? Asante!


Sasa Mkuu,
Hapa kuna vigezo ulivyovionesha kuwa kati ya hivyo ndoa inaweza kuvunjwa kisheria. Vipi kama kati ya wanandoa mmoja ana maambukizi ya VVU na mwingine hana. Haitoshei kuvunja ndoa? Au na yeye analazimika kuvumilia mpaka kufa???
 
Kuvunja ndoa ya kikisto hasa kwa wakatoliki ni ngumu nafikiri haiwezekani kama kuna chance kama hiyo ni negligible, mimi nimeshuhudia watu wanapambana kuvunja ndoa imepita miaka 40 sasa wameamua kurudiana, na hata kanisa la uingereza yaani the church of England lilitokea baada ya mfalme wa uingereza kipindi hicho kutaka askofu wa rome(vatkan) kutaka aivunje ndoa yake yule askofu alikataa na hapo mfalme akaamuru waingereza wote kuasi kanisa katoliki na kuanzisha the church of enlgand ili tu apate kibaraka atakaye vunja ndoa yake na aweze kuoa mke mwingine amtakaye yeye, nahitimishs hivii.......kuvunja ndoa ni ngumu sana cha msingi kama umechoka we ni kujiondokea ukaanze maisha mengine asanteni
Ok,naomba unisaidie kwa ili,suppose mimi ni mwanamke mkatoliki na mume wangu kanifukuza nimeondoka na kuanza maisha kivyangu,Mungu amenisaidia nimefanikiwa kwa biashara nazofanya,unfortunatelly baada ya miaka 20 Mungu ananichukua na ghafla anafika aliyekuwa Mume wangu na kudai mali nilizoacha ni za kwake kwani nilikuwa mkewe na hatukuwa na talaka,je kuna uhalali wowote katika madai yake ya kutaka kufukuza wazazi na ndugu kwenye mali nilizowaachia?Je kuna uhalali baada ya separation ya miaka 20?
 
Msaada wa kisheria jamani. nina mke tumetengana zaid ya miaka miwili. tulioana 2008 na tuna mtoto mmoja. Hatukubahatika kuwa na maelewano mazuri kwani kwao wana jeuri, pesa na mali nyingi nami sina elimu wanayohitaji mume wa mtoto wao awe nayo.

Mwez mmoja baada ya ndoa mke aliniaga anaenda Nje kusoma. sikumuelewa na alichokifanya ni kuondoka bila kuaga na akaacha pete ya uchumba na ndoa mezani.

Amerudi nimempeleka baraza la usuruhish ili tutengane rasmi.kwa sasa kesi iko mahakaman. nimempa kila kitu cha ndan. nimebaki na kitanda tu ila bado anadai kibanda changu (nyumba) iuzwe tugawane sawa. ukweli nyumba alinikuta nayo naye hakua na kazi ila kilicho ongezeka ni umeme na maji tu navyo niliuweka kipindi hayupo.

Hapo haki ikoje? na naskia fununu kwamba baba mkwe ndo anataka kuinunua ili anikomeshe. Naombeni Msaada wa kisheria wanajamii wenzangu mtoto yupo kwao ila napeleka pesa ya matunzo kila mwezi.
 
Pole sana!
Mali mlizo chuma pamoja zitagawiwa sawa baini yenu!
*mali ya mwanamke itabaki kuwa yake
*mali ya mwanaume itabaki kuwa yake labda kama mliandikishana ku share hivyo zitagawiwa sawa!

Yakupasa kusubili mwenendo wa case na utapata haki yako!

Ulifanya kosa kumpa vitu kabla ya kufata taratibu za kisheria!

mawazoni,
 
Pole sana!
Mali mlizo chuma pamoja zitagawiwa sawa baini yenu!
*mali ya mwanamke itabaki kuwa yake
*mali ya mwanaume itabaki kuwa yake labda kama mliandikishana ku share hivyo zitagawiwa sawa!

Yakupasa kusubili mwenendo wa case na utapata haki yako!

Ulifanya kosa kumpa vitu kabla ya kufata taratibu za kisheria!

Hivyo sheria ya ndoa ilibadilishwa Mimi nilidhani mgao sio lazima uwe nusu kwa nusu.
 
Ndugu, sheria ya ndoa imebainisha kwamba mali mtakazochuma wanandoa ndizo mtakazogawana pindi mkitalikiana, lakini mali ambayo uliikuta kwa mwenzi wako au alikuja nayo, itabaki kuwa yake, hvyo mahakama itakupa haki ndugu....
 
mawazoni,

Wakati unamwoa hukumwambia kuwa wewe hukusoma? au ulidanganya na akaja kugundua ameuziwa mbuzi kwenye gunia? Ni vizuri kuwa mkweli!
 
Kama uko Dar, pitia duka la vitabu vya serikali pale Jamhuri Street pale Posta ujinunulie kitabu cha Law of Marriage Act. Wakati nina kesi ya talaka na mwenzi wangu nilinunua pia nikawatembelea sana mawakili kwa ushauri (wengi dar hufanyan 10,000/= for a reasonable time of discussion) simaanishi kumkodisha bali kupata ushauri wa kisheria. wakati wa mgawanyo wa mali, kipengele cha nguvu aliyotumia mwenza katika kufanikisha kupatikana kwa hiyo mali pia huwa considered. Pia nashauri usikubali mtoto alelewe na third party (bibi au babu yake), kama mama hana uwezo wa kukaa naye na wewe una uwezo wa kukaa nae, mdai mtoto hata kama ana miaka chini ya saba.
 
Kinachoshangaza ni kuwa - unadai kwao wana "jeuri ya fedha/mali" SASA ILIKUWAJE WAKAKUKUBALI HADI MKAFUNGA NDOA??? AU ULIMDANGANYA BINTI KUWA WEWE UKO JUU - NA ALIPOGUNDUA AKAAMUA KUONDOKA NA KUKUACHIA HADI PETE YA NDOA?

Sio rahisi - mtu afunge ndoa mpeane hadi pete - halafu akuachie pete mezani................. JICHUNGUZE KASORO ZAKO KABLA YA KUDHANI NI ISSUE YA MALI NA UTAJIRI ............ ILI KUPATA USHAURI ..........sema ukweli na FUNGUKA ZAIDI:frown::frown:
 
Naomba tufahamiane ndugu. kwa comment yako nahis we ndo bamkwe wangu. vinginevyo itakuwa kweli dunian wawili wawili.
 
Back
Top Bottom