Msaada wa mawazo.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa mawazo..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jamii01, Apr 1, 2011.

 1. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Naishi kwenye nchi ya watu hapa katika kutafuta zangu nikaamua niongeze kipato kwa kufanya biashara na nyumbani (TZ) nikaamua kumshirikisha jamaa yangu amabaye ni mtu mzima na ninamweshimu sana kama mzee wangu kwamba nifanye naye biashara ukweli kila kitu kilikuwa changu hadi mtaji wote..nilichokuwa nahitaji kwake nikuweza kunisaidia kuniuzia mizigo yangu ninayotuma na kisha pesa yangu kunitumia na kuchukua malipo kiasi amabyo nilikuwa namlipa kulingana pesa inayopatikana,ukweli sikupenda kuwashirikisha ndugu zangu kwenye hii biashara yangu kwa sababu pesa ingekuwa na uwezo wa kuvunja undugu wetu ila niliwambia niko nafanya biashara na huyu mtu wakafiki..

  Shida sasa inayojotokeza huyu jamaa yangu namwambia anitumie pesa aliyoniuzia mizingo yangu ananipiga maneno tu, mara nilikuwa busy mara wateja wamenilipa kwa installment..namwambia hata kile kilichopo nitumie bado ananipiga uswahili..nimeongea naye leo kwenye cim jibu alilonipa sikutegemea kulikisikia ..kweli mie ni mwanaume lakini nikakuta machozi yananitoka..kwani mtaji wenyewe nimeupata kwa shida,naishi maisha ya shida ilinifanye serving zaidi ya yote pesa yenyewe ninyingi sana....sina uhakika kwa kuzipata tena kwa miaka ya karibuni..

  Jamani mtu wa namna hii nimfanyeje?ukweli nikija Tz hata kesho huyu jamaa nitamua au nife mimi..nyumbani hawana ubavu wa kumwambia chochote jamaa kwa kuogopa kuvunja ukaribu na bado wananiambia nisimshitaki ni vumilie lakini mie nimechoka

  Hapa nilipo nimekuwa kama na stress tupu nimekuta nimekanyaga na cim yangu gharama bila hata kujua..
   
 2. L

  Leornado JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mh pole sana, tatizo lako linawakuta watu wengi sana, kuwa makini unapofanya jambo linaloshirikisha pesa na usimuamini kila mtu.

  Cha kufanya kama mliandikiana mkataba, vunja nae fasta kabla mambo hayajawa mabaya zaidi na mwambie akurudishie vilivyo vyako muachane.

  Pia mpe muda pengine ni kweli kabanwa manake huku bongo kwa sasa hali kiuchumi sio nzuri, so unapompa mtu pesa ni kumtia kwenye vishawishi.

  Ukiona anakuzingua unaweza fata sheria, mahakamani pawe sehemu ya mwisho baada ya kila mbinu kushindwa.

  Usiwe chizi coz of money, komaa kiume bwana.
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Pesa inatafutwa tu, kama ambavyo uliipata hiyo, amini utapata nyingine pengine zaidi ya hiyo.
  Pole sana, jifunze kutomuamini mtu hasa katika mambo ya pesa.
  Kama ambavyo hukuwaamini ndugu zako ingebidi hata huyo jamaa usimuamini.
  Binadamu ni binadamu tu haijalishi mnahusiana vipi.
  Mara nyingine nafuu kumuachia ndugu yako maana hata akikuzulumu ina maana pesa bado ipo ndani ya ukoo itapunguza shida za yeye na familia yake; kuliko mtu baki, akikuzulumu ndio humuoni tena.
  Pole mkuu, umeumia sana Ila pesa isifanye tupoteze utu wetu.
  Mungu akupe ujasiri katika kipindi hiki. Emen.
   
 4. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nashukuru kwa ushauri mzuri ndugu zangu..lakini kwa nini alinijubu vibaya?na wakati pesa ni zangu!AU mie nilifanya kosa kumwamini?:disapointed:
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  umefanya kosa ndg yng! Pesa haina rafiki, pesa ni shetani! Kwnye pesa, wa2 huuana! Huyo m2 tabia yke co nzr, na alkuacha kwnz umwamin then ndo apate kukudhulum vzr! Pole sn! Amekujb vbaya cz hana nia ya kukulpa na amedhamiria kukdhulum! Hatak uendlee kmsumbua cz haitaj tn muendlee kfanya biashara! Samehe 7 mara 70. Mungu ana makusud yke kwny kila jambo, mwombe Mungu akupe ujacr na nguvu ili uyashnde hayo majarb. Yatapta ndg yng kikubwa hajakuibia roho yako! Pole again!
   
Loading...