Msaada wa mawazo ya maisha: Nijenge chumba kimoja ama ninunue tu container nilifanye kuwa nyumba ya kuishi?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
images.jpeg

NAOMBA USHAURI WA HEKIMA NA BUSARA ESPECIALLY KWA WENYE UZOEFU WA KUFANYA CONTAINER KAMA NYUMBA YA KUISHI.

Habari za wakati huu wadau wa mtandao jamiiforums kaka na dada zangu.

Jamani ndugu yenu hapa kuna hela ndogo nimepata baada ya kuuza ng'ombe, mbuzi, kondoo na kuku walioachwa na marehemu mjomba yangu mzee Alexander Ole Molel huku Simanjiro kwa maana hakubahatika kupata mtoto hata mmoja.

Nimepiga kama 3,500,000/= hivi. Sasa kwa kuwa nina plot yangu ndogo ipo Arusha mjini na nyingine kule dar, nikipiga hesabu kwa pesa hii siwezi kusimamisha nyumba iliyokamilika kwa ujenzi wa kule dar wala Arusha.

Nina wazo mbadala wa kununua container moja kama za pale bandarini kwa shillings 3,000,000/= kisha nikalifanya kama nyumba ya kuishi kwa muda wakati ninajipanga kijenga nyumba ya kawaida ya matofali.

Naombeni msaada kwa wale wenye uzoefu na maisha ya namna hii.

Naomba msinitukane wala kunikejeli. Mwenzenu ndio ninaanza maisha hivyo. Binadamu hatufanani vipato wala viwango vya maisha.

Thanks in advance.

Follow me;
===========
Military Intelligence Coup: Kisa cha rubani aliyeiba na kutoroka na Ndege ya Kijeshi ya Iraq
==========
K.G.B Espionage na Ujasusi kwa njia ya ngono kama silaha ya vita. Honey trap/Honeypot....Part One (1)
==========
Serikali na TRA, mnaweza kuwezesha utoaji wa risiti za VAT kwa njia ya mobile SMS. I stand to be corrected
==========
Ushauri kwa Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya, Wizara ya michezo, TFF pamoja na BMT
==========
Wahandisi wa kampuni za simu, kwanini tusikwangue vocha kisha tukaingiza kwenye mobile money accounts zetu?
==========
 
View attachment 701343

Ingia kwenye mitandao tafuta home caravans chagua dizaini kisha kanunue skrepu za madirisha ya mabasi hats vyoo vya mabasi vipo, A/C zipo cooler boxes zipo viti na vitanda pia vipo.
 
Kontena ni dogo na huwezi kulipanua leo au baadae. Jenga na uache matoleo hata ukiokota hela kesho unaweza kuongeza chumba kingine na hata kuwa nyumba kubwa.
Kwanza saivi hali mbaya watu wanaiba sana unaweza siku ukaamka ukakuta wameiba kontena na wewe ukiwa ndani
 
Ukimpata fundi mwaminifu Ml.3.5 Dar es salaam unapata chumba na sebule safi kabisa, ninakijua ninachokisema. Nitakuunganisha na fundi mzuri free, sihitaji hata Sh.kumi kwako wala kwake just kuungana mkono tu kwenye shughuli chanya.
Mkuu nimekuquote kwa sababu hiki ulichosema nitakihitaji hivi karibuni.
 
Back
Top Bottom