BABA SANIAH
JF-Expert Member
- Oct 20, 2013
- 4,494
- 5,690
Habari zenu wote kwa pamoja,
Nitaandika kwa kifupi ili nisiwachoshe wasomaji katika jukwaa hili.
Nimezaa na dada fulani hivi mtoto mmoja, tangia pregnancy mpaka mwisho nilimhudumia kwa hali na mali kutokana na kile nilichojaaliwa kwenye uwezo wangu na hadi mtoto anafika mwaka mmoja.
Baada ya hapo alinitaarifu mtoto anampeleka kwa dada yake nami nikasema no problem, so long nilikutanishwa nae na matumizi yote ya mtoto sasa nikawa napeleka kwa dada mtu, kwakuwa yeye ndio yuko na mtoto.
Lakini nikaanza kupata mashaka, kwanini dada mtu amlee mtoto ambae si wake, nikaanza kutumia intelijensia yangu niliyopata. Baada ya kukamilisha upelelezi nikagundua kumbe mtoto wangu kauzwa bila ya mimi kufahamishwa. Kwamba kulikua na makubaliano ya siri sirini.
Makubaliano yalikua dada mtu kwa kuwa hana mtoto na jamaa anaeishi nae anataka mtoto basi wakauziana wa kwangu ili aendelee kulinda ndoa yake kwa jamaa, nikatumia mbinu nikawatisha wakaenda kituo cha polisi kushitaki, tukaitwa wote, mimi baba wa mtoto halali mama wa mtoto halali
mama wa mtoto aliepewa baba wa mtoto aliebambikiziwa.
Kila mtu akaeleza anavyojua mama wa mtoto halali akasema mtoto wangu alikufa yule wa dada yake mama wa mtoto bandia, mtoto amezaa na mumewe alivodai baba wa mtoto bandia, ananishangaa mimi kudai mtoto wakati si wangu maamuzi yaliyofikiwa, tukapime DNA. DNA ikionyesha mtoto ni wangu na nina uhakika asilimia zote.
Je kuna haja ya kumwachia nafasi mtoto akamsalimu mama yake wakati alimuuza nikipata ushindi hapa mali zangu yaani mtoto watanipa baada ya muafaka wa suala hili kuna haja ya kuendelea kuwa na mahusiano ya kifamilia na kindugu na hiyo familia.
Ahsanteni, nawasilisha.