G'taxi
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 6,614
- 8,615
Kiufupi dogo alizaa na mwanamke mmoja ambae hakuja kuishi nae na mtoto ana miaka mitatu sasa.
Tatizo liko kwa mwanamke kukosa hekima, dogo anamtunza mtoto kama kawaida anatoa pesa za chakula na matibabu na hata bila uhitaji.
Dogo hutuma pesa bila hata kuulizwa, cha ajabu ni huyo mwanamke, takribani miaka mitatu sasa huyo mwanamke anamtukana dogo matusi ya nguoni na kashifa chungu mzima, tukimuuliza anataka nini hasemi zaidi ya matusi, atatukanwa dogo na mpaka familia nzima kwa meseji kwenye simu, ushahidi wa meseji anao na ushahidi wa kumtunza mtoto kwa pesa anao, maana alipokuja kugundua tabia mbaya za huyo mwanamke kua na mdomo mchafu alianza kuwa anatoa mahitaji kwa njia ya m pesa tu na si mkononi na meseji zote pia anazo, anacholalamikia mwanamke hasemi yeye ni kutukana tu.
Kwa hekima na mawazo ya busara, nini tufanye?