Msaada wa matibabu ya mtoto Ebeneza Pembe, anasumbuliwa na kansa ya ngozi

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Wakuu kuna hii taarifa nimeikuta Michuzi nikaona niiweke hapa ikiwa kuna mtu ataguswa na tatizo la huyu mtoto aweze kumsaidia.

Mama ROIDA MUHAMA mkazi wa Mkimbizi mjini Iringa, anamuuguza mwanaye aitwaye EBENEZA PEMBE anayesumbuliwa na saratani ya ngozi kwa miaka sita sasa.

Anaomba msaada wa hali na mali ili aendelee kumtibia mwanaye, Anahitaji kiasi cha fedha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuendelea na matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Kwa yeyote atakayeguswa tuma mchango wako kwa njia ya M-pesa 0767834377 au Tigo pesa 0717353529 kwa SILVANUS KIGOMBA au 0762 174 573 ROIDA MUHAMA (Mama wa Ebeneza).
IMG-20160321-WA0046.jpg

Mtoto EBENEZA PEMBE anayesumbuliwa na Kansa ya Ngozi kwa zaidi ya Miaka 6 anahitaji Msaada wa fedha zitakazo muwezesha kwenda kupatiwa Matibabu katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
IMG-20160322-WA0038.jpg

Mtoto EBENEZA PEMBE aliyevaa shati la Bluu akiwa amebebwa na Mama yake Mzazi Bi ROIDA MUHAMA mkazi wa eneo la MKIMBIZI manispaa ya Iringa, kushoto ni mtoto mwingine wa Bi ROIDA wakiwa katika Picha ya Pamoja.
...................
Nimeguswa na maumivu na mateso anayoyapata mtoto Ebeneza kwa zaidi ya miaka 6 nimejitolea kusaidia kusambaza taarifa za Ugonjwa wake ili kukusanya michango kwaajili ya matibabu yake.

Naomba ushirikiano wenu rafiki zangu na Mungu awabariki sana.

Chanzo:Michuzi

 
Aya watanzania tumsadie mtoto wetu ili aweze kupata matibu, tuma chochote ulichonacho kitafika na utakuwa umemuondolea mateso mtoto huyu ambae ni nguvu kazi ya mama yetu Tanzania,
Please mchongo wowote unapokelewa kuazi 100, 500, 1000, 5000 au 10000. Zote zinapokelewa hata maombi yako yana mchango mkubwa kumpatia uzima mtoto wetu huyu
 
Back
Top Bottom