Msaada wa mapishi bora ya TAMBI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa mapishi bora ya TAMBI

Discussion in 'JF Chef' started by Paul S.S, Sep 6, 2012.

 1. P

  Paul S.S Verified User

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wadau wa jukwaa hili naombeni utaalamu wenu kuntu, hatua kwa hatua ya namna bora ya kupika tambi zikawa hazikatiki katiki wala kushikamana kama wali
  zikawa nzuri na wakat wa kula unaweza kuifyonza tambi moja mwanzo mwisho kama tuonavyo kwenye matangazo
  Natanguliza shukrani
   
 2. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  1.Hatua ya kwanza unakata tambi kwa ukubwa unaotaka kama unataka kushika moja moja unakata mara tatu.
  2. unachemsha maji jikoni yakichemka unatia chumvi halafu unatia tambi zako.
  3. unazichemsha kwa muda wa dakika kumi na tano ziive zisirojeke sana, unamwaga yale maji unaacha tambi zenyewe, hakikisha umemwaga maji yote.
  4.Baada ya kumwaga maji unatia mafuta kiasi unachopenda unachanganya tambi na mafuta unaacha ichemke kwa dakika kumi hakikisha wakati zinaiva na mafuta moto wako uwe mdogo , Wengine hupendelea kuweka blueband badala ya mafuta inategemea wewe unapenda nini.
  5. Baada ya hapo zitakuwa tayai kwa kuliwa.
   
 3. P

  Paul S.S Verified User

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Thanx Joyceline kwa maelezo, vipi kama nataka kuweka na vikorombwezo vingine kama karoti,majani ya vitunguu,hoho nyanya kama zinawekwa nk nk

  hiyo ilionipa darasa itakuwa plain sana
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,609
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  MMkuu raha ya hivyo vitu vingine utumie Noodles na sio tambi maana ndio utaenjoy zaidi
   
 5. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,647
  Likes Received: 8,207
  Trophy Points: 280
  The SIMPLEST n BEST way out of that dilema is to GET MARRIED...
  Au jaribu ile ya kuzikaanga (for lack of a better word) ile kabla hujaweka maji. Kama vile unapika zile za sukari.
  Yani weka mafuta kidogo kwenye sufuria..then tia ndani tambi zako kama unavokaangaga kitunguu (mimi hupendelea kuzikata mara mbili)...zitabadilika rangi na kuwa brown..then tia maji na chumvi kiasi. Uzur wa hii koz zipo sufurian tayar unaeza kukadiria maji kiurahisi zadi.
  But as i said before...ukioa utashangaa tambi zako zenyeewe zinanyonyka mpaka mwisho. Au kwenye adverts uliona mwanaume akipika??! Lol ;-)
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280

  Kumbe mpishi mzuri eeh! Hizi za hapo kwenye rangi ndizo ambazo mimi huzipenda.
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Kuna tambi flani nyembamba kama mchele, tamu sana. Nazo unakaanga kidogo then unataia maji kidogo. Joyceline, mimi huchemsha na mafuta pia kwenye maji (kama sijazikaanga). Baada ya kuchuja maji, naweka cheese kiduuchu

  Recipe ya kivivu hii hapa.
  kaanga kitunguu na nyama iliyochemshwa kiwe brown,Weka spices (binzari kidogo)
  tia nyanya zipikwe hadi ziive kabisa.
  tia tambi, zikoroge kidogo then tia maji ya moto kiasi cha kufunika tambi
  zisipoiva ongeza maji kidogo. Angalia maji yasizidi. Baada ya kuiva, weka karoti zilizokatwakatwa, majani ya vitunguu na hoho. Changanya kisha serve (wakati karoti na hoho bado crunchy)

  Unapata msosi full suti, nusu saa inatosha kwa upishi huu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Aseeeee
  Duh!!
  Ngoja jioni nitajitengenezea hii
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Mentor kashauri uoe. Acha ubahili brazakaka
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hata sijakupata
   
 11. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,647
  Likes Received: 8,207
  Trophy Points: 280
  Hahahah King'asti kama unanionaga vile. Ila mi hutumia minced meat (nyama ya kusaga) thnx to Madame B.
  Btw izo nyembamba ndo zinaitwaje nkatafute au ziko kwenye package ya aina gani??!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,647
  Likes Received: 8,207
  Trophy Points: 280
  1. Waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba hujuana kwa vilemba vyao.
  2. Birds of a feather flock together.
  3. It takes one (mpishi) to know (n understand) one (another mpishi).

  Itakuchukua karne....
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Bwana weeh, mie nazitumia ila nasahau jina kila siku! Nikiagiza nasema zile tambi nyembambaaaaaaaaaa, naeleweka hehehe. Inakuwa kama a bag of cookies, nikumbushe nikichungulia jikoni nikupe jina kamili. Pakiti imeandikwa kiarabu na ina green background na white letters sehemu ya kati.
  Nyama ya kusaga haifai wavivu, manake mie hupenda kuikausha kwanza ikiwa na spices, kisha kuunga pembeni ndo nichanganyie na tambi zilizochemshwa.
   
 14. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,647
  Likes Received: 8,207
  Trophy Points: 280
  Aaaaaaaaaaaaaaah kama nshaionaga supermarket...ntaenda kuzunguka uko nione kama ni iyo. Ukiniwahi unipe jina.
  Af unakumbuka uliniahidi utakujaga kunipikia one day...am ctil waiting.
   
 15. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Me? Cooking for you?
  Mbona utadodea hapo ukisubiri? Mie nampikia huzbend wangu tu manake siwezi kupika nisiweke japo limbwata kiduchu!
   
 16. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #16
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Okay, Benvenuto! (karibu, kiitaliano). Nitakufundisha mimi, twisheni pia ipo.

  Ni hivi; Tambi ama Spaghetti kwa kiingereza, ni aina mojawapo ya vyakula vitokanavyo na ngano kundi la Pasta. Hivyo pasta zipo nyingi ikiwemo tambi zenyewe/Spaghetti, zingine ni fusil, penne, ravioli, tagliatelle, macharonne na nyingine nyingi tofauti tofauti zaidi ya mia moja.

  Zipo pia pasta maalumu kwa ajili ya supu tu, kwa kawaida huwa ni ndogondogo wakati mwingine karibia na mchele. Pasta zote zikiwemo tambi au spaghetti zinaweza kuwa ni kavu (zile zilizopo dukani) ambazo mara nyingi hutengenezwa viwandani na pia zinaweza kuwa fresh (yaani unatengeneza mwenyewe na kuzipika papo hapo), karibu aina zote za pasta zinaweza kuandaliwa na kupikwa zikiwa fresh. Hata tambi zipo fresh, Mi kwa ujumla hupendelea pasta fresh kwa sababu zinaradha ya aina yake nzuri tofauti na zile za dukani. Kama hujawahi hili unaweza usinielewe.

  Tambi au pasta karibu zote zinaweza kuwa za rangi pia, unaweza kutengeneza za blue, za kijani, nyekundu, za brown na kadharika na kadharika. Mhimu ni utumie natural coloring agents (usitumie rangi za viwandani sababu zina kemikali, ni tetesi lakini). Kama unataka za kijani kwa mfano, wakati unaandaa unga wa ngano tayari kwa kukandwa kuandaliwa kuwa pasta, ongeza kiasi kidogo cha mchicha uliochemshwa kidogo na kusagwa unga baada ya kuchujwa maji. Mwisho utapata pasta au tambi za rangi ya kijani.

  Nimesema twisheni ipo, sasa nisije sababisha usirequest twisheni bure...........

  Namna ya Kuchemsha tambi:
  Bado kuna mkanganyiko wa juu ni wapi tambi au chakula jamii ya pasta kiligunduliwa kwa mara ya kwanza, baadhi ya wanataaluma wanadai ni China ndiko pasta ziligunduliwa na wengine wanadai ni Italia ndiko ziligunduliwa. Bali inajulikana kote duniani kuwa ukienda nchi yeyote ukakuta mgahwa au hotel ya kiitalia (Italian hotel/restaurants), usipokuta tambi au pasta, basi hapo siyo penyewe!.

  Kwa mjibu wa kitabu cha Paolo Urbani alichoshirikiana na Silvano Rodato kiitwacho Laboratorio di Cucina ukurasa wa 190:


  • Tambi au pasta hupikwa katika maji mengi ya kutosha yaliyochemka kufikia nyuzi joto 100, yaani yamechemka.
  • Uwiano ni maji lita 10 kwa kila kilo 1 ya pasta/tambi.
  • Kamwe usijejaribu kuongeza maji ya baribi ndani ya maji hayo ya moto yanayoendelea kuchemka ya tambi au kuzinyunyiza tambi/pasta maji ya baridi baada ya kuzichuja toka maji moto kwa madai kuzisimamisha zisiendele kuiva.
  • Pasta/tambi ni chakula kinachopikwa na kuandaliwa katika hali ya haraka na kutokusimama kushangaa chochote, unapotumbukiza tambi unatakiwa ujihakikishie kuwa huna kazi nyingine itakayokufanya upunguze moto au umsubiri fulani, inatakiwa unaona wote wamekaa mezani ndo unatumbukiza tambi kwenye maji. Mara nyingi waitaliano wengi wanapokuwa njiani kurudi majumbani mwao wanapokaribia na kukunja kona ya mwisho kuingia mtaani kwao huwapigia simu waume au wake zao watumbukize tambi/pasta kwenye maji (buta la pasta!).
  • Mhimu kuliko yote ni kuwa hadi mwishoni mwa kuchemka na hadi kuungwa kwa pasta zako, ni lazima uhakikishe zinabaki bado ni ngumungumu kidogo yaani zinasikika katika meno, kama ni wali unasema bado una kiini (al dente!).

  Okay hatua za kuchemsha tambi;
  Mahitaji:

  • Tambi kilo 1
  • Maji yaliyochemka lita 10
  • Chumvi ya jikoni gramu 100
  • Mafuta ya kupika (vizuri kama unapata ya zeituni) robo kikombe
  MHIMU SANA: Tafadhari tambi haziongezwi sukari kwa sababu yeyote ile.

  Namna ya kupika:

  • Tumbukiza tambi zako kwenye maji yaliyochemka vya kutosha yenye chumvi na mafuta ya kupikia. MHIMU, USIZIVUNJE HATA MARA 1 TAMBI IWE KABLA AU UNAPOCHEMSHA!!!, tambi zichemshwe kwa urefu wake wa asili, hii ndiyo sababu uma (fork) ndio hutumika kulia tambi na siyo kijiko wala mkono!!!, unachomeka uma, unazungusha kupata kifundo cha tambi utakazoweza kuzimeza, unatumbukiza mdomoni.
  • Unatakiwa kuzikoroga mara kwa mara kwa kutumia uma mkubwa mrefu, iweleke ninaposema mara kwa mara haina mana basi mtu ashike kiuno na asimame hapo akikoroga tambi kama anakoroga uji wa ugali, unakoroga dakika 2 au 3 unapumzika kisha unarudia tena.
  • Unatakiwa kuzionja moja moja kila mara ili kuvizia zinapoanza kukaribia kuiva uzitoe haraka, usipofanya hivyo lazima utapoteza point, pale unapotaka kujuwa kama tayari zimeiva kumbe ziliiva kitambo kwa sababu we ulikuwa huonjihuonji kabla ili kuzivizia.
  • Kisha kukaribia kuiva tambi huchujwa toka katika maji na kuziunganisha na sauce (sosi) ambayo umeamua kuitumia kuungia tambi zako siku hiyo. Kwa kawaida sosi huandaliwa kabla ya kuchemsha pasta, au huku unaandaa sosi huku maji ya tambi yanachemka. Zipo Sosi (pasta sauce) zaidi ya 100, kila sosi ina jina lake na mahitaji yake maalumu, kadri unavyobadilisha aina ya sosi ndivyo na jina la tambi au pasta uliyopika linavyobadilika. Kwa uchache kuna sosi ya nyanya (tomato sauce), sosi nyeupe (white sauce, hii maziwa hutumia zaidi), sosi ya nyama ya kusaga (bolognaise sauce/minced meat sauce), Fish ragu', amatriciana, alla romana. alio-olio-peperoncino, na kadharika na kadharika.
  • Mifuko mingi ya pasta/tambi huandikwa kabisa dakika za kuchemshwa ubavuni mwake tangu kiwandani.

  Nikuchagulie pishi moja la tambi litakalokuduwaza?
   
 17. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,647
  Likes Received: 8,207
  Trophy Points: 280
  Kha..umesoma mahali ukatafsiri ama wajua kweli??! U av amazed me kwakweli kwa upembuzi wako yakinifu..yan mtu haulizi swali.
  We King'asti unaniletea pozi eti nitangoja milele wala ctaki unachek mshkaji anavojua pishi ilo?? Dah...
  Babu Asprin fanya hima uwalete wake zako cacico, BADILI TABIA, Yummy, et al 'TUISHIENI'.
  Mai waifu Catherine uko wapi uje huku...
  Binti yetu mpendwa Eversmilin Gal njoo na ww utapoolewa usijeachika...
  NB: kwann sisi tumezoea kuvunja spaghetti??!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,865
  Likes Received: 6,216
  Trophy Points: 280
  haya naona King'asti kamaliza.....

  zile ndogo ndigo nyembamba? sijui vermiceli kama sikosei? i hate them loh........... ila nitajaribu kupika kutokana na recipe yako.......
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. P

  Paul S.S Verified User

  #19
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Dah fadhili paulo unatisha, nashukuru kwa udadafuzi wako wenye weledi wa kutosha
  kwenye red nasubiri kwa hamu...........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. B

  Bibi yaga Member

  #20
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 5, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tambi
  Mahitaji:
  1. Kitunguu kikubwa kimoja
  2. Nyanya mbili kubwa
  3. Karoti kubwa moja.
  4. Pilipili Hoho Nusu
  5. Tambi gram 250
  6. Mafuta ya kupikia
  7. Chumvi
  8. Nyama ya kusaga 1/4 Kg
  9. Tangawizi
  10. Limao
  11. Kitunguu swaumu

  Matayarisho
  1. Weka sufuria jikoni, weka mafuta na ukaange vitunguu maji vikifatiwa na vitunguu swaumu
  2. Baada ya hapo, chukua nyama yako ya kusaga na uitie kwenye sufuria yenye vitunguu vyote.
  3. Kisha tia tangawizi kwenye nyama huku unaendelea kuikaanga, baadae tia nyanya, hoho na karoti
  4. Ipua na uweke pembeni
  5. Chukua sufuria nyingine, weka maji na uibandike jikoni mpaka maji yachemke
  6. Maji yakisha chemka, weka chumvi kiasi na uzitie tambi zako
  7. Ukiona zimelainika kiasi, yachuje maji yoote na tambi zibaki kavu.
  8. Chukua ule mchanganyiko wako wa viungo na tia tambi zako na uziache jikoni kwa dakika 5 hivi..
  9. Hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa...
   
Loading...