Msaada wa lift kutoka Kahama kwenda Dar es Salaam

kiazikitam

Member
May 18, 2021
58
24
Habari za wakati huu mimi ni binti mkazi wa Dar es Salaam ila kwa sasa nipo kahama, katika harakati za kujikwamua nilipata msaada wa mtu akanambia kuna kazi ya mgahawa hapa kahama hivyo nije kuanza na makubaliano yote yalifanyika ila baada ya kufika kwa nauli ya kujichanga mtu yule hapokei simu zangu tena toka juzi na sasa hapatikani tena.

Sijajua kilichomsibu mpaka sasa na mimi ni mgeni kabisaa hapa sina ninae mjua hapa na sina hata mia namna naishi anajua Mungu pekee.

Kwa sasa nataka kurudi tu Dar es Salaam tafadhali yeyote ambaye ana usafiri na yupo kahama anatarajia kuja Dar es Salaam muda wowote kuanzia sasa naomba anisaidie lifti maana kuomba hela ni ngumu naomba msaada wa lifti tu ndugu zangu.
 
Asante. Kumbe nilitakiwa kusoma post yote. Kuna mengi ya kusoma. Nilisoma title tu. Hapo atapata tu. Madereva wengi ni Me. Ke mnapitia katika majaribu sana. Sasa hapo si yupo chini ya miguu ya mwenye gari (mtoa lift) tu?

Halafu pia binadamu ni wanyama. Utamwitaje mtu toka mbali huko halafu unapotea? Wenye roho za aina hiyo nadhani ndio walikuwa ama bado wanamshabikia Magufuli. Kwao kuua, kufunga wengine kwa makosa ya kubambikizia, kufanya uhuni wa aina hii hakuwaumizi. Na wapate taarifa za binti huyu ili wafurahi - johnthebaptist, mama D, Jane Lowassa
 
Ushapata lifti? Mi ndo napita kahama apa alafu chumainakesha mpaka kwao! Hujaweka mawasiliano yoyote, ukiwa serious useme wapo majembe nimewaacha masumbwe apo, lakini si private ni maroli. Sina uhakika kama watakesha kama mm au watalala njiani tofauti na hapo, tumia njia hii.

Nenda sehemu yoyote wanakosimama Trafki waeleze shida yako, ukiwa ushajiandaa na Safari, hitokosa gari. Ningekusaidia ila chuma inakibari siwezi kukusubiria, fanya hivyo nilivyokuelekeza utapata usafiri ki rahisi zaidi endapo utaomba hao wana usalama wakusaidie.
 
Asante. Kumbe nilitakiwa kusoma post yote. Kuna mengi ya kusoma. Nilisoma title tu. Hapo atapata tu. Madereva wengi ni Me. Ke mnapitia katika majaribu sana. Sasa hapo si yupo chini ya miguu ya mwenye gari (mtoa lift) tu?

Halafu pia binadamu ni wanyama. Utamwitaje mtu toka mbali huko halafu unapotea? Wenye roho za aina hiyo nadhani ndio walikuwa ama bado wanamshabikia Magufuli. Kwao kuua, kufunga wengine kwa makosa ya kubambikizia, kufanya uhuni wa aina hii hakuwaumizi. Na wapate taarifa za binti huyu ili wafurahi - johnthebaptist, mama D, Jane Lowassa
Mkuu wewe binadamu mwema si umtumie tu nauli ya bus arudi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom