Msaada wa kuzuia harufu inayoingia ndani kutoka kwenye tanki la maji machafu

davetz28

JF-Expert Member
Dec 17, 2017
543
617
Habari Wana jamvi, nimekuja kwenu kupata suluhisho la tatizo linalosumbua nyumbani kwangu.

Kuna lile tanki la maji taka linalokusunya uchafu kutoka chooni na bafuni ambalo sasa limekuwa kero.

Siku za nyuma niliweka bomba fupi tu na bado bomba halikuwa linatoa harufu lakini kwa siku za usoni hali ilibadilika. Niliamua kuweka bomba refu zaidi lakini hali bado kwani harufu bado inaingia ndani hasa madirisha yakiwa wazi.

Nini nifanye ili kuepukana na hali hii? Je, kuna jambo naweza kufanya ili kupunguza au kuondoa kabisa harufu hii ambayo imeanza kuwa kero kwa majirani pia?
 
1. Wakati wa ujenzi wa karo la maji taka, ulikuepo na ukashuduia wewe mwenyewe kama ziliachwa nafasi kwaajili ya upumuaji wa mzigo unpokua shimoni?
2. Are you sure kwamba harufu inatokea kwenye exhaust pipe ya kwenye karo?
3. Umewahi kufanya utafiti wewe personally na ukagundua kwamba harufu inatokea nje na sio ndani?
4. Je, umejiridhisha na jografia ya chemba zinazo unganisha mambomba ya maji taka toka kwenye nyumba kwenda kwenye karo?
5. Je, unauhakika kama bomba la kupumulia halijaziba kwa bahati mbaya ama kwamakusudi?

Ebu kwanza jibu hayo maswali ili mafundi wa vyoo tukusaidie kwa ushauri.
 
Nagas za upumuaji sizijui, lakini wakati wanaunganisha bomba za maji taka nilikuwepo. Exhaust pipe haijaziba kwani tulitoa na kuweka nyingine.Toka tuweke imeshapita miaka mitano ndio tatizo hilo limejitokeza
 
Inaelekea ullijenga vibaya hilo tanki.
Kabla ya kushauri, hilo tenki likoje?
Ni tenki moja tu na maji yote yanaishia huko au ni lie standard septic tank lenye chumba kimoja kikubwa lakini vizuizi visivyofika chini vya kuongoza maji machafu na soak pit?
 
Inaelekea ullijenga vibaya hilo tanki.
Kabla ya kushauri , hilo tenki likoje?
Ni tenki moja tu na maji yote yanaishia huko au ni lie standard septic tank lenye chumba kimoja kikubwa lakini vizuizi visivyofika chini vya kuongoza maji machafu na soak pit?
Tanki moja mkuu
 
Isije kuwa inatoka kwa majirani.
Hapana,nimefuatilia na kujiridhisha kuwa tatizo halipo kwa jirani.Wengine walinishauri niweke chumvi, wengine majivu lakini nikaona nipate mawazo zaidi huku
 
Mtu anaomba ushauri watu mnakuja na mabandiko yenu.

Ok ila sio mbaya, nakushauri tafuta mafuta ya taa kama lita moja au mbili mwagia humo kila baada ya siku nane/wiki.

Japo utaingia sana gharama.

Then rudisha feedback
 
Asnte kwa ushauri,labda kama lita ngapi ili niifanye kazi kesho
 
Asnte kwa ushauri,labda kama lita ngapi ili niifanye kazi kesho
Sijajua vipimo zaidi inakuwaje ila hebu jaribu kuanza na mbili then uwe unasikilizia baada ya siku ngapi tena kitaanza

alafu fanya mpango yasambae..sasa hapa sijui utatumia njia ipi,ila hata ukichanganya na maji itakuwa sawa tuu ili harufu ya hayo mafuta yasambae
 
Kama yanarudi kwa njia bomba basi itakua haijawekwa zile 'water trap', ambazo zinafanya kazi ya kuziba harufu na wadudu wasirudi ndani kwa kuwa zinahifadhi maji. Ama pengine zimekwa zikainama, hivyo hazitunzi maji (water seal).
Kama ni kwingine itakua bomba lako la kutolea harufu ni fupi ama limewekwa vibaya, halipaswi kuwa ndani ya maji ilia lifyonze hewa chafu na kuitoa juu.
 
Back
Top Bottom