kwetugt
JF-Expert Member
- May 24, 2015
- 273
- 233
Kama maada inavyojieleza hapo juu mie ni mhanga wa hiyo kitu cheti changu cha kumaliza kidato cha nne (academic certificate) sikubahatika kukiona na hii ni kwasababu pindi vyeti vinatoka nilikua shule hivyo baada ya kuhitimu kidato cha sita nikafatilia cheti changu shuleni bahati mbaya mkuu washule nikakuta mwingine tofauti na yule niliyemuacha cha ajabu huyu mwalimu baada ya kumweleza shida yangu akaniambia cheti changu hakipo ulitokea wizi na mwizi ni mwalimu wangu hivyo mie kama mkuu wa shule nilimpeleka polisi na polisi wanaendelea na uchunguzi lakini mkanganyiko unakuja baada ya kumbana mkuu akadai mtuhumiwa baada kupata mdhamana alitorokea kusikojulikana japo alikili kuwa nacho hivyo nilizidi kumuuliza kama mtuhumiwa alikili kuwa nacheti kulikoni wewe mkuu shule usiombe kwenda kuchukua hicho cheti, mwalimu mkuu huyu alidai hiyo haikuwa kazi yake maana tayari mtuhumiwa alikua kwenye vyombo vya usalama , kumbe mie sikutambua kinachoendelea baadae nilikuja kujua huyu mwalimu mwizi walishilikiana na askali kufanya wizi maana cheti lilipotea siku wanafanya mtihani askali akiwa kama mlinzi wa mitihani ofisini kwa mkuu wa shule, hivyo ninaomba msaada wa kitaraamu kufanikisha jambo hili maana cheti namba ninazo alinipatia mkuu wa shule.