Msaada wa kupata ufadhili wa gharama za maisha nchini Urusi

Pesawebz

Senior Member
May 22, 2021
117
209
Habari za jioni wana jamii forums?

Niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi wangu! Mimi nikijana niliebahatika kupata scholarship ya kwenda kusoma urusi, ambapo mategemeo yangu ni kuondoka mwakani ,(kwa mujibu wa ubalozi wa urusi nchini Tanzania )

Hii scholarship ina cover tuition fee tu, Lakini kuhusu gharama zifuatazo najitegemea

1. Gharama za kupanga chumba cha kulala
2. Gharama za afya yangu
3. Gharama za kula na kuvaaa

Hivyo naomba msaada wa kupata mtu wa kunisaidia , au taasisi yoyote ambayo naweza kuwaendea wakanisaidia ! Maisha ya mtaani ni magumu sana, nimejitahid kulima na kuomba kazi kila sehemu Lakini maisha magumu sana sijafanikiwa kabisa tangu nimalize diploma yangu 2015

Mungu kanisaidia nimepata scholarship ambayo itanilipia ada tu, tafadhali naombeni msaada

Natanguliza shukrani
 
Mkuu samahani lakini suala la kozi Lina athari yoyote na gharama za kuishi?
Hapana ila wakati mwengine huwa kuna chansi za ufadhili kwa watu wa kozi fulani pengine akimaliza afanye kazi katika mashirika husika.

Lakini pia anamweza kumshauri kwa kozi hiyo haina haja ya kwenda kutaabika huko akampa ushauri mwengine mzuri.

Ni mtizamo wangu tu
 
Back
Top Bottom