Msaada wa kupata paka

Jalala

Member
Apr 15, 2010
47
18
Natafuta Paka wa kufuga ninasumbuliwa na panya sana na naogopa kuwawekea sumu maana niliweka sumu ikamuua panya mbwa akala nae akafa naomba msaada kwa yeyote mwenye paka
 
Hebu acha masihara mkuu...unakaa nchi gani...nenda kwa majirani hapo hutafika nyumba ya tatu na paka utapata....au wataka link undownload.
 
Ninao wadogowadogo wana mwezi sasa Wahi haraka. Ni free. send me an e mail
 
Hiyo umbwa ni kali ila muda unawafungulia paka inakuwa ndani amani tu

kama ni hivyo sawa.....lakini paka nayo huwa ina kiherehere sana....uingalie kwa ukaribu....kama ukiipata
 
Yaani Preta huwezi amini nimeshapata paka jioni naenda kuchukua, asante Maarifa , jamii forum salute.
 
Yaani Preta huwezi amini nimeshapata paka jioni naenda kuchukua, asante Maarifa , jamii forum salute.

hongera sana kwa kupata paka......naomba uilee kwa upendo na malezi mema.......kama hutajali utuwekee na picha yake hapa....
 
Tena sio mmoja wako wawili very cute!! Jalala wapige picha halafu uwawekee waone. God bless
 
Natafuta Paka wa kufuga ninasumbuliwa na panya sana na naogopa kuwawekea sumu maana niliweka sumu ikamuua panya mbwa akala nae akafa naomba msaada kwa yeyote mwenye paka

Mwananyamala kwa BIBI NYAU (kuna kituo cha daladala kwa jina hilo)...
 
ila paka wa mjini hawali panya... tena wakijua hapo kuna panya ndio kabisaaaaa... watakuwa wanashinda juu ya makochi na wali sio juu ya dari au sakafuni.... kwanza chakula chenyewe ukiweka chini hawali... wanapenda starehe sana... labda upate paka wa uswahilini.. tatizo hao nao full kujisaidia ovyo au kuiba vyakula... wanakula mpaka kuku..... yaani hawa CCM hawa wametuharibia mpaka wanyama wetu wa kufugwa,... enzi za nyerere mamo hayakuwa hivi.... rejea kitabu cha akina juma na roza hadithi zake....

MAGAMBA mshindwe kabisa
 
Paka wamekua Maarifa waone wlivyokuwa
 

Attachments

  • DSC00642.JPG
    DSC00642.JPG
    807.4 KB · Views: 69
  • DSC00870.JPG
    DSC00870.JPG
    616.8 KB · Views: 64
Maarifa na Mimi Paka MMoja Please, Nilikuwa na Wawili nikagawa mmoja, Na huyo mmoja alikuwa na Watoto 4, bahati mbaya amekufa na vitoto vilikuwa na wiki moja vimekufa vyoote.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom