Kilimo cha kisasa cha maembe

Chief

Platinum Member
Jun 5, 2006
3,291
2,619
Msaada tafadhali wajemeni. Nina shamba mahala ambapo nataka kupanda miembe. Ushauri? Wapi nitapata miche ya miembe?
Nipo Dar.

======

Zao la embe hustawi vizuri katika maeneo ya tambarare na miinuko kati ya futi 0-600 usawa wa bahari.

Kiwango cha wastani cha mvua inayohitajika kwa kilimo cha embe ni mililita 650 hadi 1850 kwa mwaka.

Miembe hustawi katika udongo wenye uchachu (ph) kati ya 5.5 na 7.2. udongo wenye chachu zaidi huwa na upungufu wa madini mbalimbali ikiwemo zinki, chuma, fosforas na kalsham.

Kuandaa mashimo
Kuchimba mashimo mapana kutafanya udongo uwe laini ili kusaidia mizizi kuzaliwa kwa wingi, upana wa shimo uwe sentimita 60x60 upana kwa urefu, kwa maeneo yenye udongo mgumu na miamba ya mawe kipimo kiwe sentimita 100x100 upana na urefu.

Uchimbaji wa mashimo uwe wa kutengeneza udongo katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni udongo wa juu wa kina cha sentimita 30 na sehemu ya pili ni udongo sentimita zilizobaki za kina cha shimo.

Mbolea za kupandia
Tumia mbolea samadi au mboji iliyoiva vizuri debe moja hadi mbili kwa shimo, changaya mbole na udongo wa kwanza kutoka shimoni, iwapo itatumika mbolea ya viwandani kama DAP, TSP, NPK au Minjingu Phosphate changanya mbolea hiyo na udongo wa juu wenye mboji (top soil).

Upandaji
Panda miche ya miembe katika misimi ya mvua za mwaka, au wakati wowote iwapo inatumika njia ya umwagiliaji kwa vipindi visivyo na mvua. Weka maji ya kutosha wakati wa upandaji ili kuimarisha mshikamano wa udongo na unyevu.

Kipimo
Miembe hupandwa katika vipimo tofauti kutegemeana mipango ya matumizi ya ardhi husika na miundombinu ya shamba. Upandaji unaweza kuwa wa miti 160 hadi 1300 kwa hekta moja. Vipimo vya umbali kati ya mti ana mti vifuate mistari iliyonyooka.

Kipimo cha wastani kwa wakulima wadogo na wakati ni mita 8x8, mita 6x8, mita 4x8, mita 4x7 au mita 5x7. Wastani kwa hekta ni miembe 200-400 ujazo wa vipimo vingine vinaweza kufikia miti 1200 na Zaidi kwa hekta. Matumizi kwa vipimi hivyo vinahitaji ushauri wa mtaala, kabla ya kutumia.

Ukataji
Ukatiaji hufanyika katika hatua ya kwanza ya ukuaji miti ukifikia urefu wa sentimiti 60-100, ukatiaji wa kwanza utatofatiana na ukatiaji wa pili na kuendelea.

Ukatiaji wa kwanza, kata sehemu majani yanapopishana ili kupata umbo la mti unaopishana kutoka katika chanzo cha tofauti. Ukatiaji wa pili na kuendelea kata sehemu ya juu ya pingili ya tawi ili
kupata matawi mengi.

Magonjwa na wadudu
Miembe hushambuliwa na magonjwa kama Ubwiru unga (powder mildew), Chule
(Antharacnose), magonjwa mengine hutokea kwa mara chache sana. Wadudu mbalimbali wanaoshambulia mazao tofauti, hushambulia miti ya miembe kama Vidukari, Vung’ata, Kifaurongo, Mbawa kavu, nk.

Udhibiti wa magonjwa na wadudu
Fanya usafi wa palizi shambani kila inapolazimu ili kupnguza vyanzo wa wadudu na magonjwa, matumizi ya dawa yanafanyika kila dalili za ugonjwa zaitakapo jitokeza au mashambulizi ya wadudu yatakapoonekana.

Ukataji mkubwa
Miembe inapokuwa katika hatua ya uzalishaji huhitaji kukatiwa kila imaliziapo hatua ya uvunaji na kujiandaa kwa uzalishaji katika msimu ujao. Ukatiaji huu huwezesha mti kuchipua majani mapya kwa pamoja na kukomaa kwa pamoja, hatimae hutoa maua kwa pamoja kwa wakati unaokusudiwa.

Urutubishaji na mbolea
Mbolea ni muhimu katika uzalishaji wa embe, mbolea huendelea kutumika
wakati wa kukuza miche na kuzalisha matunda. Mbolea zinazotumika ni N.PK, MOP, Urea, Minjingu, Samadi, Mboji, Chokaa na virutubisho visaidizi.

Mbolea zitawekwa kulingana na mahitaji ya udongo na kwa wakati maalum, uwekaji holela wa mbolea unaweza ukaathiri uzalishaji utakaotokana na ukosefu wa maua.

Uvunaji na utunzaji
Embe zitunzwe zikiwa zimekomaa, embe lililokomaa lina umbo tofauti kulingana na aina ya embe, kiashiria kikuu ni embe kubonya kwa eneo la kikonyo, alama nyingine ni kubadilika kwa rangi ya ndani ya nyama ya embe kutoka nyeupe kuwa njano hafifu.

Embe zinazovunwa zioshewe kwa maji ya moto na kuhifadhiwa sehemu kavu na
salama, chagua embe na kuziweka katika madaraja mfano daraja la 1 na daraja 2. Hii itakusaidia kujua ipi embe ni tayari kwa kupeleka sokoni.
======
Michango ya wadau
Mkuu salam u nyingi na karibu kwenye kilimo

Wauza miche ni wengi sana Dar es Salaam na kwingineko lakini wauzaji miche bora ni wachahche sana.
Hivyo ni vema ukafahamu mahali pa kupata miche bora( ya kiisasa ama ya kienyeji iliyoboreshawa)

Kwanza kabisa Tambua mbegu bora: Kuna aina kama 17 ya mbegu bora za embe kwa ajili ya matumizi na masoko
tofauti. Hivyo tambua kwanza soko lako linataka nini kisha chagua mbegu iendanayo na soko/matumizi yako.

Kuna mbegu kama sita ivi kwanza BOLIBO (ya kienyeji lakini iliyoboreshwa), Kuna alfonso, Keit, Kent, Apple ambazo
ni tamu hazina nyuzi nyuzi nyingi, zina zaa sana kati ya tunda 400 - 3000, ukubwa wake ni 0.25kg - 1.3kg nk.

Hivyo kabla hujaenda kununua hizo embe ni vyema ukatambua sifa ya kila mojawapo (hata ukigoogle utapata).

Wauzaji kama nilivyosema wapo wengi ila kuna association of Mango growers (AMAGRO) wapo mtaa wa Mkurumah karibu petrol station wale wanawajua wadau wenye vitalu vyenye mbegu za uhakika nchi nzima. Mimi nafahamu wachache
1. Dr. Diwani anacho kitalu Kinondoni karibu na makaburini na ni Mkulima mkubwa sana wa embe wilayani Mkuranga hivyo yeye anazo mbegu za Uhakika.

2. Kuna kitalu Rufiji - Kibiti kinamilikiwa na kikundi cha wakulima (Rufiji Environmental Group) ambao walipata tuzo mwaka jana Nanenane ukifika kibiti karibu na kituo cha polis utaona bango lao

3. Chambezi Research Sub station kipo bagamoyo 5km kabla hujafika bagamoyo kuna kibao chao on the left hand side uningia ndani about 3km wana aina karibu zote 17 za embe za kisasa

4. SUA wanazo hizo mbegu pia unaweza ukazipata ingawa zitakua ghali kidogo

5. Mkuranga Research substation nao wana mbegu bora za miche ya miembe wapo few km (3-5) kutoka njia ya kwenda halmashauri ya wilaya ya mkuranga.

Angalizo: Wapo wajasiriamali wengi wanauza micha ya embe wengine kweli ni nzuri na za uhakika lakini wengine wameiga tu na kuingia kwenye hiyo fani.

Mfano: ukiotesha kokwa la embe yeyote linalozaa sana halafu ukaweka kikonyo cha embe bora halafu ikatokea chipukizi chini ya sehemu iliyoungwa(grafting) kama lisipokatwa na kuachwa na ikitokea kikonyo kilichoungwa kimekauka mche utaendelea kuwa wa kienyeji na sio wa kisasa.

Nawakilisha
----
Soko ni ubunifu tu, kama unataka soko la uhakika ingia contract na hotel kubwa kama mimi ili uwe unasupply matunda (may be kwa mwaka mzima) vinginevyo itakuwa ni hasara kwako coz msimu wa embe ukifika bei huwa inashuka sana.

Pia tumia artificial ways ambazo zitakufanya uwe unavuna matunda kipindi ambacho si cha msimu wa embe [bei uwa ipo juu sana kipindi hiki]
 
Ukipata hii mifupi ni mitamu na ina soko sana!

MAEMBE.jpg MAEMBE TENGA.jpg
 
Nakushukuru sana Fmewa:

Nyati: Wewe ulipata miche wapi au ulipanda mbegu (kokwa) za embe?

Miembe ipo maeneo mengi. Kwa upande wangu, kwangu kulikuwa na mwembe unaozaa sana hivyo nikaomba ushauri wa mbegu mzuri toka kwa mtaalamu aliyekuwa anapajua kwangu. yeye ndo aliyenipa ujanja huo.

Hiyo kokwa nilichukua pale pale kwangu na vile vile miche yote iliyokuwa inajiotea pale chini ya ule mwembe nayo iligeuzwa miche ya kisasa.
 
Wakuu, hivi ni wapi soko kubwa la embe? Mahitaji ya soko yako vp, zinazopatikana ni kiasi gan na zinatoka wapi?

Soko ni ubunifu tu, kama unataka soko la uhakika ingia contract na hotel kubwa kama mimi ili uwe unasupply matunda (may be kwa mwaka mzima) vinginevyo itakuwa ni hasara kwako coz msimu wa embe ukifika bei huwa inashuka sana.

Pia tumia artificial ways ambazo zitakufanya uwe unavuna matunda kipindi ambacho si cha msimu wa embe [bei uwa ipo juu sana kipindi hiki]
 
Wakuu

Nimepita Kibiri kwenye kile kikundi cha wakulima wa kitalu cha embe. I tell you wako vizuri saaaaaaana kuliko hata nilivyo tarajia.

Wameanzisha kampeni yao ya '' Lima miti kumi ya embe upate Shillingi millioni moja. Kampeni yao ni kwamba nunua miche kumi (30,000) chimba mashimo na kuweka samadi (5,000x10= 50,000), mwagilia kwa mwaka ni assumption dumu moja miche 5 na dumu moja la maji ni TZS 300 na kwa wiki nyeshea mara 2 (2x2x300x52 = 62,400) na garama nyinginezo 30,000. Jumla 172,400

Mapato: kila mti unayo potential ya kuzaa hadi embe 3,000 kwa msimu lakini wao wamechukua average ya 500/tree
hivyo unaweza kupata embe 5,000 kwa miche kumi na kila mmoja unaweza kuuza kwa sh 300 = 1,500,000 ukitoa garama laki 2 unapata faida ya sh 1.3million minimum.

Eneo kwenye compaign yao wanasema hata kama kuna eneo la bustani kima 5 meters kuzunguka nyumba yao unaweza kuotesha embe utapata kivuli lakini pia matunda yake ni fedha.

Naomba tuwaunge mkono. wao ni wakulima wadogo wa miche bora ya embe (Dodo, bolibo, Tommy, Keit, Kent, Alfonso, red Indian, Palmer, n.k) pia wanatoa ushauri kwa kweli nimevutiwa nao saaaaaaaaaaaaaana.
sikutarajia kama ningeweza kupta elimu niliyopata kwao, ukipata nafasi ya kuwa KIBITI

please pita kwenye hiki kikundi ujionee.
 
Google mango growing in kenya, utapata pdf document ya page 122, Itakusaida sana kujua aina za maembe na uzalishaji. Kwa bahati mbaya kwa tz ni 2 pages only na hazina details nyingi. Thanks.
 
This is a great opportunity indeed, for those who have land, i have 14 acres on a flat land in moshi and i have witnessed mangos doing very good yields around this region.

Changamoto ni maji kwa ajili ya kunyeshea miembe hii ikiwa bado midogo kipindi cha kiangazi, maji ya mto mdogo yapo about 1.5kilomenters.

I have no any worry about the market ..... naomba ushauri.
 
Hiki kilimo ni kizuri, pia waweza anza na hata miche michache hata 20 kisha ukaendelea taratibu.

Tunaweza, anza kwa kuwasiliana na hizo contact ulizopewa.
 
Back
Top Bottom