Msaada wa kuokoa nyumba, wadudu wanaharibu mbao

Tatizo kadiri wanavyoendelea kula mwisho wake paa litakushukia siku moja mkuu Jumanne12
Nitaongeza mbao nyingine mbovu ambazo zinaoza kirahisi maana mmiliki wa nyumba hiyo alifurahia kununua mbao za bei nafuu sasa hayo ndio majibu tusipende mteremko bila kupanda mlima ndugu yangu siku zote bure aghali
 
Waite wana maombi kuna mapepo yanataka kukupa umaskini, wakimaliza nyumba wanahamia kwengine. Jinasue fastaaaaa
 
Wakuu naomba msaada wa maarifa na jinsi ya kufanya.

Kuna wadudu wanatafuna mbao za nyumba, milango, makochi, vitanda na chochote kilichotengenezwa kwa ubao.

Wanapokula utadhani mtu anapitishisha msumeno. Utakapoona ni unga tu ukipukutika chini.
Maana yake, kama wakiendelea paa litakuwa weak; litazidiwa na uzito; na hatimaye
litananihii .... naogopa hata kusema!!

Ukibomoa sehemu iliyoliwa, unakuta shimo na unga wa kutosha unamwagika chini.
Na wadudu wenyewe ni aina ya cartepillar.

Msaada tafadhali. Suluhisho lake ni nini?

View attachment 517017
Huyu ndio mhalifu mwenyewe.​
Ulipata solution mkuu?
 
Back
Top Bottom