Msaada wa kumkamata mwizi huyu wa simu dukani

mabwiku

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
447
390
Habari wakuu, kuna rafiki yangu nipo nae mkoa, yeye anajishugulisha na biashara za simu pamoja na accesories zake na vitu vidogo vidogo.

Lakini kuna wizi ambao umeibuka katika duka lake ambao tunashindwa kuelewa ni nani huyu mwenye mchezo huu.

Mara ya kwanza watu wasiofahamika walipanda juu ya paa wakatoboa na kuzama ndani. Walikomba simu zote kwenye display, tukajaribu kufuatilia mpaka police. Tulizungushwa mpaka tukachoka maana hakuna msaada zaidi ya kutulia pesa zetu,mpaka imei namba za hizo simu tuliwapa lakini mwisho tukachoka kabisa.

Miezi 7 imepita, usiku wa kuamkia leo tena wamepanda kama kawaida yao wakatoboa juu na kuchukua simu zote zilizokua kwenye display, but this time aliweka security wa kampuni fulani, najua kampuni husika itawajibika kulipa coz mlinzi wao alikuepo.

Nadhan huu mchezo kuna mtu nyuma ya pazia manake haiwezekani kila siku yeye tu ndo anaibiwa, tunaitaji kumjua walau hata mwizi mmoja tujue muhusika manake police hawana msaada zaidi ya kupoteza muda.

Kwa mwenye mawazo na ushauri unakaribishwa, hata kama ni kuwadhibu kwa tiba mbadala pia tunapokea mawazo hayo, sababu tumechoka na hichi kitabia.
 
poleni na wizi, ushauri:
1. achaneni na imani za kishirikina ktk kumuadhibu huyo mhusika.
2. paa au dari ya hilo duka ni dhaifu. imarisheni hapo. wekeni hata security camera mumjue mhusika
3.mkishindwa kupaimarisha, hameni muwekeze sehemu nyingine
 
Afinge cctv tu kwisha kazi,me tangia nifunge nalala milango wazi,na nyumbani kwangu nilifuga mbwa,jamaa walikuwa na mchezo kama huo hapo zamani ila kabla sihafunga camera mbwa walinisaidia sana,kuba siku waliingia ndani mbwa waka wavamia ilikuwa movie tam sana na mimi niliwaacha mbwa wawaoneshe adabu asubuhi nilikuta vipande vya nyama vimezagaa uani na mishipa ya kwenye miguu ila jamaa walifanikiwa kusepa na chamoto walipata,tangia sikuhiyo kwangu naishi raha mustarehe.
 
Huo ni wizi wa kawaida sana tu. Wenzenu huwa wanafunga grill ya nondo humo ndani ya roof wakitoboa bati watanasa kwenye nondo. Kuna mmoja aliwahi kunasa mguu hapo kwenye grill. Wenyewe aubuhi wamekuja wamemkuta baado kanasa.
 
Kabla hujapata solution kwasasa Jaribu kua unazitoa hizo Simu kwenye display unapofunga duka na kuzichukua home unapolala,

Pia jaribu kua muangalifu na vijana wanaopita kwenye maduka ya simu na kujifanya wanauza perfume "Manukato"

Hua wana mchezo fulani anakupulizia perfume usoni maeneo ya Puani ili ujaribu harufu yake but hizo hua ni dawa za kulaza,utalala na watakomba kila kitu,
kuna mtu aliwahi fanyiwa hivyo ndio maana nakutahadharisha.
 
Afinge cctv tu kwisha kazi,me tangia nifunge nalala milango wazi,na nyumbani kwangu nilifuga mbwa,jamaa walikuwa na mchezo kama huo hapo zamani ila kabla sihafunga camera mbwa walinisaidia sana,kuba siku waliingia ndani mbwa waka wavamia ilikuwa movie tam sana na mimi niliwaacha mbwa wawaoneshe adabu asubuhi nilikuta vipande vya nyama vimezagaa uani na mishipa ya kwenye miguu ila jamaa walifanikiwa kusepa na chamoto walipata,tangia sikuhiyo kwangu naishi raha mustarehe.
Itabidi nikutafute mkuu. natamani sana kufuga mbwa ila sina pa kuanzia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom