Msaada wa kukadiria gharama za ujenzi

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,907
Habari wakuu .

Nataka kuanza ujenzi ule wa mdogomdogo atleast by the end of the year niwe nimepaua na kuweka grill kwenye madirisha na milango ya nje.

Ramani ina ukubwa wa m 15 x m 14 na ni nyumba ya vyumba 4, vyumba 2 ni self contained na vikolombwezo vyake vyote.

Uwanja ni tambarare na nataka kujengea tofali za kuchoma na mawe kwa msingi.

Sasa nishaurini niwe na kiasi gani kukamilisha hatua nilizozitaja hapo juu, japo kiasi cha kuanzia kipo atleast ya kukamilisha msingi around 3mln.

Ramani ya nyumba kwenye picha inafanana kama hivi na floor plni yake iko hapo chini.
View attachment 1714028View attachment 1714029View attachment 1714030
 
Attachments

  • NDENJE LAST PLAN1.jpg
    NDENJE LAST PLAN1.jpg
    30.1 KB · Views: 32
  • NDENJE LAST PLAN-1.jpg
    NDENJE LAST PLAN-1.jpg
    29.5 KB · Views: 26
  • NDENJE LAST PLAN3.jpg
    NDENJE LAST PLAN3.jpg
    33.2 KB · Views: 28
  • GROUND FLOOR.pdf
    92.4 KB · Views: 118
Habari wakuu .

Nataka kuanza ujenzi ule wa mdogomdogo atleast by the end of the year niwe nimepaua na kuweka grill kwenye madirisha na mipango ya nje.

Ramani ina ukubwa wa m 15 x m 14 na ni nyumba ya vyumba 4,vyumba 2 ni self contained na vikolombwezo vyake vyote.

Uwanja ni tambarare na nataka kujengea tofari za kuchoma na mawe kwa msingi.

Sasa nishaurini niwe na kiasi gani kukamilisha hatua nilizozitaja hapo juu ,japo kiasi cha kuanzia kipo atleast ya kukamilisha msingi around 3mln.

Ramani ya nyumba kwenye picha inafanana kama hivi
View attachment 1714028View attachment 1714029View attachment 1714030
Unaweza kumeza karibu milioni 25 ikamilike kabisa mpaka tiles
 
Habari wakuu .

Nataka kuanza ujenzi ule wa mdogomdogo atleast by the end of the year niwe nimepaua na kuweka grill kwenye madirisha na mipango ya nje.

Ramani ina ukubwa wa m 15 x m 14 na ni nyumba ya vyumba 4,vyumba 2 ni self contained na vikolombwezo vyake vyote.

Uwanja ni tambarare na nataka kujengea tofari za kuchoma na mawe kwa msingi.

Sasa nishaurini niwe na kiasi gani kukamilisha hatua nilizozitaja hapo juu ,japo kiasi cha kuanzia kipo atleast ya kukamilisha msingi around 3mln.

Ramani ya nyumba kwenye picha inafanana kama hivi
View attachment 1714028View attachment 1714029View attachment 1714030
Ukiweka floor plan ya nyumba yako nakupa mahesabu ya msingi. Mimi siyo fundi Ila nina experience.
 
Nimeiweka hapo juu kwenye post yangu
Matofali ukiyalaza utahitaji 1800 kutegemea na depth of foundation.
Blinding mifuko 5 ya cement, mchanga tani moja na kokoto tani moja na nusu.
Nondo 40 (12mm).
Ring beams 400.
Tie wire 3kg
Mbao 2X4 utahitaji 65, 2x2 at least 10.
Misumari kilo 3 (inchi 3 na 2.5).
Concrete ya beam (mkanda); Cement mifuko 25, mchanga Tani 2, kokoto tani 4.

Piga mahesabu ya uchimbaji, setting na kazi nyingine. Gharama ya msingi ni kama 5m to 6m.
 
Gharama ya msingi nyumba 14m kwa 15m ni 6 million?
 
Matofali ukiyalaza utahitaji 1800 kutegemea na depth of foundation.
Blinding mifuko 5 ya cement, mchanga tani moja na kokoto tani moja na nusu.
Nondo 40 (12mm).
Ring beams 400.
Tie wire 3kg
Mbao 2X4 utahitaji 65, 2x2 at least 10.
Misumari kilo 3 (inchi 3 na 2.5).
Concrete ya beam (mkanda); Cement mifuko 25, mchanga Tani 2, kokoto tani 4.

Piga mahesabu ya uchimbaji, setting na kazi nyingine. Gharama ya msingi ni kama 5m to 6m.
Thanks but, Nondo 40(12mm) na Ring beams 400 unamaanisha nini mkuu?
 
Mkuu tafuta professionals wanaitwa quantity surveyors, wanausoma mchoro wako nakukuaandalia makadirio yote unayoihitaji.
Ila Itabidi uongeze mchoro wa section na foundation plan.
Michoro yote ninayosema nahitaji ushauri kwa wazoefu ambao tayari wameshajenga. Mambo ya QS huwa wanakuwa na estimates za juu sana na wana consider standards materials na kanuni za kwenye madaftari sasa hii sio rafiki kwa watu wa kawaida, ni proper kwa serikali na kwa wanaojenga maghorofa huko
 
Mkuu tafuta professionals wanaitwa quantity surveyors, wanausoma mchoro wako nakukuaandalia makadirio yote unayoihitaji.
Ila Itabidi uongeze mchoro wa section na foundation plan.
Watamtia gharama za kutosha, ni heri akamate mafundi local ambao wameshajenga nyumba nyingi watakua na uzoefu wanaweza kumpa makadirio, sijui lakini kila mtu anavyoona ila kwangu nilifanya hivyo na iliniokorla gharama sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni nyumba yako binafsi unataka kujenga mkuu? Nimeicheck chap chap naona ina changamoto za kimpangilio. Kwa mfano kuna corridors nyingi sana na nyembamba mno. Zitakuwa giza na ngumu kutumia (corridor za 90cm ni minimum kabisa). Vyumba vya kulala vidogo Kama bado hujaanza kujenga nakushauri urekebishe design

Pia angalia vyoo vilivyowekwa. Vyembamba na virefu bila, utatumia tiles nyingi kuliko unavyohitaji. Nahisi wazo la choo na bafu ni kuwa na washbasin kwa nje kwenye hizo vestibule za bafuni...hayo ni mambo ya zamani na hiyo basin itakuwa gizani (taa itakuwa inawashwa 24/7 na hewa itakuwa nzito).

Ningeshauri uweke washbasins ndani ya vyumba husika. Dining Room ya 2.2m ni changamoto kuweka meza na viti pande zote mbili, watu wakae na kuvuta viti na wapishane (mtu kuweza kupita nyuma ya aliyekaa).
 
Thanks in but,Nondo 40(12mm) na Ring beams 400,unamaanisha nini mkuu?
Inategemea na utakavyojenga mkanda wako. Bado unaweza kuondoa mambo mengi na kusevu hela.
Ila, nyumba yako ina kuta nyingi sana. perimeter karibu 110m na hapo bila veranda.

Sasa 110 m matofali na reinforcement ya msingi/ au hata kama utatumia mawe bado itakugharimu.

Halafu huyo jamaa aliyekuchorea, amekufanya uamini nyumba yako ni 15 X14 ila ni ndogo kuliko, na eneo kubwa la mchoro huo siyo livable.
All in all, wewe ndiyo mwenye nyumba na una matamanio yako, ila ningependa uje utuletee mrejesho. Kwa sababu naamini bila 6m au at least 4m ukijibana sana, bado hujajenga msingi.

Again, hiyo ni based on experience, mimi siyo fundi.
 
Back
Top Bottom