Msaada wa kuhama kutoka idara Msingi kwenda idara nyingine

braity

JF-Expert Member
May 24, 2020
354
442
Habarini ndugu mabibi na mabwana,
Nijikite moja kwa moja kwenye mada kama kichwa kinavyoelezea.
Naomba msaada kwa mwl yoyote au mdau yeyote wa Elimu aliyewahi kufanikisha swala la kubadili idara ya kufanyia kazi.
Mimi ni mwalimu nafanya kazi idara ya Msingi na nina hamu nihamie vyuo vya kati, hususani Vyuo vya Ualimu (cheti) kufanya kazi huko. Naomba nifahamu ni hatua zipi naweza kuzifuata kufanikisha hili.
Sifa zote ninazo na Cv yangu ipo sawa.
Naamini kupitia humu tuna maafisa Elimu, wakufunzi, wadau mbalimbali wa Elimu wanaoweza kutusaidia mawazo na mwongozo mzuri wa kufikia tuyatakayo. Ahsanteni
 
Hongera kwa kuwa na wazo hilo, cha msingi kwanza nikupambana uwe na uhakika kule unakotaka kwenda kama kuna nafasi baada ya hapo utaandika barua kwa katibu mkuu wizara ikipitia kwa mwajiri wako kuomba kuhamia au kwenda kuhudumu katika nafasi hiyo.

NB
Anuani katika barua utakayo andika ni
1. Anuani yako
2. Katibu mkuu wizara
3. Mkurugenzi wa halmasahuri yako
4. Afisa Elimu WILAYA
5. Mkuu wako wa shule
Nina imani kwa hayo maelezo kidogo yatakusaidia ndugu yangu na zaidi ya yote Mungu akutangulie katika mapambano yako.
 
Unataka tu kuonekana huko au kuna unachokifata? manake kama unazo sifa ina maana mshahara wako na hao wa huko hakuna tofauti!!
 
Hongera kwa kuwa na wazo hilo, cha msingi kwanza nikupambana uwe na uhakika kule unakotaka kwenda kama kuna nafasi baada ya hapo utaandika barua kwa katibu mkuu wizara ikipitia kwa mwajiri wako kuomba kuhamia au kwenda kuhudumu katika nafasi hiyo.

NB
Anuani katika barua utakayo andika ni
1. Anuani yako
2. Katibu mkuu wizara
3. Mkurugenzi wa halmasahuri yako
4. Afisa Elimu WILAYA
5. Mkuu wako wa shule
Nina imani kwa hayo maelezo kidogo yatakusaidia ndugu yangu na zaidi ya yote Mungu akutangulie katika mapambano yako.
Nashukuru sana kwa Mwongozo wako ndugu yangu ubarikiwe sana
 
Hongera kwa kuwa na wazo hilo, cha msingi kwanza nikupambana uwe na uhakika kule unakotaka kwenda kama kuna nafasi baada ya hapo utaandika barua kwa katibu mkuu wizara ikipitia kwa mwajiri wako kuomba kuhamia au kwenda kuhudumu katika nafasi hiyo.

NB
Anuani katika barua utakayo andika ni
1. Anuani yako
2. Katibu mkuu wizara
3. Mkurugenzi wa halmasahuri yako
4. Afisa Elimu WILAYA
5. Mkuu wako wa shule
Nina imani kwa hayo maelezo kidogo yatakusaidia ndugu yangu na zaidi ya yote Mungu akutangulie katika mapambano yako.
Hapa kwenye anuani ya Katibu imenichanganya kidgo. Ni katibu mkuu utumishi au Katibu mkuu wizara ya Elimu? Naomba msaada wa hilo brother!! Ahsante
 
Mkuu jaranono wale ni wakufunzi wa vyuo (tutors) viwango vya mishahara vimetofajtishwa na walimu wa elimu msingi/sekondari usikariri kwenye kwamba kwa kuwa ni mwalimu basi mshahara ni uleule hapana
Na hvi vyuo viko chini ya NACTE
Mkufunzi mwenye degree anaenza kazi ana level moja ya mshahara na anayefundisha University anae anza kazi na aliye na degree kaka yeye
The same to masters etc......
Wale wako vizuri kuliko anakotaka kutoka jamaa mwache apambane
 
Hapa kwenye anuani ya Katibu imenichanganya kidgo. Ni katibu mkuu utumishi au Katibu mkuu wizara ya Elimu? Naomba msaada wa hilo brother!! Ahsante

Nafikiri ingawa sina uhakika vyuo vya Kati viko chini ya katibu mkuu Tamisemi
N.B
Fanya uchunguzi ili uwe na uhakika
 
Vyeo vya kati vipo wizara ya elimu.viko chini ya nacte
Sio sahihi vyuo vya elimu vya kati viko chini ya katibu mkuu wizara ya elimu vile vya afya vya kati viko chini ya katibu wizara ya afya na waajiri wao ni makatibu siyo nacte.
 
Nadhami hujamuelewa yeye ameongelea Kuhusu kusimamia vyuo vya kati vinasimamiwa na NACTE na universities vinasimamiwa na TCU hizo taasisi haziajiri kwa upande wa watumishi huko sah8hi
 
Back
Top Bottom