Msaada wa kuchapisha kitabu

KUNO NA KUNO

Member
Jul 11, 2014
7
2
Wandugu wapendwa. Salamu nyingi sana.
Mimi ni mwanachama wa JF kwa kitambo sasa. Nina ombi ninaloomba waungwana mnisaidie. Nimeandika mswada wa kitabu kinaitwa Harakati za Fungate, Lizame Tugawane Mbao. Kitabu hiki kina mambo mengi ya kijamii (sana) kinazungumzia mtu mmoja aliyezaliwa kijijini tena kusikofika hata magari, ni maskini kuanzia unyayoni hadi kwenye unywele! Akapata bahati ya kufaulu, babake akashindwa kumsomesha, ikafikia mzee wake akapelekwa mbele ya baraza ashtakiwe kwa kushindwa kusomesha mtoto wake wakati ana mifugo hasa mbuzi na kuku, ikabida auze kuogopa kufungwa. Pia huyo bwana akapata ufadhili wa kigeni kwenda kusoma nje, akiwa huko akawa anawaza tu watu wake kijijini na tabu za maisha, alipomaliza masomo akarudi nchini, ila akabadili mfumo wa maisha akalewa na madaraka, akasahau kwao akajichanganya na maisha ya peponi....

huo ni muhtasari tu, natamani waungwana, mkiweo JF mnisaidie kuchapisha kitabu hiki kiifikie jamii. Naomba kuwasilisha wandugu!

kwa mawasiliano tafadhali tuwasiliane kwa disabilityhabari@gmail.com au 0777004455
 
Good,bt how exactly you wish you had had been assisted?,uchangiwe hela au uoneshwe sehem ya kuchapisha?,me cjakusoma ndungu mwandishi
 
Nenda business printers,wale watoaji wa magazeti ya majira,ukifika hapo,mtafute mr msami,au kombe,wao mtakubaliana jinsi ya kuchapisha,at the end watakupa percent ya uandishi baada ya kitabu kutoka.
 
Back
Top Bottom