Msaada wa kuagiza gari online

adata5

Member
Jan 17, 2013
69
8
Wadau me ni mfanyakazi serikalini nimejichanga hela nimepata tumilioni 8.8 Nataka kuagiza gari noah 2001 au 2004 nahitaji msaada katika mambo yafuatayo
FOB
CIF
BID
Hivyo vyote vina maana gani na dealer gani wanabei nzuri yaani website gani e.g BE FOWARD OR JAPAN USED CAR OR SBT JAPAN ambao mawakala wao wapo bongo yaan nisiliwe hela na gharama za kodi zipoje yaan napigaje hadi nilifikishe mlangon
Halafu nimesikia wafanyakazi wa serikali bei zao za kodi zipo chini kuna ukweli katika hili na ninafanyaje hili nipate punguzo hilo
NATANGULIZA SHUKRAN ZANGU ZA DHATI KWA WATAKAOSAIDIA
 
Nenda kwa wakala wa beforward watakusaidia sana ila watakuchaji pesa ya clearing and forwarding laki mbili na nusu
 
Shukran mkuu nazani umenipa mwanga sehemu ya kuanzia ngoja niangaike nikishindwa nanunua showroom za bongo hapa hapa nisije nikakila kihela chenyewe bure
 
Nenda kwa wakala wa beforward watakusaidia sana ila watakuchaji pesa ya clearing and forwarding laki mbili na nusu
hao jamaa ni uhahika na gharama zao sio kubwa sanaBei unayotakiwa kuielewa ni CIF,Maana ni bei itakayojumlisha bei ya kununulia na kuisafirisha hadi Tanzania,kuhusu kuitoa hapo ni kazi ya mawakala,unaweza kuwapata kupitia Welcome to GariYangu.Com lakini kama utanunua TOYOTA, NOAH, MODEL AZR60G,basi gharama ya kuitoa bongo itakuwa niCustoms Value 4,250.00 USDImport Duty 1,062.50 USDDumping Fee 1,062.50 USDExcise Duty 265.62 USDVAT 1,195.31 USDTotal Taxes 3,585.93 USDna gharama ya kuinunua itakuwa ni USD 2500 hii ni CIF
 
Sahau hiyo habari ya wafanya kazi wa serikali kupata punguzo la kodi. Hiyo iliishaondolewa kwa taarifa nilizo nazo. Jiandae kulipa all taxes in full.

Tiba
 
Mkuu sijakuelewa vzr hapo kwenye gharama,tafadhali fafanua!
 
Mkuu sijakuelewa vzr hapo kwenye gharama,tafadhali fafanua!

kama alivyosema mdau mmoja hapo kuwa hakuna tax exemption kwa wafanyakazi,ipo kwa wabunge tu,hapo ndipo utakapoishangaa Tanzania na wanaotaka kutuletea ukombozi wa 2,kwanini iwe kwa wabunge na sio walimu tena wa shule za msingi wenye mishahara duni?

turudi ktk mada
Jiandae kulipa kodi yenye jumla ya Tanzanian shilingi USD 3,585.93 + na bei ya kuinunua gari hadi ifike Tanzania USD 2500 =USD6,085.93 Ni kama milioni 9737488 hadi gari inatoka. hapo bado hujalipa pesa ya wakala na plate no na mengine.hayo ni makadilio tu.
 
Mengi ushaambiwa

FOB = ni bei ya gari kule japani

CIF = bei ya gari japani + usafiri kutoka japani mpaka hapa (freight) + insurance

me nipo katika kampuni wa japanees hapa dar kama utapenda ni pm nitakusaidia zaidi!!
 
halafu kuna jamaa mmoja alitolea gari bandari ya mombasa hivi kule kuna unafuu kuliko huku kwetu au kunafanana msaada kwa wanaojua hilo
 
halafu kuna jamaa mmoja alitolea gari bandari ya mombasa hivi kule kuna unafuu kuliko huku kwetu au kunafanana msaada kwa wanaojua hilo
Zamani tulikua tunasema kua kwenye Boda (mipakani) wanatoaga Charges ndogo za kodi kuliko Makao Makuu Dar es salaam. Hivyo kodi ya Gari kwa Bandari ya Dsn ilikua kubwa zaidi kuliko ukilipitishia mpakani kutokea Mombasa. But siku hizi system iko Centralized so hauokoi kitu chochote kwenye upande wa kodi. Unaweza ku-save vitu vingine kama time na port charges maana Mombasa wanapakua kwa muda mfupi zaidi kuliko DSM, lakini huo umbali wa kuendesha from Mombasa tu DSM ni extra cost zingine.

Kwa kukushauri tu kama hujajipanga basi pitishia gari Zanzibar na ulisajili kulekule (hapo kodi ni ndogo), Kisha livushe hilo gari kama limekuja tu kutembea ambapo kuna hela kidogo (Faida za Muungano) utalipia ya kutumia namba za Zanzibar huku bara. Hapo utakua ukitafuta hiyo kodi taratibu na siku ukiipata unawapa different ya kodi (Bara - Zanzibar), then mambo poa.
 
Mkuu shark kweli una mauzoefu umenifumbua macho ngoja nikomae hapahapa bongo kula like hiyo:thumbdown::thumbdown::thumbdown:
 
Sahau hiyo habari ya wafanya kazi wa serikali kupata punguzo la kodi. Hiyo iliishaondolewa kwa taarifa nilizo nazo. Jiandae kulipa all taxes in full.

Tiba

We jamaa Ni muongo Sana kama kitu hukijui kaa kimya au uliza, inawezekana akapata msamaha ikiwa Tu gari haijazidi miaka kumi tangu itengenezwe na anatakiwa afanye kazi kwa muda usiopungua miaka miwili. Na msamaha anaoupata ni excise duty on import na import duty pia gari isizidi CC 3000
 
Mkuu nokla safi sana hapa ndo nilikuwa napataka ngoja nikomae na ofisi nitajua nitaanza wapi na kumaliza wapi nitakuja na majibu wadau den nitaona nimesevu sh ngapi
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom