Msaada wa kisheria

Msaranga

JF-Expert Member
Feb 10, 2009
956
227
Naomba kujua yafuatayo sheria inasemaje.
Mfano mwanaume ameoa mke wa ndoa na hawana watoto kabisa na ikatokea yule mwanaume akafariki na wakati kabla hajafariki aliacha osia kuwa atakayeridhi mali zake zote ni mtu mwingine kabisa labda mtoto wa kaka yake. Sasa hapo sheria inasemaje kwa yule mke wa ndoa ataachwa bila kitu au anaweza kudai.naomba kujua kutoka kwa wanasheria.
 
Mirathi inatawaliwa na sheria tatu hivi, lakini kwa waafrica ni mbili. ya kimila au ya ki-islamu. We ni muumini wa ipi kati ya hizo. Then tutapeana mawazo
 
mfano mimi mkristo inakuajae tafadhali
 
mfano mimi mkristo inakuajae tafadhali

Sheria ya kimila inakutawala. Huruhusiwi kujichagulia sheria ipi itumike (kuna sheria ya kiserikali ambayo ni ya tatu, ya ki-islamu haikuhusu kabisa). Haki ya mke katika matrimonial property and its division inamlinda sana mwanamke. atamdai msimamizi wa mirathi jasho lake alilochangia katika mali waliyochuma pamoja, hata ile ambayo alimkuta nayo mume kama iliendelea kutumika na wana ndoa pamoja. Mke sio mrithi wa mali za mume katika sheria ya kimila. Hivyo mke atadai jasho lake tu. Kama mume hana watoto au wajukuu, basi warithi halali ni dada na kaka zake wa tumbo moja-baba na mama mmoja.
 
sheria ya mirathi ya ipo wazi kidgo, inampa marehem maamuzi ya nani ampe wosia, halazimishwi wala hachaguliwi m2 wa kumpa wosia, kama aliamua wosia wake uende kwa m2 mwingine ni sawa, lakini mali hiyo katika wosia isiwe mali ya wanandoa, bali iwe ya marehem.
kama ni mali ya wanandoa, mke atatakiwa apate sehem yake kama sehem ya jasho lake.
kuna kesi ambazo zimeshawahi kuamriwa, kuwa marehem ana haki ya kumchagua m2 wa kumuandika kwenye wosio, akiwa katika utimamu wa akili.
 
Kuwa makini kidogo, na maelezo yako. Unasema wosia au urithi? Yote si kweli, wosia hawezi kumpa mrithi mmojawapo autunze, sheria inakataza. Unapewa mtu ambaye sio mrithi autunze kama haukutunzwa benki, msikitini, kanisani etc. Na urithi hivyo hivyo hawezi kumnyima mrithi halali bila sababu ya msingi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom