Msaada wa kisheria

Entreprenuare

JF-Expert Member
Aug 24, 2019
1,616
1,712
Nina maswali 2 hapa.

1. Kwa mfano siku ya kwenda mahakamani imefika, imetokea mshtakiwa wako amefika alafu wewe mshtaki hujafika hiyo siku, mahakama huwa inatoa tamka gani, au nini kitafuata? Au umeamua hiyo kesi uipotezee kabisa ila bila kutoa taarifa mahali popote, ila mda huo mshtakiwa wako yupo nje kwa mdhamana.

2. Jinsi gani unaweza kudai fidia juu ya mshtakiwa wako, i mean zile cost ambazo ulikuwa unaingia wakati unafuatilia kesi kuanzia kituo cha polisi mpka kufika mahakamani, cost kama za usafiri, etc....
 
1. Usipofika mahakamani na mshitakiwa akafika kesi huahirishwa na mshitakiwa anahesabiwa hudhurio. Iwapo mlalamikaji hatafika kwa mahudhurio matatu shitaka huondolewa na mshitakiwa kuwa huru.

Iwapo hutaki kuendelea na shitaka unatakiwa kuitaarifu mahakama ifute shitaka bila ghalama yaani hapo mlalamikiwa halipi hata mia.

2. Ukiitelekeza kesi mahakamani, mshitakiwa hakulipi hata senti yaani ghalama za mgambo, polisi, kufungulia kesi mahakamani, usafiri na mengineyo. Ghalama kama hizo hujumuishwa wakati wa hukumu hivyo kitendo cha kutelekeza kesi unakuwa umekubali yaishe bila ghalama labda itokee mfanye makubaliano na mlalamikiwa nje ya mahakama.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom