Neemandandika
Member
- Aug 25, 2014
- 29
- 4
Habarini wakuu, naomba niende moja kwa moja kwenye tatizo langu.
Mimi nimejiriwa katika kampuni binafsi, hapo nyuma kumetokea tatizo kazini hivyo mimi na wenzangu watatu tuna kesi polisi na polisi wanaendelea na uchunguzi wao.
Mwenzangu mmoja yeye amekubali ku resign na mwingine alikuwa ameshaacha kazi. So ishu imebaki mimi kwani bado sijaridhia ku resign.
Mshahara wa mwezi August 2019 bosi alikata pesa yake yote aliyokuwa ananida tofauti na makubaliano ya kukata kidogo kwa awamu tatu, hii ilikuja ghafla baada ya kuona nina kesi ambapo alitarajia ningekutwa na hatia hivyo anifukuze kazi ilihali yeye amekwisha chukua chake.
So pesa kidogo iliyobaki ndiyo akaipeleka bank kama mshahara wangu na kuwaambia bank kuwa mimi nina kesi hivyo wafanye juhudi ya kupata pesa zao kwani soon angenifukuza kazi.
Bank walikatapesa yao hivyo mimi mwezi huo sikupata hata senti. Tofauti na matarajio ya bosi kesi bado iko polisi hivyo imemlazimu kunilipa tena mshahara wa September-2019 ambapo alipeleka mshahara wote bank, bank wamezuia pesa zote na nilipotaka kujua kwa nini wamezuia nikajibiwa bosi wangu kawapa taarifa kuwa hana uhakika kama anilipa tena mshahara mwingine kwani naweza kutwa na hatia hivyo kufukuzwa kazi. So na mwezi huu sijapata kitu.
Kisheria bado ni mfanyakazi wa hiyo kampuni hivyo siruhusiwi kufanya kazi sehemu nyingine.
Utata ni
1: Je bank wanahaki ya kukata pesa zangu zote?
2: Je bosi wangu anaruhusiwa kuwapa bank hizo taarifa bila hata mimi kunihusisha ilihali hata kesi mahakamani haijafika?
Wakuu wapi naweza pata/peleka swala langu hili kupata msaada wa kisheria kama jambo hili nimeonewa ama lina make sense.
Asanteni