MSAADA WA KISHERIA

Salam zenu ndugu wana JF.

Husika na kichwa cha topic naomba msaada wa kisheria kwenye haya ninayoyapitia,

Baada ya kumaliza form 6 (results hazikuwa Poa) nikabaki kitaani kiniwaza la kufanya bahati nzuri nikapata kazi kwenye kibanda cha money services (mpesa, tigo pesa na crdb fahari) maisha yakaendelea mdogo mdogo (slary ndogo 200000) sema kwa kuwa nipo home bado nikaona isiwe shida kuliko kushinda naomba omba hela Za kunyoa bora nikomae nikiwaza yajayo.

Tatizo limekuja wiki iliyoisha baada ya kutapeliwa pale kwenye kibanda na matapeli Kwan kwenye hela walizonipa niwatumie kwenye mpesa walinichanganyia na za bandia japokuwa wakati nahesabu niliona ziko sawa ila baadae wakawa nikama namba wamesahau mpaka wampigie mhusika na wakazitaka ila ndani ya sekunde kadhaa wakanirudishia kuwa namba ndo yenyewe wameikumbuka nitume, na mm sikuona mabadiliko yoyote nikasesabu mafungu maana nsahesabu mwanzo zikawa sawa nikawatumia.

Kesi ilikuja wakati WA kukabidhi kwa boss akagundudua mia 6 na 70 ni bandia, ilinichukua muda kuamini ila ndo hvyo hata mm niligundua haziko sawa. Huyu boss anataka nizilipe hvyo almost miezi 4 ntafanya kazi bure bila hata mia wakati hata police hajareport. Nawaza kuacha hii kazi ila sina hata hela ya kumpa na nikimwambia najua hatanielewa.

Naomba msaada wa kisheria kwa mwenye uzoefi na kesi kama hii.
Mbaya zaidi iwe mchezo umechezwa na bosa mwenyewe.

Maisha ni mzunguko sana.
 
Ukimsababishia mwajiri wako hasara anayo haki na jukumu la kukata mshahara wako ili kufidia hiyo hasara.

Ingawa kaa nae chini muongee ili asiwe anakata mshahara wote mkuu.
Kama ataendelea kukata mshahara wote.

Hapo atakuwa anakutengenezea mazingira ili uache kazi. In legal perspective, we call it CONSTRUCTIVE TERMINATION.

Kwa msaada zaidi uje ofsini kwangu mkuu uchangie consultation fee maana hii ni NOBLE PROFESSION.
 
Duh thanks, na nikikimbia kazi nashitakiwa?
 
Duh thanks, na nikikimbia kazi nashitakiwa?
Ingewezekana mngekaa na kuongea kibinadamu, tatizo tukishakuwa boss ni order kwenda mbele na kuogopwa kwa sana, hata uhuru wa majadiliano haupo kwa hiyo inakuwa ngumu kwako, unabaki kuomba misamaha tu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom