Naomba ushauri wa kisheria namna ya kumshughulikia jirani anayenitukana

Amzibue ya kutosha mpaka akili imkae
Aaah nimekua nikisoma na kuambiwa kua Ni kosa la jinai kujichukulia sheria mkononi kama hakuna uladhima wa kufanya hivyo....
Yani ingekua ni kama njia ya kufanya self defence basi ingenibidi nifanye hivyo..
Lakini kwasasa yanipasa kutumia njia sahihi.
 
Habari wana JF.

Nilikua naomba kupata clarification kidogo ya kisheria kuhusiana na jambo hili Kuna mtu(Mpangaji mwenzangu) amekua akinizingua sana kwa kunitukana kwa matusi na wakati mwengine kutoa kauli za vitisho.

Hivi sasa ni mara ya 3. Nilibahatika kumrekodi kwa njia ya simu week kama mbili zimepita na nilipotaka kumchukulia hatua za kisheria Mama mwenye nyumba aliingilia kati na kusuruhisha suala hili.

Lakini leo karudia tena ingawa sikubahatika kumrekodi. Je naweza kufungua kesi na kutumia hizo previous records kama ushahidi au haziwezi tumika tena kama ushahidi kwasababu ni muda mrefu kidogo umepita sasa.

Nikihofia kua maybe nitaulizwa kwanini sikuja kufungua kesi wakati ule?

Hivyo mwenye uelewa wa kisheria naomba msaada, unazungumzia nini kuhusu scenario kama hii.
Si uhame tu ili uepuke huo ukorofi wake
 
Back
Top Bottom