Naomba ushauri wa kisheria namna ya kumshughulikia jirani anayenitukana

Symonjerry

Member
Nov 16, 2017
68
86
Habari wana JF.

Nilikua naomba kupata clarification kidogo ya kisheria kuhusiana na jambo hili Kuna mtu(Mpangaji mwenzangu) amekua akinizingua sana kwa kunitukana kwa matusi na wakati mwengine kutoa kauli za vitisho.

Hivi sasa ni mara ya 3. Nilibahatika kumrekodi kwa njia ya simu week kama mbili zimepita na nilipotaka kumchukulia hatua za kisheria Mama mwenye nyumba aliingilia kati na kusuruhisha suala hili.

Lakini leo karudia tena ingawa sikubahatika kumrekodi. Je naweza kufungua kesi na kutumia hizo previous records kama ushahidi au haziwezi tumika tena kama ushahidi kwasababu ni muda mrefu kidogo umepita sasa.

Nikihofia kua maybe nitaulizwa kwanini sikuja kufungua kesi wakati ule?

Hivyo mwenye uelewa wa kisheria naomba msaada, unazungumzia nini kuhusu scenario kama hii.
 
Nenda kamshitaki mahakamani kwa jinai
Lugha ya matusi au kukutishia
Mahakama ya mwanzo hapo unapo ishi
Si lazima kuanzia police sheria ina kuruhusu
 
Habari wana JF.

Nilikua naomba kupata clarification kidogo ya kisheria kuhusiana na jambo hili Kuna mtu(Mpangaji mwenzangu) amekua akinizingua sana kwa kunitukana kwa matusi na wakati mwengine kutoa kauli za vitisho.

Hivi sasa ni mara ya 3. Nilibahatika kumrekodi kwa njia ya simu week kama mbili zimepita na nilipotaka kumchukulia hatua za kisheria Mama mwenye nyumba aliingilia kati na kusuruhisha suala hili.

Lakini leo karudia tena ingawa sikubahatika kumrekodi. Je naweza kufungua kesi na kutumia hizo previous records kama ushahidi au haziwezi tumika tena kama ushahidi kwasababu ni muda mrefu kidogo umepita sasa.

Nikihofia kua maybe nitaulizwa kwanini sikuja kufungua kesi wakati ule?

Hivyo mwenye uelewa wa kisheria naomba msaada, unazungumzia nini kuhusu scenario kama hii.
Zinaweza kutumika. Lakini utatakiwa uzingatie taratibu za kuwasilisha ushahidi wa kielektroniki, lazima uelezee namna gani ulirekodi na namna gani ulihifadhi rekodi hiyo bila kuchezewa na mtu mwingine (kuedit)
 
watanzania mpoo waoga sanaa

wee mchabangule makofi ya kutosha kabisa alafu yeye ndio akimbilie kwenye sheriaa……………..
 
Mkuu samahani nina swali nje mada,

Kodi yako hapo inaisha lini??
Muda wa kodi uliobaki sio issue
Issue ni sehemu niliyopanga ni potential sana kwangu kiasi cha kwamba siwezi kuwaza kuondoka eneo hilo kulingana na nature ya harakati za kimaisha ninayoziendesha ambapo hadi sasa nishajenga msingi wa kimaendeleo kwa takribani miaka miwili sasa kupitia nyumba niliyopanga.
 
Bado hajapata makwazo hapo,yakikolea yeye mwenyewe ataiacha nyumba hata Kama kodi bado haijaisha
Kuondoka nataka ndo iwe njia ya mwisho kabisa kati ya machaguo mengine.
Na ndo mana najaribu hata kutumia vyombo vya kisheria kuweza kulitatua jambo hili
 
Zinaweza kutumika. Lakini utatakiwa uzingatie taratibu za kuwasilisha ushahidi wa kielektroniki, lazima uelezee namna gani ulirekodi na namna gani ulihifadhi rekodi hiyo bila kuchezewa na mtu mwingine (kuedit)
Nadhani namna ninayoweza kueleza na ikaeleweka kua ni kwa namna gani nilirekodi ni kwa njia ya simu ya mkononi.
Ambayo ni simu yangu mimi binafsi isiyojihusisha na mtu mwengine kwa namna ambayo haitoharibu ushahidi wala kuchezewa ushahidi
 
Upo sahihi. Ukifika hatua hiyo ni vyema uwaone wanasheria wakusaidie jinsi ya kuweka vyema hicho kiapo kitachoeleza hayo.
 
Back
Top Bottom