Msaada wa kisheria unahitajika kuhusiana na jambo hili

Symonjerry

Member
Nov 16, 2017
68
86
Habari wana JF.

Nilikua naomba kupata clarification kidogo ya kisheria kuhusiana na jambo hili Kuna mtu(Mpangaji mwenzangu) amekua akinizingua sana kwa kunitukana kwa matusi na wakati mwengine kutoa kauli za vitisho.

Hivi sasa ni mara ya 3. Nilibahatika kumrekodi kwa njia ya simu week kama mbili zimepita na nilipotaka kumchukulia hatua za kisheria Mama mwenye nyumba aliingilia kati na kusuruhisha suala hili.

Lakini leo karudia tena ingawa sikubahatika kumrekodi. Je naweza kufungua kesi na kutumia hizo previous records kama ushahidi au haziwezi tumika tena kama ushahidi kwasababu ni muda mrefu kidogo umepita sasa.

Nikihofia kua maybe nitaulizwa kwanini sikuja kufungua kesi wakati ule?

Hivyo mwenye uelewa wa kisheria naomba msaada, unazungumzia nini kuhusu scenario kama hii.
 
Back
Top Bottom