Msaada wa Kisheria: Nimenunua Fremu nimepata changamoto hii

Dseni

Member
Aug 13, 2012
33
125
Shida iko hivi...

Nilinunua fremu 2 kwa mtu: tuliandikisha makubaliano Serikali za Mitaa (Mtaa wa Mivumoni, kata ya WAZO, wilaya ya Kinondoni- Dar es Salaam). Zile fremu nikazifanyia marekebisho (renovation). Na nilizikodisha kwa watu zote.

Hata hivyo, Baada ya mwaka sasa kumbe yule mtu aliyekuwa ameniuzia tayari alikuwa ameshaingia mkataba na mtu mmoja ambaye alizinunua frem hizo lakini hakumalizia pesa.

Walikubaliana kwa Tsh milioni 6 lakini yule aliyenunua alitanguliza Tsh. Milioni 2 ikabaki milioni 4. Baada ya kudaiana kwa muda mrefu walikubaliana kuvunja makubaliano yao kwa masharti kwamba auze frem hizo, na baada ya kuuza, basi alirudishe ile milioni 2.

Lakini kwa bahati mbaya sana huyu muuzaji aliponiuzia hizo fremu (kwa milioni 6 cash) Hakumpa hela yule mnunuzi wa awali ile pesa aliyoitanguliza na badala yake alimpa Tsh. Laki 7 tu na ikabaki Milioni 1 na laki 3. Pesa ambayo mpaka sasa hajamlipa yule mnunuzi wa awali.

Baada ya kudaiana kwa muda mrefu huyu jamaa anayedai aliamua kwenda kwenye BARAZA LA ARDHI LA USULUHISHI LA KATA YA WAZO ambapo baraza liliandika STOP ORDER kwamba kazi yoyote isifanyike hapo mpaka yule mdai alipe pesa yake.

Binafsi nilienda barazani kuwaambia kwamba zile fremu ni mali yangu. Naye alikiri kwamba ameuza kabisa. Hata hivyo BARAZA wamesema hizo fremu ziko kwenye mgogoro kwa hiyo HAKUNA BIASHARA YOYOTE KUFANYIKA mpaka Huyu mnunuzi alipwe deni hilo.

Hata hivyo, huyu mdaiwa anataka dhamana ibadilishwe; yaani kutoka kwenye fremu zile alizouza ili iende kwenye nyumba yake anayoishi.

Lakini baraza wamekataa kabisa wanasema fremu ziko kwenye mgogoro. Na kwamba STOP ORDER itatoka ikiwa tu huyu mdaiwa atalipa.

Swali:
1. Je ni sheria gani inayowapa mamlaka watu wa baraza kuweka STOP ORDER kwa eneo ambalo tayari lilishauzwa?

2. Kwa kuwa muuzaji walivunja mkataba wa awali na wakakubaliana kulipana, mimi naingiaje kwenye kesi hii?

3. Kwa kuwa huyu mdaiwa anataka kuhamisha dhamana ili frem ziendelee kufanya kazi, je kwa nini baraza wanakataa?

Au kuna harufu ya rushwa!

Naomba Msaada
0769080629

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mirisho pm

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
3,525
2,000
Ningekuwa wewe kama kuna biashara nin ningemlipa huyo jamaa kwa makubaliano na muuzaji wa awali..... tena anaweza kupa na ardhi kabisa... achana na mambo ya sheria tumia busara kiongozi
 
papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
3,815
2,000
sio kila vita lazima uipigane, sometimes step back!, wewe intervene, mwite muuzaji na huyo mdai wake mbele ya hilo baraza la ardhi, mchnae huyo mdai mil1 hivi au kama unaweza mchane 1.3mil yote chini ya usimamizi wa baraza la ardhi, alfu hiyo amount iweke kama deni kwa huyo muuzaji kama atakulipa sawa, asipo kulipa poa tuu kwisha...kulikoni kupata hasara kubwa zaidi,

Tena upo uwezekano mkubwa kabisa wa hao wawili ( muuzaji na huyo mdai) wanakuchezea ka mchezo kakutaka kukudhuru hizo frem, hivyo usiwape muda wa kwenda mahakaman/ mabarazani, na kuanza kukuzuga zuga huku wakiwa na lao jambo, migogoro mingi ya ardhi inachukua muda mrefu na mwisho wewe ndiye utakuwa mwathirika wa maamuzi..............
 
mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,478

Mlipe huyo mnunuzi wa awali halafu huyo aliyekuuzia wewe akupe hati yake ya nyumba kama dhamana ya hiyo 1,300,000 uliyomlipa huyo jamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom