Msaada wa kisheria: Nilimpa mimba mke wa mtu, mtoto amefanana sana na mimi, nitampataje?

Rafiki yangu, mbona habari zako Mimi ninazo tayari? Wewe Fanya hivi, najua # ya simu yangu unayo, nipiie usiku saa 4 hivi tutengeneze appointment wrote watatu na mtoto wako wa nne ili uje nikukabidhi bidhaa yako bila shida!! Fanya hivyo usiogope.
Akiuona huu ujumbe jamaa lazima ajikojolee kwanza bila kujua....
 
Nawasalimu wanajf,

Naandika nikiwa na majonzi, huzuni na masikitiko moyoni na usoni.

Katika harakati za hapa na pale, nilikutana na mdada ambaye baadae katika kufunguka aliniambia kuwa ni mke wa jamaa mmoja ambaye katika kunielekeza vizuri nikagundua niliwahi fanya naye kazi ya muda miaka kadhaa iliyopita. (Note : wakati ananieleza haya tayari nilishamgegeda mara moja ).

Baada ya kutambua hayo nilichukua uamuzi wa kuachana naye mara moja, lakini aliniomba sana ila niliendelea na msimamo wangu, alikubaliana na matokeo kwa sharti na ombi la tuandae pambano la mwisho la kuagana, nlikubali kwa shingo upande. Kabla hatujapanga vizuri akapata taarifa kuugua mama mkwe wake kijijini, alienda kumuuguza.

Baada ya wiki tatu akanipigia simu anarudi, na anataka apitie ninapokaa kabla hajaenda kwake kwani alinibebea zawadi(tunaishi Wilaya moja ila tofauti mitaa tu), nilimkubalia na akafika ghetto.

Baada ya stori za hapa na pale, tukajikuta tupo ulingoni, lakini kabla ya mshindo akanisihi kuwa yupo siku hatari hivyo ni-withdrawal(nimwage nje) lakini kutokana na hali ilivyokuwa tulishindwa kufanya hilo. Tulimaliza rounds kadhaa akaenda zake, kibaya mumewe alikuwa amesafiri kikazi na alirudi baada ya wiki. Baada ya muda alinipa taarifa za ujauzito na kuniambia ni wangu. Nilikuwa nje ya nchi kwa muda mwaka na miezi kadhaa.

Amejifungua mtoto wa kiume na sasa mtoto anamiezi kama mitano hivi, nimerudi na nimemuona mtoto kwa kweli ni copy yangu kabisa (mama wa huyu mdada anajua ukweli wote na aliwahi iona picha yangu akaishia kumcheka mwanawe tu).

Kwa kweli naumia Sana kuona damu yangu ikipotea bure.

Kwa wajuvi wa masuala ya sheria na/au ushauri, nifanye vipi ili nimpate huyu mtoto wangu au ndo imekula kwangu?

Ushauri : Inaumiza Sana, tusiwape mimba wake za watu, watoto wanakosa matunzo yetu halisi.

Wasalam, karibuni kwa mapovu, ukosoaji na ushauri.



Achana na maisha ya watu na mtoto wa watu, Kama mtoto hajui, Baba yake hajui, unachotaka ni nini? Ubinafsi wako uvuruge nyumba ya watu?
 
hizi game zinazopigwa kwa lengo la kuagana huwa ni hatari sana. pole ndugu
 
Aisee!! Dunia ina mengi sana! Hivi mwanamke hadi unatoka kwenda kulala na mwanaume mwingine,kwamba mumeo hakutoshi??! Navaa viatu vya huyo mumewe anavyolea huyo mtoto kwa mapenzi makubwa akijua ni wake huku mkewe akiwa anamnn'gong'a kisogo !
 
Achana na maisha ya watu na mtoto wa watu, Kama mtoto hajui, Baba yake hajui, unachotaka ni nini? Ubinafsi wako uvuruge nyumba ya watu?
Siyo kuvuruga Nyumba ya watu tu, Bali hata Maisha yake yatakiwa hatarini. Huwezi juwa jamaa akibaini huo upuuzi atachukuwa hatua zipi dhidi yake...
 
Siyo kuvuruga Nyumba ya watu tu, Bali hata Maisha yake yatakiwa hatarini. Huwezi juwa jamaa akibaini huo upuuzi atachukuwa hatua zipi dhidi yake...

Una miaka mingapi? haujielewi unachotaka kufanya, labda umchukue mtoto na Mama yake, mtoto tu? huyo mwanamke anaenda kuishi kwa tabu milele!
 
Kwanza tambua kwenye SHERIA kuna principle inayosema "YOU CAN NOT BENEFIT FROM YOUR OWN WRONGS" alafu ujue pia kutokujua sheria sio kinga(defence), kikubwa mume wa huyo mwanamke ndio atakayetoa maamuzi cause tamaduni za kiafrika zipo wazi kuwa Mume anamiliki familia, ila kama lolote litatokea kuhatarisha maisha ya mtoto ama Mama basi utakuwa na haki ya kupewa mtoto wako kwa taratibu za kisheria, ila jaribu kutafakari hii scenario kupata uelewa zaidi...
" Mwizi kaiba Gari aina(Landcruiser V8) Arusha kaja nayo Dsm, baada ya mwezi ikaibiwa akiwa kai paki Mlimani city, Ni halali akitoa taarifa polisi na kuanza kuitafuta hii gari yeye binafsi kama mmiliki halali wa hiyo gari".?

Jibu ni HAPANA. Hutathubutu hata kuripoti polisi hata kama ungemuona akiondoka nayo kwani huwezi jua ka ndo mwenye nalo. Kifupi, Huyu bwana ajinyamazie ila awe akipitia mitaa hiyo mara kwa mara. Ajifanye rafiki wa siku nyingi kwao. Ipo siku, kitanuka tu.
Nimeona wengi wakirudishwa kwao wakiwa weshabalehe. Chochote atakachotoa pale kiwe ni kwa sababu yeye ni rafiki wa hiyo familia.
 
Rafiki yangu, mbona habari zako Mimi ninazo tayari? Wewe Fanya hivi, najua # ya simu yangu unayo, nipiie usiku saa 4 hivi tutengeneze appointment wrote watatu na mtoto wako wa nne ili uje nikukabidhi bidhaa yako bila shida!! Fanya hivyo usiogope.
Alijua haupo JF?
 
Humpati haya kwa dawa elewa ujifa unaenda motoni ILA ya kufa kwako utapata azabu kudogo TENA nakuombea ulaniwe na mungu upewe azabu Kali kama mungu akujalie moto mkali zaidi
 
Back
Top Bottom