Msaada wa kisheria: Nilikuwa nagombana na mtumishi mwenzangu yeye ajahamishwa kituo ila mimi nimepelekwa kijijini

Wamizigo

Member
Sep 8, 2017
52
54
Habari wana jf?,

Mimi ni mtumishi (mshika chaki) kuna mtumishi mwenzangu tumezinguana nae kutokana na tabia zake za ajabu, hasa za kunisema vibaya mbele za wanafunzi, huku yeye akijikweza.

Kutokana na kuzinguana huko, taarifa zilifika kwa afisa elimu, na afisa akadai kuwa tuandike barua za kuomba kubadilishiwa vituo vya kazi kwa kujihamisha wenyewe ili tuwe shule tofauti. Sasa barua zimejibiwa jana, cha ajabu mimi nmehamishiwa shule ya kijijini kabisa halafu mwenzangu kaachwa pale pale kwenye kituo cha awali (hajahamishwa), nmejaribu kumuuliza afisa elimu sababu za kutomhamisha mwenzangu ambaye ndo chanzo cha ugomvi hata walimu wengine wanamjua wanakaa nae mbali, afisa anajibu kuwa sijamhamisha kwa sababu ni mwalimu wa sayansi wewe ni Arts na shule ina uhaba wa walimu wa sayansi.

Baada ya kunijibu hivyo nimeshindwa nifanyaje na nilikopelekwa ni bush kweli,ukiangalia hata makosa sina kabisa, sasa nifanyaje kabla ya siku 7 nilizopewa za kwenda kuripoti hazijaisha?
 
Baada ya kunijibu hivyo nimeshindwa nifanyaje na nilikopelekwa ni bush kweli,ukiangalia hata makosa sina kabisa, sasa nifanyaje kabla ya siku 7 nilizopewa za kwenda kuripoti hazijaisha?
Mkuu hapo itakubidi tu uende. Hakuna sheria inayopinga wewe uhamishwe na mwingine abaki. Hii ni kutokana na uwepo wa mahitaji wa shule husika. Pole usikate tamaa, ndo maisha uliyoyachagua. Ila kama umri wako bado ni mdogo, nakushauri ukapambane na kitabu tena ili ukae town, labda siku moja nawe utakuwa DEO.
 
Asante kwa ushaur wako
 
Suala la msingi lilikuwa mtenganishiwe shule za kufundisha jambo ambalo Afisa Elimu amelifanya,wewe uliomba kuhama mwenzio aliomba kubakia hapo hapo shuleni mlipokuwa mnafundisha wote
 
Suala la msingi lilikuwa mtenganishiwe shule za kufundisha jambo ambalo Afisa Elimu amelifanya,wewe uliomba kuhama mwenzio aliomba kubakia hapo hapo shuleni mlipokuwa mnafundisha wote
Wote tuliomba shule zingine tofauti na pale tulipokwepo ndo tulivyoambiwa
 
Pole sana nenda uongee na afisa elimu umpe kitu flan atakufanyia makeke urudi town ...kijijin mzee baba uko utasanda kama ulizoea bebe za town ..jarb kujiongeza itakuwa jamaa yako katoa ...kitu flan.
 
Kuna walimu hawajitambua kabisa, uwoga wako ndio ulio kupeleka kijijini, kimsingi ulipaswa ukatae kuiandika hiyo barua ya kuomba kuhama kituo afisa elimu asingekuwa na uwezo wa kukuhamisha labda kwa malipo na hela hiyo asingekuwa nayo hivyo ungebaki hapohapo shuleni, siku nyingine muache uoga
 
Back
Top Bottom