Msaada wa kisheria: Naomba ufafanuzi pale inapotokea mtuhumiwa kutofika Mahakamani bila kutoa taarifa kwa Mahakama

Entreprenuare

JF-Expert Member
Aug 24, 2019
1,616
1,714
Wakuu naomba kuuliza,

Hivi inapotokea mtuhumiwa kutofika Mahakamani bila kutoa taarifa kwa Mahakama, siku ambayo mahakama iliamuru mlalamikaji kuja na mashahidi mahakamani.

Je, Mahakama huwa inachukua hatua juu ya mtuhumiwa?

Pia, kwa mimi mlalamikaji, nitapataje haki yangu?
 
Kwanza ana kesi nyingine ya kujibu dhidi ya mahakama, pia kiujumla kama umeshashinda kesi vile.
 
Kwanza ana kesi nyingine ya kujibu dhidi ya mahakama, pia kiujumla kama umeshashinda kesi vile.

Na kwa mfano, angekuwa ametoa taarifa, kisheria haitakiwi kutofika mahakamani zaidi ya siku ngapi? Na ikitokea hivyo inakuaje?
 
kama angetoa taarifa ,hakimu angempangia siku nyingine ya kesi kw ridhaa yake endapo mtuhumiwa ana hoja ya msingi ya kuhairisha kesi,lakini kama hakutoa taarifa na hajaonekana mahakamani ni ni kesi nyingine na kinachofuata ni hukumu tu.
 
Mahakama inatoa samansi kwenda polisi ili jamaa akamatwe.. alafu anafutiwa dhamana....halafu anapewa adhabu maybe miezi sita gerezani huku akiendelea kusikiliza kesi yake ya awali kutokea gerezani...na akiwa gerezani jezi yake inawekwa nembo nyekundu na pia huwa hawatoki kwenda gengeni kufanya kazi za gereza
 
Kama ni mshtaka alipata dharula akashindwa kufika mahakama bila kutoa taarifa Mara moja,je kesi uwa inapelekwa mbele au inafutwa!?
 
Kama ni mshtaka alipata dharula akashindwa kufika mahakama bila kutoa taarifa Mara moja,je kesi uwa inapelekwa mbele au inafutwa!?
Utapewa summons wito wa kuja mahakamani siku nyingine, ukitegea kutofika Mara 3 kesi inafutwa
 
Back
Top Bottom