Msaada wa Kisheria: Naomba kuelimishwa kuhusu umiliki wa tovuti zisizosajiliwa Tanzania

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,877
2,000
Habari wakuu,
Naomba ufafanuzi kuhusu Section 79(c) of the Electronics and Postal Communications Act, No 3 of 2010. Naomba kujuzwa kama ni kosa kisheria kumiliki tovuti(website) ambayo domain yake inaishia na dot com (.com). Nimeuliza hivi kutokana na shauri fulani linaloendelea mahakamni. Mimi nimekuwa nikiwasaidia watu kusajili na kuendesha tovuti kwa domain zisizoishia .tz sasa nimetishwa na habari hii nisije ingia matatizoni au kuwaingiza matatizoni wateja wangu ambao nawatengenea tovuti(websites). Na kama ni halali unafuata taratibu zipi usiwe umevunja sheria? Kama ni kosa mbona zipo tovuti hizo nyingi tu za hapa Tanzania zinaishia .com kama hii www.ippmedia.com? Kipande kifupi kinachozungumzia sheria hiyo hiki hapa chini nimetoa ktk kipande cha Final HANSARD mahali hapa http://www.researchictafrica.net/co...c_and_Postal_Communications_Act_no_3_2010.pdf
Domain-ccTLD.PNG

NOTE: Naomba michango isilenge kuingilia kesi iliyopo mahakamani tusijeongeza matatizo kwa mhanga wa kesi husika.
 

ISO M.CodD

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
4,951
2,000
Kuna nyuzi nyingine kadhaa za nyuma kidogo tuliliongelea hili suala. Sheria kama sikosei inataka every 'public entity' iwe na domain iliyosajiliwa Tanzania. Sasa sijui kama ni kusajili tu ama ni lazima pia entity husika iitumie hiyo domain kama primary domain yake (which is an outrageously stupid idea).

Mwanasheria au mwenye ujuzi wa hii sheria ajibu maswali haya:

Mfano nina entity yangu inaitwa developers.
1. Je, ni lazima nisajili domain iitwayo developers.co.tz?
2. Kama jibu la 1 hapo juu ni ndiyo, je kutokufanya hivyo adhabu yake ni nini?
3. Je, naruhusiwa kisheria kusajili domain ya TLD tofauti na ccTLD ya .tz? Mfano developers.com au developers.org au developers.net
4. Kutegemeana na jibu la 1 na 3 hapo juu, je ni lazima kuitumia domain ya .tz kama primary domain ya public facing website ya entity husika?
5. Kutegemeana na jibu la 1 na 3 hapo juu, ni lazima nitumie .tz kama official website kwenye documents za kisheria na kiserikali?

Wazoefu kama Maxence Melo wanaweza kutusaidia kwa hili, nadhani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom