Msaada wa kisheria namna ya kuwagawia watoto urithi wao nikiwa bado hai!

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
685
484
Nawaomba wanajf mnielimishe namna nzuri na ya kisheria ya kuwarithisha watoto mali zangu! Pia sheria inasemaje juu ya umiliki wa mke hasa kwa Mali alizomkuta Nazo mume wake?
 
Kwa sheria ya dini ya kiislaam...

Mtu harithiwi mpaka afe(awe maiti)

Kabla ya kifo huo ni wosia...

Na wosia hauandikwi juu ya wale wenye haki ya kurithi...

Na wenye haki ya kurithi ni mama, baba, mke, mume watoto, na kaka na dada. ..wa marehemu

Na wosia hautakiwi kuzidi theluthi ya mali nzima ya marehemu...

Na mirathi inahusu mali ya marehemu tu ukiondoa kile alichousia au deni...

Mali ni yako uliyochuma mwenyewe tu...

Hakuna mali ya pamoja kama hamkuchuma pamoja... Iwe kabla ya ndoa au baada ya ndoa. .. Iwe ya mke au mume...

Mali inayogawiwa mirathi iwe ndogo au kubwa. ..

Kisheria ya kiislaam. .. Mirathi imeshagawiwa na allah. .. Hakuna anayeruhusiwa kugawa mirathi tofauti na alivyogawa allah. .. Kinyume chake ni dhambi kubwa kwenda kinyume na sheria ya allah. ..

Ahsante.. .
 
[QUOTE="DsmicSound,
Kwa sheria ya dini ya kiislaam...

Mtu harithiwi mpaka afe(awe maiti)

Kabla ya kifo huo ni wosia..
[/QUOTE]
Nashukuru kwa maelezo hayo!Kimsingi nilitaka nianze kuwagawia Mali zangu watoto wangu hivyo nilitaka mnieleweshe sheria inasemaje?
 
Hakuna urithi mwenye mali akiwa hai.

Unachoweza kufanya ni kuhamisha umiliki toka kwako kwenda kwao , wape kama zawadi. Tafuta wakili atakuandalia nyaraka za kuhamisha umiliki.
Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi
 
Hakuna urithi mwenye mali akiwa hai.

Unachoweza kufanya ni kuhamisha umiliki toka kwako kwenda kwao , wape kama zawadi. Tafuta wakili atakuandalia nyaraka za kuhamisha umiliki.
Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi
 
Back
Top Bottom