deo_gratias
Member
- Jul 31, 2016
- 13
- 1
Habari wana JamiiForum!
Nina huzuni kubwa sana kwani baba yangu mzazi amekamatwa na police wakishirikiana na askari wa TANAPA na kuwekwa ndani zaidi ya wiki sasa bila ya maelezo yoyote yale ya kutosha.
(stori kwa ufupi)
Baba yangu anamiliki silaha aina ya short gun kihalali kabisa. amekuwa akiitumia kwa shughuli za kuamia shamba na wadudu waharibifu.
siku ya tarehe 8 mwezi wa 8, police wa wilaya ya Bagamoyo, wakiambatana na askari wa TANAPA walikuja nyumbani kumfuata baba yangu. kwa bahati siku iyo iyo baba alikua akielekea Bagamoyo wilayani ili kulipia bunduki yake. walipomkosa nyumbani wakaamua kuwasiliana na wenzao waliopo bagamoyo ili kwamba (baba) akifika huko asitoke mpaka watakapofika.
walipofika bagamoyo walimkamata na kumuweka ndani kwa na kutuambia kuwa wanahisi silaha yake ilitumika katika uhalifu. Tangu siku iyo, wamekuwa wakitupa jibu moja tu kwamba "wanafanya uchunguzi"
kinachoniumiza zaidi ni kwamba, kuna tetesi kuwa wanawatesa (torture) ili wakubaliane na zile tuhuma wanazowapa. tumekuwa tukizuiwa hata kumuona tangu siku iyo.
naomba msaada wa kisheria hata kwa mawazo tu jinsi ya kumtoa baba yangu.
kwanza naomba kujuzwa "Ivi kisheria, mtu anaweza kukamatwa bila ya kithibitisho?"
kama ndiyo "Atakaa ndani kwa mda gani kabla ya kufunguliwa kesi?"
"je ni ruhusa kumtesa mtu ili akubali kosa ambalo hajatenda?"