Msaada wa kisheria kuishitaki mifuko ya hifadhi ya jamii mfano nssf,ppf,..nk | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kisheria kuishitaki mifuko ya hifadhi ya jamii mfano nssf,ppf,..nk

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by bakuza, Jul 23, 2012.

 1. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kutokana na mifuko hii kukiuka utaratibu wa mwanzo kati yake na wanachama bila kuwashirikisha wanachama wake ningeomba wajuzi wa sheria na vyama vya kutetea wafanya kazi wajitokeze kusaidia katika hili.Hii ni baada ya taarifa yao ya kusitisha malipo kwa wafanya kazi mpaka baada ya kufikisha miaka 55.
  Soma taarifa husika hapo chini:-

  [h=6]SSRA: Hakuna kujitoa NSSF, PPF

  23rd July 2012

  Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema kuanzia sasa mwanachama wa mfuko wowote hataruhusiwa kuchukua mafao yake kutokana na sababu yoyote mpaka hapo atakapofikisha miaka 55.

  Hata hivyo, licha ya kuzuia fao la kujitoa na kutoruhusiwa kuchukua mafao yao, mwanachama wakiwamo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma NSSF) atapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye sheria ya SSRA.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, mabadiliko hayo yametokana na sheria za mamlaka hiyo kufanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge Aprili 13, mwaka huu na kwamba imeshasainiwa na Rais Jakaya Kikwete na imeanza kutumika rasmi.

  Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo.
  “Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi lakini kuanzia sasa mwanachama wa mfuko atapata mafao yake pale atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiari (55) au kwa lazima (60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu” ilisema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kufafanua kuwa:

  “Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni.

  Taarifa ya Mkurugenzi huyo iliendelea kusema kuwa mafao ya kujitoa yanapunguza na kuondoa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

  Hata hivyo, ilisema pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya madini yataendelea kutolewa kama kawaida ikiwemo kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.

  Ilisema wanachama wanatakiwa kuwa watulivu kuhusiana na mabadiliko hayo na kwamba maslahi yao yatalindwa na hakuna atakayepunjwa kutokana na utaratibu huo.

  SOURCE: Nipashe[/h]
   
 2. m

  mob JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  hii naipinga kwa nguvu zangu zote na ikibidi nitaandamana kudai haki yangu. ninazungumza hivi nikiwa na maana kuwa ikiwa nina hela yangu na iko ppf/nssf na ninaumwa sana na hali inazidi na uwezo wa kufanya kazi tena sina inamaana nife bila ya kuzitumia hela zangu .sikubali narudia tena sikubali
   
 3. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  kuna ulazima wa kufanya maamuzi magumu...hili jambo halivumiliki hata kidogo...:nono:
   
 4. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ishitaki SSRA na siyo hiyo mifuko. Mifuko inapokea tu order kutoka kwa Regulator.
   
 5. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hilo nalo neno Rejeo
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Nadhani wafanyakazi tunazo njia mbili kuu za kukataa huu uhuni wa serekali.

  [1] Kuishitaki SSRA , NSSF na PPF

  [2] Kuandaa maandamano na migomo nchi nzima kushinikiza serekali ifute sheria hii kandamizi.

  [3] Sheria hii haipaswi kuwaingiza wafanyakazi wa zamani iwahusu wafanyakazi wapya tu ambao wameingia makazini wakati wa sheria inaanza kufanyakazi.
   
 7. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe NGONGO huu ni uonevu wa hali ya juu kabisa Hivi itakuwaje kwa wale waliokatika sekta binafsi ambao uhakika wa kufanya kai miaka hiyo ni mdogo sana wamefanya sana kazi miaka 10-15 Wakaingia kujiajiri hapo awachangii tena katika mfuko huo inakuwaje hapa. Kaacha kazi akiwa na miaka 30 sasa inabidi asubiri mika 25 bila kuchangia ndipo aende kuchukua mafao yake hii aiingii akilini hata kidogo
  Wanachama wote tuitishe mgomo sasa wa nchi nzima kupinga hili kama walitumia fedha zetu warudishe hili alikubaliki hata kidogo. Kwani tumesikia kuwa wamechukua fedha zetu wakalipa mishahara ya wafanya kazi hii ilikuwaje na CAG alisha sema mifuko hii inakoelekea ni kufilisika sasa ndio wanaingiza hili michango yetu hii si inakuwa kama DESI sasa
   
 8. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  I think the locus standi is solid for those who joined these social security funds before the enactment of this repugnant law. My opinion is that the law should not affect members retrospectively as this will be against the rule of law. In the name of the rule of law, the law should bind the new members who will join the funds in knowledge of the effects and sours of this unprecedented, intimidating, repugnant and inhumane law.
   
 9. m

  mhandisi_1 Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 15
  Hawa watu watunga sheria wote ni wafanyakazi wa serikali ndio maana hawajui kwa nini watu wanaacha kazi. mazingira ya kazi kwenye sekta binafsi sio ya kumfanya mtu afanye kazi mpaka miaka 55. Mathalani nenda migodini utafanya kule mpaka ufikishe miaka 55! si utakufa kabla ya wakati huo? Jambo jingine kwa sekta binafsi suala la umri wa kustaafu ni irrelevant - mtu unaweza kufanya kazi hata miaka 80 kama una nguvu wao umri sio shida wao ni kazi tu. Sheria hii inaweza kuwa relevant kwa wafanyakazi wa serikali na mashika yake labda.

  Suluhisho la tatizo hili ni kwa wafanyakazi wanaoathirika kupiga kelele na kuchukua hatua zote wanazoweza kuhakikisha sheria hii inarekebishwa ili kuzingatia mazingira tofauti kabisa katika sekta mbalimbali za kazi TZ, wakubwa mjue sio watu wote wanafanya kazi kwenye mazingira kama unayofanyia wewe mkurugenzi unayetaka eti kutuelimisha. We dont need that sensitization we are struggling to survive!
   
 10. Ndukidi

  Ndukidi JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 821
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Nakubaliana na wewe kwa 1 and 2. hii 3 hapana, haitakiwi kubagua, ni sheria kandamizi basi.. haijalishi umeanza jana, leo au kesho. ifutwe , na hii mifuko ianze kutoa mikopo kwa kutumia hiyo michango yetu kama collateral mbona wanatoa kwa seriali na watu binafsi kama akina Mzindakaya, Sumayi? Inashindikana nini kwa mchangiaji mfanyakazi ambaye tayari ana hela kwenye mfuko husika?
   
 11. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha kuona kuwa serikali inakubali kwa roho kwatu kuhujumu wafanyakazi wake, ambao ndiyo ni chanzo kikubwa cha kodi itokanayo na PAYE. Kwanza serikali inafahamu kuwa wastani wa kuishi kwa watanzania kwa mujibu wa utafiti wa mwaka jana ni miaka 48, kuweka upeo wa umri wa miaka 55 ni mbinu chafu ya kupora kinyemela makato ya wafanyakazi waliyoyatolea jasho jingi na kwa miaka mingi kwani wengi wa wafanyakazi hao watakuwa wamefariki dunia, chanzo kikubwa ni kushindwa kukabiliana na ugumu wa maisha baada ya kuacha kazi kabla ya kutimiza miaka 55. Pili mafao watakayoyapata wachache watakaobahatika kufikia umri wa kustaafu yatakuwa kiduchu na yasiyo na thamani kutokana na mfumuko wa bei, na asilimia ndogo ya faida (asilimia moja) licha ya kuwa michango hiyo imeiwezesha mifuko ya hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye miradi mikubwa yenye tija. Mifuko ya hifadhi ya jamii hapa nchini kwa mfumo wa sasa unawanufaisha wafanyakazi wa hifadhi hizo, hususan wakurugenzi kwani package zao za kustaafu na marupurupu na mishahara wanayolipana ni kufuru. Tusikubali.
   
 12. M

  Mshind Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakika nch yetu ina mkosi mkubwa kama si laana kwa kukiuka maadili na wosia wa baba wa taifa mwl nyerere. tazama viongozi wote walio fuata baada ya mwl. wote tia maji tia maji, hakuna mwenye fikra thabiti ya kukwamua Tanzania na watu wake kutoka ktk uchumi duni na matatizo mengine ya kijamii, tazama maamuzi yanayotolewa yote sasa uozo mtup, watanzania huta msaada wala mtu wa kutusaidia au wakujivunia. nazani sasa watanzania tukubali kufa kwa faida ya vizazi vijavyo. No success without sacrifice ktk hili la pension watanzania tupigane kiume kungo'a fikra mbovu tena zisizo natija hata kidogo, we have fixed account from various banks we can keep our money for future!
   
 13. b

  bullof New Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na uamuzi wa kulifikisha hili suala mahakama kuu kuipinga sheria hii ni mbovu inayo pora haki zetu mchana kweupe. Inafanya maisha bora kwa kila mtanzania kuwa ndoto. Tuna mkumbuka Nyerere:A S cry::A S cry:
   
Loading...