Msaada wa kisheria kuhusu suala lililopo CMA

maruudaniel

JF-Expert Member
Dec 19, 2020
888
1,067
Suala langu lipo CMA na mwisho wa mashauri yapo mwishoni mwa mwezi huu. Kwani nilichelewa kufungua madai kwa sababu nilipata ajaili iliyopelekea kuchelewa kufungua madai.

Na katika kufungua madai niliwasilisha Documenti za matibabu na Ed sheet ambazo zilikubalika kwa ajili ya mashauri ila mwezi uliopita nilikuja kugundua PF3 kutoka Polisi ilikuwa inahitajika kwani mwanasheria wa hiyo Kampuni niliyokuwa nafanyakazi ndo anahitaji kwani anasema sikupata ajali kwa hiyo aoni sababu iliyosababisha kuchelewa kufungua madai.

Kwa ujumla PF3 pamoja na PF-90 zote ninazo na nilivyomwambia Mwanasheria wangu kwa nini hakuniambia juu ya huitaji wa hivi vitu aliniambia vile alivyovipeleka mwanzo ni sawa kwani kwa sasa harusiwi kufaili documenti mpya kama hizi PF-3 na PF-90 .

Je, ni fanyeje kuhusu hili swala kwani ninahisi sitatendewa haki.

Pia naomba yeyote mwenye namba ya simu ya Mkurugenzi wa CMA aniwekee hapa.

Asanteni sana
 
Ila wana sheria sometimes dah! Yaani yuko tayari kutetea ili haki ya MTU ipotee!
 
Wanasheria wengi siku hizi ni viraza tu wanajifanya wajuaji lkn hamna kitu ni ubishi tu umewajaa, wengi wefaulu kwa madesa halafu wamajifanya kufungua law firms lkn kumbe ni watupu

Unakuta mteja anamshauri Wakili wake kwamba waweke documents fulani ambayo anaamini itamsaidia katika kesi yake lkn wakili anajifanya mjuaji Na kumwambia sio muhimu zilizopo zinatosha kumbe ni uvivu tu wakuandika...

Lkn cha ajabu ruling au uamuzi ukitoka utaambiwa kwamba nyaraka Fulani hukuambatanisha ambayo kimsingi ndiyo ileile ambayo wakili kilaza aliikataa.

Kama kazi ya uwakili hamuiwezi nendeni shamba mkalime kuliko kujifanya mnafungua law firms wakati kichwani mpo empty.
 
Back
Top Bottom