Msaada wa kisheria kuhusu kuvunja mahusiano

Wadau nawashukuruni sana nisingependa kwenda kwa dawati la ustawi wa jamii kwa sbabu huko watatutaka tugawane mali pasu kwa pasu yaani sawa.kitu ambacho itaniathiri tena sana kwani nina mali kama nyumba ,viwanja na gari.kwahiyo ndo maana nimeona nimpatie hicho kiasi.kuhusu kuachana kwa kweli ndoa na hyu mdada ni shida sitoweza vumilia hata kidogo hatuendani kweli kukaa nae ni kama bahati mbaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wadau mnajua sidhani kuna mtu kwenye mahusiana anapenda kuachana na mwenzake laki mpaka ifikie haya maamuzi unakuta mmefikia point of no tolerance.mtoto wangu nitamtunza mpaka atakapotimiza umri wa kwenda shule ntamchukua niishi nae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mwanaume kuna mwanamke nimezaa nae na tumeishi nae kwa muda wa mwaka mmoja kwa bahati nzuri amebahatika kupata mtoto nikiwa nae na hatukuwahi kufunga ndoa rasmi.

Sasa tumeshindwana nae kuishi kama mke na mume na tumefikia uamuzi wa kuachana sasa ili kuachana ameomba nimpatie kiasi cha pesa na kiwanja kimoja nimpatie mtoto wetu yaani nibadilishe hati isome majina ya mtoto wetu.
.
Ndugu, Kisheria huwezi kuachana ma mke ambaye hakuwa mke wako, yaani mwanamke ambaye hamkufunga nae ndoa. Hata kama mmebarikiwa na mtoto mmoja bado huyo si mkeo na huwezi kuachana nae kwa taratibu za mme na mke wanapoachana. Kwa maana nyingine hiyo pesa na kiwanja unavyotaka kutoa sio stahili yake hata kidogo. Wajibu wako ni kutoa pesa kwa ajili ya malezi/matunzo ya mtoto mliezaa pamoja, na sio kutoa mali yeyote.
Nakushauri usitoe kiwanja wala hiyo milioni 10, cha msingi gharamika hiyo laki tatu kila mwezi kwa ajili ya malezi ya mtoto. Vinginevyo labda kama unataka kutoa sadaka tu. Maana hata mahakamani huyo mzazi mwenzio akikupeleka hatakuwa na kesi ya msingi zaidi ya kuomba mahitaji muhimu ya mtoto ambaye hata shule hajafikiriwa kuanza.
 
Nashukuru sana bwana Dragon kwa ushauri wako.ila huwa nasikiabkisheria wanasema kuwa kama mtu mmeishi nae kwa miezi sita na matendo yenu ilikuwa inaonesha kama nyie ni wanandoa.huyo kisheria ni kama mke wako na anakuwa na haki zote pndi ikitokea mmeachana mtagawana mali zote kumbe sio kweli?

Mkuu, sheria inasema miaka miwili na sio miezi sita. Ikitokea miaka miwili au zaidi mmeisha kama mme na mke basi kila mmoja wenu atakuwa na haki yake kama mwanandoa pindi mtakapoachana, lakini hii inatokea tu pale hakuna upande (kati ya mke au mme) ambao umekana kuwepo kwa mahusiano ya kindoa.
 
Wadau nawashukuruni sana nisingependa kwenda kwa dawati la ustawi wa jamii kwa sbabu huko watatutaka tugawane mali pasu kwa pasu yaani sawa.kitu ambacho itaniathiri tena sana kwani nina mali kama nyumba ,viwanja na gari.kwahiyo ndo maana nimeona nimpatie hicho kiasi.kuhusu kuachana kwa kweli ndoa na hyu mdada ni shida sitoweza vumilia hata kidogo hatuendani kweli kukaa nae ni kama bahati mbaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwan ni mkeo mpaka hzo Mali mgawane?!!..

Kumzalisha hakumpi yeye fursa ya kutaka mahela yote hayo,!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mwanaume kuna mwanamke nimezaa nae na tumeishi nae kwa muda wa mwaka mmoja kwa bahati nzuri amebahatika kupata mtoto nikiwa nae na hatukuwahi kufunga ndoa rasmi.

Sasa tumeshindwana nae kuishi kama mke na mume na tumefikia uamuzi wa kuachana sasa ili kuachana ameomba nimpatie kiasi cha pesa na kiwanja kimoja nimpatie mtoto wetu yaani nibadilishe hati isome majina ya mtoto wetu.

Vile vile yeye anataka nimpatie mtaji wa shilingi milioni 10 ili akafanye shughuli zake pamoja na hayo mtoto nitakuwa namuhudumia kwa kiasi cha shilingi 300,000 kila mwezi. Sasa ombi langu liko juu ya hizi pesa milioni kumi10 nataka tuandikishane ili huko mbeleni kama atazitumia vibaya asije kurudi kwangu kwani natafuta mwanamke mwingine nioe sasa nilitaka tuandikishane kwa mwanasheria ili asije huko mbeleni akasema vinginevyo.

Naombeni ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
Utoe milion kumi?unapigwa pesa wewe..muache aende mahakamani.hvi milion 10 ni ya kumpa tu mtu hivi hivi?mwambie ache mtoto kwako na asepe

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Jamani wana jf wenye uzoefu mnisaidie,mzazi mwenzangu kaniganda japo nimemwambia simpendi naomba tuachane kwa amani alinipa masharti yote nimetekeleza lkn karudi kwangu.nilimpatia pesa kiasi cha shilingi milioni 10 pamoja na kiwanja tukakubaliana kila mwezi ntakuwa nampatia laki tatu ya matumizi ya mtoto lkni hata hataki kuondoka,aliondoka amekaa wiki moja karudi kwangu.nifanyaje ili aende zake moja kwa moja.msaada niko na stress sana ya huyu mwanamke.

Mwambie 😍 💕 ❤ ❤ ❤ ❤ ❤ ❤
 
Ulikosea kumpa hizo Mali, ungefuata ushauri wa Dragoon pale juu.

Ondoka wewe nyumbani
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom