Msaada wa kisheria kuhusu kuvunja mahusiano

OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,498
605
Mimi ni mwanaume kuna mwanamke nimezaa nae na tumeishi nae kwa muda wa mwaka mmoja kwa bahati nzuri amebahatika kupata mtoto nikiwa nae na hatukuwahi kufunga ndoa rasmi.

Sasa tumeshindwana nae kuishi kama mke na mume na tumefikia uamuzi wa kuachana sasa ili kuachana ameomba nimpatie kiasi cha pesa na kiwanja kimoja nimpatie mtoto wetu yaani nibadilishe hati isome majina ya mtoto wetu.

Vile vile yeye anataka nimpatie mtaji wa shilingi milioni 10 ili akafanye shughuli zake pamoja na hayo mtoto nitakuwa namuhudumia kwa kiasi cha shilingi 300,000 kila mwezi. Sasa ombi langu liko juu ya hizi pesa milioni kumi10 nataka tuandikishane ili huko mbeleni kama atazitumia vibaya asije kurudi kwangu kwani natafuta mwanamke mwingine nioe sasa nilitaka tuandikishane kwa mwanasheria ili asije huko mbeleni akasema vinginevyo.

Naombeni ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeridhia kabisa ama unahisi unashurutishwa???!! Aliyepelekea kuvunja mahusiano yenu ni mke ama wewe binafsi? Usalama wa mtoto na malezi yake huko atapokuwa umeridhika?!! Kwa nini msitumie jitihada za kuyamaliza na kufunga ndoa baadala ya kutumia wanasheria na nguvu kutengana kwa fidia ya almost 20mln +??!!

Najaribu kuwaza huyo mpya nae akija kufuata nyayo za baby mama sijui uamlaumu!!1
 
Kama mdau alivyosema kwa hiyo Umeridhia Mtoto awe mbali na wewe kisa wewe na yeye mumeshindwana? Huoni utakuwa unajiwekea precedence hata kwa huyo unayetaka kumuoa kuwa wewe mkivurugana unamlipa anasepa na kuandikishiana kwa Mwanasheria? Sijui lakini mimi bado mchanga kwenye haya mambo ila ningeuwa mimi ningetathimini kwanza madhara ya mtoto pia na kuangalia sababu iliyopelekea kuchokana na je kumpa mtaji kama ndiyo suluhisho la kudumu au la muda mrepi?
 
Nendeni bomani na kwenye dawati la ustawi wa jamii..wataachanisha kwa usawa kabisa..

Nawapongeza kwa kuachana,mana mmegundua kua hamuendani.
 
Mpe tu

Malezi yalivyo magumu

Hakikisha kiwanja unabadili jina lisome la mwanao...... (hakuna ubaya hapo)

Ila.ngoja wanasheria waje(wa jf hapa walivyo wachoyo wa kushauri....)
Mimi ni mwanaume kuna mwanamke nimezaa nae na tumeishi nae kwa muda wa mwaka mmoja kwa bahati nzuri amebahatika kupata mtoto nikiwa nae na hatukuwahi kufunga ndoa rasmi.sasa tumeshindwana nae kuishi kama mke na mume na tumefikia uamuzi wa kuachana sasa ili kuachana ameomba nimpatie kiasi cha pesa na kiwanja kimoja nimpatie mtoto wetu yaani nibadilishe hati isome majina ya mtoto wetu,vile vile yeye anataka nimpatie mtaji wa shilingi milioni 10 ili akafanye shughuli zake pamoja na hayo mtoto nitakuwa namuhudumia kwa kiasi cha shilingi 300,000 kila mwezi.sasa ombi langu liko juu ya hizi pesa milioni kumi10 nataka tuandikishane ili huko mbeleni kama atazitumia vibaya asije kurudi kwangu.kwani natafuta mwanamke mwingine nioe.sasa nilitaka tuandikishane kwa mwanasheria ili asije huko mbeleni akasema vinginevyo.naombeni ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasheria watakuelekeza hapa pia unaweza kwenda kwenye ofisi ya mwanasheria kupata mwongozo Zaidi.
 
tulia nae tu mfanye maisha....utengano sio mzuri mnamkosesha mtoto uwepo wenu na mapenz yenu...amna kitu kinachonisikitisha kama kuona mtoto analelewa na mzazi m1
 
akija kutaka sababu ya kuachana utashangaa ilivyo ya kijinga..ila nenda ustawi jamiii wakupe muongozo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom