Msaada wa kisheria kuhusu kufukuzwa kwenye nyumba ya serikali

Adm

Senior Member
Sep 19, 2010
149
45
Habari wanasheria wa jf,naombeni msaada kwenye hili langu jambo. Mimi ni mtumishi wa serikali(mwalimu) kwa sasa sipo kituoni niko chuoni. Niliporipoti kwenye kituo cha kazi uongozi wa kijiji pamoja na kata ulinipatia nyumba ya kuishi nyumba ambayo hapo awali kabla ya shule kujengwa ilikuwa ikitumika kama nyumba ya bwana shamba. Nimekaa kwenye nyumba hiyo kwa miaka 5,hivi majuzi bwana shamba kaletwa huko kijijini. Sasa uongozi wa kijiji umekuja bila hata taarifa rasmi ya kimaandishi ukinitaka nitoke kwenye nyumba hiyo bila hata kunipatia nyumba nyingine. Ndugu zangu mnaofahamu sheria za makazi hasa kwenye nyumba za serikali sheria inasemaje juu ya hilo jambo? Naombeni msaada
 
Wewe ndiyo ulikuwa unakaa kwenye nyumba hiyo kimakosa, hebu naomba za uongozi wa kijiji niwashauri kisheria wakufanye nini ili iwe mfano kwa watu wanaopindisha taratibu.
 
Back
Top Bottom