Msaada wa kisheria kuhusu kuachishwa kazi

Heater

Member
May 28, 2019
88
150
Kuna Boss mmoja aliniita ofisini kwake kwamba kuna kazi anakwenda kunipatia.

Baada ya Usaili akanambia nianze na Probation wiki mbili, kisha atanipa mkataba lkn katika izo wiki mbili atakuw akinilipa kila wiki, na ni kweli alifanya hivyo.

Sasa katika izo wiki mbili nilikua chini ya muajiriwa wake, tulifanya kazi vizuri, zilipoisha wiki mbili akaniambia sifai ivo hatoweza kuendelea na mimi, na hatukuwa na mkataba wowote wa kimaandishi.

Naombeni ushauri wenu kisheria, hii iko sawa?

Je, ni sahihi kufanya kazi kipindi cha Probation pasipo mkataba wowote?

Je, muda wa probation upo kisheria ama ni muajiri anaamua iwe muda gani?

Je, kuna sehemu yeyote nimedhulumiwa haki yangu ama kila kitu kimekwenda fear?
 
Heater

Member
May 28, 2019
88
150
Acha hizo TWO WEEKS unataka kuanza kusumbuana na watu? Wakati mwingine hali kama hiyo ipokee huenda kuna kazi alikuwa anaitegemea ili aweze kukuajiri bahati mbaya imekataa. Huenda kwa kuwa ana mawasiliano yake akakuhitaji baadaye
Sio kusumbuana ni kuelimishana tu, kwamba sheria inasemaje, maana wengine hatuna uelewa wa maswala hayo, kujua stahili yako n nzuri sana ktk maisha
 
Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
15,492
2,000
Acha hizo TWO WEEKS unataka kuanza kusumbuana na watu? Wakati mwingine hali kama hiyo ipokee huenda kuna kazi alikuwa anaitegemea ili aweze kukuajiri bahati mbaya imekataa. Huenda kwa kuwa ana mawasiliano yake akakuhitaji baadaye

Huyu jamaa anaonesha ni mtata, na inawezekana hata kazi ametemeshwa kwa sababu hiyo.

Kaambiwa atafanyiwa probation ya 2 weeks, akionekana anafaa atapewa kazi. 2 weeks zimeisha na imeonekana hafai, anataka mkataba wa 2 weeks ambazo ameshalipwa.
 
GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
4,943
2,000
Hizi sio ngonjera za kupiga blah blah mitandaoni.

Onana na wakili ashughulike na tatizo lako on practical basis!

Kwenye mambo ya sampuli hii hauhitaji ushauri nasaha na tenzi za faraja. Hapa unahitaji kazi na kushughulikiwa tatizo PRACTICALLY.
 
Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
15,492
2,000
Hizi sio ngonjera za kupiga blah blah mitandaoni.

Onana na wakili ashughulike na tatizo lako on practical basis!

Kwenye mambo ya sampuli hii hauhitaji ushauri nasaha, unahitaji kazi na kushughulikiwa tatizo PRACTICALLY.

Mkuu umesoma vizuri thread yake?

Huhitaji mwanasheria hapo, ni straight kwamba hakuwa mfanyakazi, alikuwa kwenye interview bado.

Sasa inakuwa ni kama kumshataki mtu kwa kukunyima kazi.
 
GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
4,943
2,000
Huhitaji mwanasheria hapo, ni straight kwamba hakuwa mfanyakazi, alikuwa kwenye interview bado.
HAPANA. Probation na terms zake zinapaswa kuwa kwenye MKATABA RASMI wa kazi.

Na kuna muda maalumu wa probation na masharti yake!

Ndio maana nikasema hapa panahitaji maelezo ya kina!

Muda wa probation, barua ya uthibitisho, notisi ya kumuondoa kwenye probation nk.

Probation haifanyiki tu kiholela unaitwa na kupewa kienyeji enyeji. Hii haiko sawa.

Huyu aonane na wakili.
 
rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
13,537
2,000
Yani alivyofanya ni kama alifanya dili la muda tu then dili limeishaa ametemwaa...
HAPANA. Probation na terms zake inapaswa kuwa kwenye mkataba wa kazi...

Probation haifanyiki tu kiholela unaitwa na kupewa kienyeji enyeji. Hii haiko sawa.

Huyu aonane na wakili.
 
GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
4,943
2,000
Aeleze ni kazi gani hiyo ya probation ya wiki mbili? Kuna implications katika muda wa probation as far as locus standi to get reliefs is concerned.

Otherwise naona hii kazi ina magumashi mengi! Na huyo mauajiri ana tatizo kubwa probably UKWEPAJI KODI.
 
adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
5,156
2,000
bora wewe kuliko sisi tuliopewa mshahara wa mwisho mwezi wa 3 na kupewa likizo bila malipo kwa muda usiojulikana!!.na tuna mikataba yetu ambayo iko valid.sijui tunabaki kundi lipi??
 
Heater

Member
May 28, 2019
88
150
n
Huyu jamaa anaonesha ni mtata, na inawezekana hata kazi ametemeshwa kwa sababu hiyo.

Kaambiwa atafanyiwa probation ya 2 weeks, akionekana anafaa atapewa kazi. 2 weeks zimeisha na imeonekana hafai, anataka mkataba wa 2 weeks ambazo ameshalipwa.
nimekuelewa vizuri sana, isipokuwa ungejielekeza kwenye thread ingependeza zaidi kuliko kunishambulia na kunizoom nikoje ndani yangu, Lengo ni kuelewa tu sababu nilipata chance mbili, moja mkoani ingine mjini, nikaona nibaki mjini ambako tayari nina uzoefu napo, inapotokea swala kama ili ni lazma uloose mentally, ukiangalia option ya pili nayo ishapotea, sababu kuu pia naelewa Wachina hufanyaga mengi pasipo uelewa wa kisheria au tu huwa hawataki kuzingatia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom