Msaada wa kisheria kuhusu kuachana na mwanamke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kisheria kuhusu kuachana na mwanamke

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mwanaweja, Aug 22, 2011.

 1. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndugu wanajamii forum naomba mnisaidie katika hili swala. mimi ninamwanake amabaye nimeishi naye muda wa miaka 6 tukabalikiwa kupata mtoto mmoja ana miaka 5. kweli tuliishi kwa shida sana maana nilimuoa nikiwa nasoma lakini Mungu akatubarikia mpaka mwaka jana mwezi September niliondoka kuja kimasomo shahada ya pili kabla sijaja huku nilikuwa nimeajiriwa wizara ya maji na umwangiliaji kipindi kile lakini kutokana nakuwa ninafamilia niliondoka nikaenda NMB mshahara wangu unakopitia nikaweza kupata form ya kujaza na kwenda mahakamani kuapa ili mshahara wangu mke wangu awe anachukua kama kawaida kwa kutumia account yangu. tangu kipindi hicho kulikuwa hakuna tatizo lakini karibuni nilianza kupata tuhuma mke wangu anamadeni mengi sana nikajaribu kumuuliza kilichofuata hapo ni matusi na kejeli za kila aina ndipo nilipo amua kuacha yote ili niendelee na masomo mpaka December au January mwaka kesho nitakapo kuja likizo nilikuwa nataka niachane naye maana siwezi ishi na mwanamke anayetukana wazazi wangu na hata mimi.
  Vitu tulivyo navyo ni kiwanja na tumejenga kijumba cha vyumba viwili na sebule. Naomba ushauri wenu wakisheria maana amekuwa akiandika hata sms za kutaka kumuua mtoto hata wakati mwingine kupiga simu nakuongea haya maneno ndio maana nimekaa kimya siwezi hata kuwasiliana naye na sms hizo ninazo hapa. Je, ustawi wa jamii watakubaliana na mimi kuchukua mtoto akakae hata na mama yangu? Maana kunauwezekanao akamuua mtoto wakati wowote maana mimi bado nasoma naniko mbali sana.
  Natanguliza shukurani zangu na MUngu awabariki sana
   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,446
  Likes Received: 7,185
  Trophy Points: 280
  Du pole sana.Wanawake tunalilia sana haki zetu.what abt those who misuse them,is there any adhabu 4 them?
   
 3. A

  Aine JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aise, pole sana ndg yangu kwa hilo, wanawake bwana!

  Je, mlifunga ndoa gani?
  Nenda Mahakamani ili kuvunja ndoa hiyo haraka na hizo msg usizifute ndio utakuwa ushahidi wako ukiwa mahakamani.

  Kuhusu mtoto, kisheria mtoto aliye chini ya miaka 7 anatakiwa kuwa chini ya mama yake ingawa mtoto kama anaweza kujieleza vizuri anaweza kutoa msimamo wake mahakamani kwamba ataishi na nani kati ya baba na mama. Lakini pia mahakama inatumia kigezo cha hali ya uchumi kati ya baba na mama ili kuamua ni mzazi yupi amtunze mtoto huyo.

  Kwa kesi yako, kwa vile mama anamtishia kumuua mtoto hizo meseji usizifute kwani zitakusaidia pia wewe mahakamani kama ushahidi wako kwamba huyu mama hawezi kumtunza mtoto kwani anatishia kumuua. Aidha, kutishia kuua ni kosa la jinai
   
 4. T

  Tall JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.Ni kazi kubwa mwanamke amuue mwanawe.UWE NA AMANI.
  2.Wewe nawe ulimweleza nini hadi akutukane??? au nawe ulianza kumnyanyasa kwa vile anachukua mshahara wote??
  3.Hata hivyo sioni sababu ya msingi ya kumuacha mkeo. VUMILIA akili yako yote iweke kwenye masomo,IWAPO ukirudi masomoni
  ukakuta ana mimba au ana mtoto mwingine hapo waweza kudai TALAKA.
  Nahisi kama kuna jamaa anakuchakachulia mkeo vileeeeeee???? LAKINI USIJALI MAISHA NDIVYO YALIVYO.
   
 5. m

  mbosia Senior Member

  #5
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  pole sana je mtoto ana umri gani ?
   
 6. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  sija mnyanya ila nilikuwa namuuliza tu kuhusu deni alilokopa kwa jamaa yangu 100000 kurudisha baada ya mwezi 1 tsh 150000 na huku anapata mshahara lakini kilichofuata hapo ni matusi na kusema kwa kuwa waliomkopesha hatawalipa maana hawana ustaarabu baada yakunieleza mimi lakini nikajitahidi nikamtumia hela ili alipe hilo deni akapeleka kwao hiyo hela kwa kisingizio kuna mgonjwa nitamsaidiaje hapo?
   
 7. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  nashukru sana mkuu tuko pamoja lakini mimi sio muda mrefu nitarejea kwenye likizo kwa hiyo mimi nataka nimpatie talaka ili kama kuna mtu anamdaganya wakagange maisha yao
   
 8. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  jibu maswali yafuatayo↲
  Je mna ndoa ya msikit au kansani?↲
  Kama mna ndoa ni ngumu sana kumwacha ila unatakiwa uoneshe mahakama your marrage is not reparable ↲
  Ka hukufunga ndo S.66 of Marrage Act ni presumption umemuoa so mtagawana mali kuhusu mtoto Child Act inatoa ka yupo below 7 yrz ataenda kwa mama bt unaweza shawish mahakama ikupe ni pm tuonge kirefu
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Facts ulizotoa ni limited sana kuweza kupata ushauri wa kisheria. Hatujui hata ni ndoa ya aina gani. Whatever the case, unless mkubaliane ku divorece, itakubidi uwe na ushahidi kuwa ndoa imevunjika beyond repair. Itakubidi uonyeshe kuwa kati ya sababu zifuatazo zimefanya ndo yako ivunjike.

  (a) adultery committed your wife, particularly when more than one act of adultery has been committed or when adulterous
  association is continued despite protest;
  (b) sexual perversion on the part of your wife;
  (c) cruelty, whether mental or physical, inflicted by your wife on you or on the children, if any, of the marriage;
  (d) wilful neglect on the part of your wife;
  (e) desertion of you by your wife for at least three years, where the court is satisfied that it is wilful;
  (f) voluntary separation or separation by decree of the court, where it has continued for at least three years;
  (g) imprisonment of your wife for life or for a term of not less than five years, regard being had both to the length of the sentence and to the nature of the offence for which it was imposed;
  (h) mental illness of your, where at least two doctors, one of whom is qualified or experienced in psychiatry, have certified that they entertain no hope of cure or recovery;
  (i) change of religion by your wife, where both parties followed the same faith at the time of the marriage and where according to the laws of that, faith a change of religion dissolves or is a ground for the dissolution of marriage.

  Kama ndoa ni ya Kiislamu itabidi upate certificate toka kwa bodi husika kuwa wamejaribu kuwasuluhisha lakini iimeshindikana. Mie nafikiri hakuna haja ya kukimbilia divorce. B'se inaonyesha kabla ya kwenda masomoni mlikuwa mnaishi vizuri tuu. You need to find out yourself what exactly happened. Mambo ya divorce yatawacost sana si nyie tuu bali pia mtoto. Hapa zinahitajika busara na hekima za hali ya juu. Weka emotions pembeni. Kufanya maamuzi magumu kama haya kwa kutumia emotions ni mbaya sana.

  Pia kumbuka wakati ukiwa huko masomoni mke wako kama mwanamke mwingine anakuhitaji wewe kama mume zaidi ya pesa zako za mshahara. Ushauri wangu ukirudi likizo, usimkurupushe. Kaa nae chini mzungumze kama mume na mke. Don't rush to divorce. Tofautisha kati ya irretrievable breakdown and a temporary rift. Kama anakutumia messages za kukutukana, wala usimjibu kwa kumtukuna. Wasiliana nae kama mke wako.

  Pia mkuu jiangalie wewe mwenyewe unaweza ukawa ni cause ya breakdown. Lugha yako kidogo inanitia wasiwasi. Unasema una mwanamke ambaye umeishi naye muda wa miaka 6 wakati huyo ni mke wako wa ndoa. Sijui kama unam-underrate kwa sababu ya yaliotokea au ndio huwa unamwita hivyo?
   
 10. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kaka EMT Nimekupata sana kweli sio hata mimi ninasema tuachane maana najitahidi sana kuwa nayekaribu hasa ukizingatia January mwaka huu mama yetu(i mean mama mkwe) alitangulia mbele ya haki kweli lilikuwa nipigo kubwa kwake na hata kwa familia nzima yetu ukizingatia nilikuwa mbali ndio maana ninajitahidi sana kutoa ushauri na Lugha za kumfariji kila wakati. Tatizo nipale unapokuwa mumeongea vizuri kabisa bila hata kukwaruzana lakini baada ya muda may be 6hr. unapokea sms inanitukana tena matusi yanguoni akiakaa muda may hata siku 1 au 2 anaomba msamaha. Ukimwuliza kwa nini uliandika sms anakujibu ni hasira, ukimuuliza hasira zinatoka wapi kama wakati tunaongea hatukugomabana anasema alipata hasira tu. Kwa mfano juzi amenitukana wee kwenye sms jana usiku akaandika sms yakuomba msamaha sasa tutaishi maisha ya aina gani? kuna mambo ambayo nahisi kuwa pengine anakunywa pombe au kama hanywi basi anaweza kuwa na matatizo ya akili kwa sasa au kunajambo alilofanya mbaya linamchanganya kwennye akili hasa niliposema naenda likizo.
  "Unasema una mwanamke ambaye umeishi naye muda wa miaka 6 wakati huyo ni mke wako wa ndoa" kwa hili nimekoseha mkuu haikuwa intention yangu
   
 11. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hatuna ndoa yakidini tuna ndoa ya kimila na mkuu nitakupataje hata contact hujatoa?
   
 12. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  sure, haki yaendana na wajibu! Judging after hearing one sided story huyo mama hafai hata kumlea mtoto! Ustawi wa jamii na mahakama wataamua!

  Women just like men r'nt saints!
   
 13. l

  lyt New Member

  #13
  Aug 28, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka pole sana nayaliyokupata.kuachana sio sulihisho kabisa kaka.chakufanya Mwombe M ungu akupe uvumilivu umalize masomo vizuri na utakaporejea mweke mkeo chini muongee kama marafiki atakueleza hela alifanyia nini inawezekana ulimuuliza kwa ukali au kunakitu anachokifanya kwa siri na hizo hela nikumsihii wote muwe wawazi katika maisha yenu mtaishi kwa amani.Suala la kutukana lazima liwe na sababu kwani kama mmeishi wote siku zote hajakutukana iweje sasa maybe ua the course men.kaeni myasuluishe kwa amani hatua mlofikia ni nzuri kimaisha haitapendeza kila mmoja awe peke yake na vlevle mtamnyima mtoto malezi bora.Kaka ukumbuke distance maranyingi inavunja mahusiano kilichopo kua mpole kama unampenda mkeo anza kujikomba kwakwe,jishushe kabisa kaka uanze kuirejesha amani ndo mengine yatadhihirika kaka hamna siri chini ya jua.ila kuachana sio suluhisho kabisa unaweza ukapata mwingine ambaye ni nyoka.shika sana ulichonacho kaka.hiyo hela isiwaachanishe mmetoka mbali sana
   
 14. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  nashukru sana kwa ushauri wako pia hata mimi sina ubaya naye ila tu kama nilivyoeleza kunitolea matusi hasa pale ninapotoa mchango nini kifanyike na kwa wakati gani nilijaribu kumuuliza kama mshahara hautoshi lakini hakujibu. Na kama kunakitu anafanya kina adhiri mpaka mtoto. Maana mtoto anatakiwa kusoma lakini yeye hatunzi hata hela ya ada ya mtoto. Nimemshauri aache shughuli zingine zote akipata mshahara atumie kwa chakula, matumizi ya kawaida na kumtunza mtoto wetu hasa katika swala la shule maana yuko kwenye shule za english medium lakini kinachofanyika ni kinyume natulivyokubaliana.
   
 15. Baba Ziro

  Baba Ziro Senior Member

  #15
  Sep 6, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huyo bwana hakufai tena, we nenda likizo kafuate taratibu zote za kimahakama kisha mpe talaka, wanawake hawana jema itakuwa ana mwanamme mwingine, pole sana ndugu yangu.
   
 16. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  na shukuru mkuu kwa mawazo yako maana ndoa siku hizi ni karaha wala sio raha kwa hiyo tuombeane nikifika nitajua lakufanya
   
 17. I

  IDUNDA JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2014
  Joined: Oct 31, 2013
  Messages: 458
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  bro, kutukanana tu kwenye ndoa ni sababu ndogo sana ya kuweza kuachana, nakushauri vumilia. matusi ni kitu kidogo sana rafiki yangu. mimi mke wangu hata akinitukana siwezi umiza kichwa sana labda kama kufumaniana hapo ndio kesi nyingine, kwani kwanza inategemeana amenitukana kwa sababu gani, pengine siku hiyo ameamka vibaya na ukizingatia umetuambia mama yake amefariki pengine inampa stress hivyo ukimgusa kwenye kovu analipuka. wewe ulipokuwa ulikuwa hutukani sijui ulikulia mazingira gani ambayo hayana challenges ndogondogo kama hizi, kama ulikulia maisha ya kijeshi kama sisi wengine unatukanwa unachapwa unanyanyaswa hadi inafika kipindi unakuwa sugu na kuweza kuishi maisha yeyote yale na kuishi na mtu yeyote yule ukammudu....hasa kutukanwa na mwanamke ni kitu kidogo sana na lazima kuna sababu iliyofanya akutukane. sisapoti kukutukana ila nasema hiyo sababu inavumilika kwa wanandoa na si sababu ya kuachana. kwa kifupi, kwa mwanaume aliyekamilika kiutu uzima na mwenye uwezo wa kukaa na familia, yote hayo uliyoyaongea ni ya kuvumilia na kurekebishana tu tena kwa maneno ya mdomo tu. ungeniambia umemfumania hapo nisingekuwa na la kusema kwani hiyo ingekuwa kesi kubwa, ila matusi tu? kwani kwenye maisha yako hujawahi tukanwa, uyo wife wako ndio wa kwanza kukutukana? amekutukana unataka kumuacha? unafikiri huyo utakayeenda kumuoa hatakutukana? kama sababu unayotaka kuachana na mkeo ndio hii, aisee utaacha na kuoa kuacha na kuoa hata mara 20.

  zaidi ya yote, mtu anayetukana sana hivyo sio yeye, ni shetani tu anamtumia, na pengine shetan ameona ndoa yenu ikiendelea mtafanikiwa sana sasa anataka akuachanishe ili mvurugikiwe wewe na mkeo na mtoto wenu.

  bofya hapa kwenye link yangu SHERIA KWA KISWAHILI
   
 18. K

  KIBONGOMKUTI JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2014
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 1,415
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Tafuta nauli umpeleke kwa TB Joshua huwa nasikia kuna mapepo uhenda ana pepo linamtuma akutukane ili ndo ivunjike liendelee kumfaudu peke yake.
   
Loading...